Shujaa Mwendazake
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 4,016
- 6,759
Nikiitazama hii picha,
Nikitazama video nyingine za mtuhumiwa Mbowe akihutubia taifa na sehemu mbalimbali ambazo kulikuwa na viongozi wa kitaifa, kiserikali,kitaasisi, kidini na kisiasa napata tabu sana kufikiri walikuwa hatarini kiasi gani IKIWA Freeman Mbowe alikuwa ni Gaidi kweli.
Walinzi wake inasemekana ni watuhumiwa pia, ilikuwaje bado Freeman alikuwa this much close na viongozi wa kitaifa kama tayari walinzi wake walikuwa suspects na yeye akiwa ni boss wao.
Pichani Mbowe pamoja na Mh Rais, Mkuu wa Majeshi, Mkuu wa jeshi la polisi na viongozi wengine wa kiserikali. Naweza kusema Mtuhumiwa wa Ugaidi akiteta na Rais wa Nchi!. Usiniambie hapo Mabeyo na Sirro ndo walikuwa wanamlinda Mh Rais, bali nao ni viongozi tu.
System ilikuwa down sana kipindi hicho. Hata Mtuhumiwa huyu alikuwa akiingia sehemu nyeti Bungeni kila uchwao. Hii kesi all in all inajudge mapungufu makubwa ya mfumo wa ulinzi katika awamu iliyopita.
Kazi na iendelee!