Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Morogoro, Barnabas Okola, amesema kikao cha wenyeviti wa mikoa kilichofanyika Agosti 13 kilitarajiwa kuhudhuriwa na viongozi 30, lakini waliohudhuria walikuwa 15.
Amesema katika kikao hicho baadhi ya wenyeviti waliibua hoja kuhusu tuhuma za Makamu Mwenyekiti, John Heche, kuhusu madai ya kuchukua michango ya chama na wadau bila kuiwasilisha kwa chama.
Okola amesema baadhi ya wenyeviti ambao hawakuhudhuria wanadaiwa kutoridhishwa na mwenendo huo, huku suala hilo likiongeza presha ndani ya chama na huenda likafikishwa katika Baraza Kuu.
Soma Pia:
Amesema Baraza Kuu linalotarajiwa kufanyika Septemba 15 linaweza kutoa mwelekeo wa suala hilo, ikiwemo iwapo tuhuma hizo zitajadiliwa rasmi na kuchukuliwa hatua ndani ya chama.