Tuiachie Serikali itoe majibu ya nani anahusika na shambulio la Lissu, msituchanganye wananchi

Nyani Ngabu

Hivi umemsoma anachokiongea?
CDM na wafuasi wake wameituhumus erekali na hasa bashite na kikosi chake, Yeye anakanusha sio kweli na anaweka ukwlei anao ujua yeye kuw ahiyo ni inside job au tukio alijatokea kabisa, maana nimeona anahoji hata matundu ya risasi kuw asio kweli pengine jama wamelipiga gari misumari mana matundu ya SMG hayawi vile.


swali kwako sasa:
Ni haki kwake kutoa huku , lakini wakitoa wana CDM na wengine ni kosa kwa fikra zako?
 

- Sikutaka kabisa kuligusa tatizo lake ila kwa matusi ya juzi nimeamua kuiliingia kichwa kichwa, ninasema ninasubiri warudi na habari yao kuhusu kilichotokea kwa sababu tayari kuna mambo mengi sana ambayo hayaingii kivhwani, ninategemea waje na habari yenye uhakika na evidence, that is all

le Mutuz
 
- Unasema yule mama wa watoto 3 ni mtoto mdogo anayetumiwa kumtukana Rais? Are you serious? Kazi yangu ni Social Media so relax I make money sio longo longo tu!

le Mutuz
i do respect kazi yako ya social media, sina tatizo na hilo....! tatzo unatumika vibaya brother.....hao wakuu wako (mtukufu na bashite ) wakifanya mission yao ikifeli ww ndio unatumika ku-dump their mistakes na kusawazisha ili upepo ukae sawa, kitu ambacho unakuja kuwa-attack upande wa pili kwa gharama yoyote ili mradi umewasafisha .....nikupe mfano kidogo tukio la pale clouds hadi ushahidi wa cctv camera ulikuwepo lakn ulitumika tena kutetea uovu na kupindisha ukweli kuwa uongo....anyway unatetea ugali wako sikulaumu !

Sent using Jamii Forums mobile app
 
- wanaolalamika ni Viongozi wa zamani na famailia zao maana mirija imefungwa, wananchi wa mtaani hawajawahi kuwa maisha bora zaidi ya waliyonayo sasa msiwasingizie hawana tatizo na Rais.

le Mutuz


All in all kiukweli nikikusoma humu napata picha Mkulu anafikiria nini na ukichukulia nyie ni watu wakaribu na washahuri wake, hakika kazi ipo!
na kikubwani hapo anapoanza kuona waliomtangulia ndio wabaya wake naamini ni kosa kubwa sana anafanya na pia its Bless kwetu wananchi na wasioutaka utawala huu, japo wapiganapo mafahari wawili ziumiazo ni nyasi.
 
FACTS: Uchunguzi unaanziaga na waliokuwepo kwenye tukio, hapo ni dereva na Lissu mwenyewe.... kitendo cha kuchukua muda mrefu kuwahoji watu hao wawili kinaweza kupoteza ushahidi.
Dereva angechukuliwa maelezo siku hiyo hiyo ingesaidia kupata details za muhimu sio kwa sasa ambavyo muda umepita anaweza kuwa amesahau important details ama ameshaongea na watu ambao wamekwisha mfundisha nini cha kusema na nini cha kukaa kimya ilimradi kesi ilalie upande fulani.
secondly, kitendo cha Lissu kupata fahamu Askari walitakiwa wawe pale kupata maelezo yake ya awali sababu zikiwa ni hizo hizo zilisotajwa kwa dereva. Tatizo ni jambo hili limebebwa kisiasa na kila mtu ameshahukumu na tupo blinded by our political affiliation lakini kuna possibilities kuwa hili jambo linazaidi ya siasa.
Na hata sisi waongeaji na wachambuzi wa mtandaoni tuongeee mpaka mwisho wa dunia hatuwezi kujua the whole truth sababu there only few people who have the privilege to that information.
Hata marekani hawajawahi kusema nani alimuua JF Kennedy, au kusema kama ni kweli uchaguzi wao uliingiliwa na Russia, au Uingereza kusema ni nani alimuua Princess Diana.
 
Kwani lemutuz anataka kusema nini?
Tukio liko staged ?
Maana naona mara alivaa shati blue,hii inasaidia nini kwa sasa?
Mgonjwa yuko mahuti huti,kweli unawaza alivaa shati gani?
Dereva wala lissu wala mbowe hawajasema lolote kuhusu kumtuhumu watu unao jaribu kuwatetea?
Hivi vita yako na mange unaleta jamiiforum home of great thinker?
Sidhani kama wewe lemutuz unaweza kuwa na fact zozote zaidi ya dereva au lissu?
Kama ukisema wewe ndo ulikuwa dereva kwenye Nissan nyeupe ndio njia pekee naweza kuamin fact zako ?
Nakama unajua zaidi,kwa nini usiwasaidie police?
Kwa umri wako na mambo yako am very sure baba yako ana udhunika akikaa akikuangalia..

HITIMISHO..
Uwezi shindana na tundu lissu hata apo kitandani alipo sasa...
Ridhiwani kikwete ni beyond your league..
Mange kimambi amekuzidi hadi followers..
Tafuta kazi nyengine,au uwe mc kwenye kitchen party..
 
Mdogo wako IPI alivyouwawa kwa sumu raisi hakuwa magufuli....listi inaendelea
 
Unajichanganya mwenyewe
 
Ila Nape alitishiwa risasi live je jeshi la police mpaka leo limejitokeza kusema yule alikuwa nani??mbona hawajasema mpaka leo??tuendelee kuamini maneno yao ya kusema oohh tusubirie wanachunguza??
hivi Nape alitishiwa risasi au bastola? lakini kule ilikua ni kutishiwa au kushurutishwa kutii amri halali. hizi akili za kuambiwa ni shida sana.
 
Kadri muda unavyozidi kwenda ndivyo tunavyoendelea kuwafahamu "WatuWasiojulikana"
 
Kufuatia post kwenye page ya mbunge wa kawe mh Halima Mdee na kisha Le Mutuz kuijibu hoja kupitia page yake ya instagram nakupa hapa "dots" kadhaa halafu mwenyewe utambue kinachoendelea au ukamilishe picha.

Dot #1. Program ya upimaji afya maeneo ya mnazi mmoja dar es salaam ilikua ikiratibiwa na mkuu wa mkoa wa dar es salaam.

Dot #2. Le Mutuz amekua akimtetea sana mkuu wa mkoa wa dar es salaam katika kashfa mbalimbali zinazokua zikimwandama, kwa maana nyingine amekua ni kama msemaji wake.

Dot #3. Halima Mdee hakutaja wazi identity nyingine zaidi ya kutaja jina "BASHITE"

Je, le mutuz anaweza kumweka wazi huyo mtu alokua akishiriki upimaji watu mnazi mmoja kwa siku tano?? Dhahiri huyo ndo BASHITE anayetafutwa.
 

Attachments

  • IMG_20170912_143717 (1).JPG
    41.1 KB · Views: 27
  • IMG_20170912_143650.JPG
    45.7 KB · Views: 36
Habari za muda huu waungwana, natumai muwazima na mnaendelea na shughuli zenu za kila siku katika kujenga taifa hili la Tanzania. Baada ya matukio kadhaa yanayoendelea kurindima na kushangaza watu wengi, kuna mambo kadhaa ambayo ningependa kushea na nyie.

Hivi kiukweli serikali inaweza ikawa inahusika na series ya matukio yoote haya yanayoendelea ikiwa ni pamoja na kumpiga Lissu risasi,kumpiga Meja Jenerali Mstaafu risasi,kuchoma moto kampuni ya mawakila ya IMMMA na kuiba nyaraka za Manji ndani ya kipindi hiki kifupi?
Na kama inahusika, inamaana inashindwa kupangilia mambo yake kistaha au kwa ustadi wa hali juu!! inamaana huyu bwana hana washauri wakumwambia "hapana,sasa unaharibu!"sidhani.
Ninavyoona nikweli mpango wa kumtoa 2020 upo na ndio upo katika kilele chake..huyu bwana huenda hatakiwi sasa wanamuharibia tuu ilimradi achafuke. Hayo ni mawazo yangu....

Lissu hakuwa tishio kwa serikali,kwa nionavyo mimi Lissu alikua mtoa maoni tu tena mshauri mzuri tu (japo kwa kashfa muda mwingine), sasa sijui nani anaweza kumuua mtu kisa anabisha kila kitu. Nahisi kuna watu wapo kutengeneza haya madizasta yoote ilimradi aidha Tanzania ichafuke au wapite kiurahisi 2020 na kikubwa "hawa watu wana hela na pengine waliishi kama wafalme kabla ya 2016 na sasa wanaishi kama mashetani"

Tusubiri tuone....
 
"Husika" maana yake nini?
 
Mkubwa Tundu lissu alikuwa tishio kwake maana alikuwa mkosaaji wake mkuu hata alikuwa hana ubavu wa kuzijibu hoja zake na hata washauri wake walimgwaya Tundu Lissu,Mahakamani Majaji walikuwa hoi mbele yake na huko Bungeni spika aliambiwa awashughulikie wapinzani kwa kuwafukuza ili waje waropokee huku uraiani ili Bwana mkubwa awakomeshe hata hivyo alishindwa. Sasa kukawa hakuna namna bali kutumia gari kumfatilia na mwishowe WASIOJULIKANA wakafanya mambo yao!!!!Hivyo amini usiamini Tundu Lissu alikuwa mwiba kwa serikali ya awamu ya tano!!!!!
 
Hakuna serikali duniani ambayo haifanyi ujasusi kwa

nza,pili hakuna serikali inayoweza kufanya ujasusi kishamba hivyo. Tatu mpango wa kumtoa ni kweli upo ila mbona kama unakosekana umakini!sababu gani watu hao hawajawahi kuwa tayari kdadisi,kujifunza na niwavivu kufikiri. Matokeo yake wamekuwa wapiga kelele za mdomo badala ya vitendo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…