Sasa tuna tarehe rasmi ya kuanza mafunzo, weka historia, wahi kujiandikisha uwe katika batch ya mwanzo.
Mafunzo ya ufundi uashi (masonry) Kwa vitendo (hands on training) yanatarajiwa In shaa Allah kuanza kutolewa kuanzia tarehe 1 February 2021 kwa wiki nne mfululizo.
Mafunzo hayo yatakuwa ya Vitendo zaidi na yatajumuisha...
1. Kufundishwa na kutambua majina ya bidhaa na vifaa mbali mbali vya kazi za uashi (masonry) na matumizi yake.
2. Mafunzo ya vitendo jinsi ya kuchanganya mchanga, saruji, kokoto, maji, na uwiano wake (ratios).
3. Utunzaji wa bidhaa wakati wa uzalishaji na baada ya uzalishaji.
4. Kuponya uzalishaji (curing) na uhifadhi wa vifaa na Bidhaa.
5. Matumizi ya bidhaa yaani kutengeneza muundo wa sampuli za ujenzi majengo kwa vitendo.
6. Matengenezo madogo na utunzaji mashine za kuundia bidhaa za ujenzi (repair and maintanance).
Na maswala mengine ya uashi na ya kiufundi yatayojitojeza.
Pia kutagusiwa
Uuzaji wa bidhaa utazojifunza kuzalisha na jinsi fundi mwashi anavyoweza kutambua fursa za soko ya kazi yake.
Nyote wenye ndugu jamaa na marafiki wenye kupenda kujifunza ufundi, walio na kazi na wasio na kazi , fursa hiyo.
Mafunzo ni kwa wote, wanawake na wanaume.
Mafunzo yatatolewa bure bila malipo na posho ya kujikimu wanaojifundisha itatolewa kwa kipindi chote cha mafunzo. Ma shaa Allah.
Kwa maelezo zaidi Wasiliana na Abdul Ghafur 0625249605.