Uchaguzi 2020 Tuikomboe Tanzania kupitia Lissu, hakuna nchi Duniani ina mifumo miwili ya lugha za kufundishia

Uchaguzi 2020 Tuikomboe Tanzania kupitia Lissu, hakuna nchi Duniani ina mifumo miwili ya lugha za kufundishia

Tatizo la Tz sio suala la kutumia lugha mbili, bali ni umahiri wa waalimu wetu ktk masomo yetu iwe kiswahili au kiingereza na masomo mengine ya kitaaluma iwe Biology, geography n.k .

Anti na kusoma kwake kwa kinyaturu, kuwa lawyer, na kuwa mbunge miaka yote ameshindwa kujua matatizo ya Elimu Tz , mpaka juzi alipokwenda Ubelgiji?

Je amejaribu kupita ktk shule za wenzetu na kuona miundo mbinu yao na qualification za waalimu wao ?? Hata wa Shule za Primary , jina la Mwl Mkuu na Qualification zake huwa wanaweka ktk Bango nje ya Shule.

Au amuone Mbatia wa NCCR atampa Shule , maana tatizo naona linaanzia na Yeye.
 
Naupenda huu mjadala juu ya lugha ya kufundishia katika mfumo wetu wa elimu. Tunahitaji kujadiliana vizuri jambo hili muhimu. Lakini Lissu hafai kuwa Rais wa Tanzania. Nafuu hata prof Lipumba.
 
Humu kinachotuumiza ni ushabiki kuliko uhalisia,watu wengi wanaonekana kumjadili TL kuliko kujadili alichosema.Lugha mbili zinazotumika Tanzania kama lugha za kufundishia zina mdhara makubwa katika mstakabali wa elimu yetu.

Mm ni mwalim ,wanafunzi kuanzia msingi wanafundishwa kwa lugha ya kiswahili miaka nane au tisa kuazia chekechea mpaka darasa la saba.Kiswahili anafjndishwa kama somo ila sio kama lugha ya kupata maarifa.

Akienda form one anakuta masomo yote aliyo yasoma primary lugha ya kufundishia ni lugha ya kingereza ,sasa anaanza kupata shida kuelewa lugha alafu ndoo aelewe content iliyomo.Kiswahili kinabaki kama somo kama ilivyokuwa kingereza wakati akiwa msingi.

Kinachofuata sasa kwake ni kuanza kuyakariri kama yalivyo kwa kuwaya lugha hailewi kuyaelewa ,sasa ni wachache wanaoweza kukakariri ndio wanaofaulu mtihani na walioshindwa kuyakariri wanafeli kabisaaa.

Lakini serikali hiyo hiyo imeleta ubaguzi imerihusu shule za private zitumie kingereza lufundishia wanafunzi msingi ili wakifika sekondari wakutane na lugha wanyoijua na hawatakariri kama hao wengne ,lakini ikakubali watanzania waliowengi na wanyonge waende sekondari washindwe hiyo lugha mpya kwao wanaona ni burdani .

Ushauri tutumie lugha moja hasa kingreza kwa kuwa sisi hatujawa na uwezo wa kutengeneza vya kwetu kama ilivyo China,Japan na Urusi ,sisi tunatumia vilivyotengenezwa ambavyo lugha ni kingereza.Walimu wapigwe msasa wa elimu ya msingi waanze kufundisha kwa kingerza ,tutaona mabadiliko baada ya miaka kumi au ishirini.
 
Ujaelewa kinachozungumzwa.Jipe muda wakujielimisha utaona hoja ya msingi ilipo,hixo ccm yako ndiyo iliyotufikisha hapa.Kila miaka tunabadili mifumo ya ufaulu kwenye elimu yetu hiyo yote nikwasababu mfumo wetu waelimu niwa ovyo ila serikali ya ccm imeshindwa kuja na mwarobaini.Hoja ya lissu nikusuka upya mfumo waelimu utakaokua umekidhi mahitaji ya kila sekta kuanzia elimu ya awali hadi chuo kikuu.Na ninajambo rahisi sana kukiwa na dhamira yakufanya hivyo.
Mfumo wa kutumia lugha moja tu ya kiingereza kufundishia katika elimu yetu hauwezi kuwork katika shule zetu..
 
Mfumo wetu wa elimu ni mbovu kupindukia na walioongoza nchi toka uhuru wameshindwa kabisa kuusuka uendane na mabadiliko ya dunia.Serikali inaongelea swala la nchi kujitegemea kwenye majukwaa ya siasa uku hawajui ili nchi iweze kujitegemea lazima uanze kwanza kua na mfumo wa elimu utakaokuzalishia wasomi wabunifu,wasomi watendaji katika nyanja zote,watakao kua mahiri kwenye uchumi,afya,ufundi,kilimo,biashara,mapinduzi ya viwanda namengine.
 
Kingereza kinapewa ukuu kwasababu ya mfumo uliopo.Hizo nchi toka mfumo wao wa elimu unaaanzishwa waliweka lugha zao kwanza ila sisi nikama hajutui kipi ni kipi.Kwahiyo ili kukifanya kiswahili kufika uko ni lazima tusuke upya mfumo wetu na kukisuka upya kiswahili ili kiendane na hali zote kuanzia matumizi ya kawaida hadi kufundishia.Uko nyuma kulikua na mabaraza kama BAKITA kwaajili ya kiswahili sasa hivi sijui kama yapo au yanafanya kazi kusudiwa kwasababu nikama kiswahili kimeachwa kijisimamie chenyewe kitu ambacho kwa mfumo uliopo ni ngumu.Na ukumbuke kwamba mfumo unakiona kingereza ni rahisi zaidi kutumika na kufundishia kuliko kiswahili.
mweongo,

Mi nafikiri jitihada zizingawe kukikuza kiswahili zaidi siku moja kiswahili kitumike kufundishia pia. Tunakipa ukuu wa bure tu icho kiingereza, kuna nchi zna lugha zao wenyewe na zimeendelea pakubwa tu
 
Kwa dunia ya leo lugha sio kigezo cha kumkwamisha mwekezaji kuwekeza na kupata matokeo chanya. Lissu mwenye amekaa Ubelgiji miaka 3, je alikuwa anaongea kifaransa, ki datchi au kijerumani? Kama unataka kuongea kiingereza au lugha yoyote ile ni juhudi zako mwenye zitakusaidia na utaongea tu.
Shida sio kuongea kinge, shida ni kuwa mwanafunzi hawaelew wanachofundishwa shuleni. Mtu anatakiwa also english waikati huo huo masomo mengine yanafundishwa kwa kiengereza!

Tuwe na lugha moja tu tokea chekechea mpaka chuo, km ni kiswahili bas ni mwanzo mwisho na ndo wachina wanafanya hivyo na english huwa somo la giada. Like wise kwa kiengereza.

Watu wanapata changamoto mavyuoni including myself. Kwahiyo tuchague lugha moja, english au swahili. SWALI NI, KISWAHILI KINAJITOSHELEZA KUFUNDISHIA MASHULENI NA CHUO KIKUU KAMA WACHINA WANAVOFANYA?
 
Mbona unaongea kama vile watu wote wanaishi daresalam au watu wote wana uwezo kifedha.Lugha ni zaidi ya kuongea na kuandika.Lugha ndo msingi wa maendeleo nahili sio jambo jepesi jepesi kama unavyolichukulia.
Ndio maana nikasema ukiweka juhudi, unaweza kujifunza lugha yoyote unayotaka duniani. Darasa linakupa mwongozo tu, lakini ukitaka kujua kitu kiundani ni juhudi zako.
 
Mnyonge mnyogeni haki yake apewe, Lisu leo amenigusa kwenye swala la lugha ya kufundishia. Jambo hili limekuwa mwiba kenye elimu na maisha ya Watanzania miaka na miaka.. Ni ukweli usiofichika kwamba lugha ya kufundishia ni tatizo kubwa sana kwenye mfumo wetu wa elimu. Magufuli mwenyewe ni mhanga Mawaziri wetu ni wahanga, Wabunge ni wahanga. Tuunge mkono chadema vijana wetu wapone...
Hivi mna uhakika na hayo myasemayo?
 
Unatoa mifano ya nchi ambazo kuanzia mazingira ya mwalimu,mwanafunzi na shule yenyewe yako vizuri.Hebu itazame tanzania alafu niambie hicho ulichokiandika kama kinawezekana hapa bongo kwa hali iliyopo sasa.Kwasababu hapa changamoto sio uwezo mdogo tu wa mwalimu kufundisha bali ata mwanafunzi mwenyewe anaweza kau na uwezo mdogo kutokana na changamoto kadha wa kadha zakimazingira,lishe n.k.
Wewe ni muongo. Kinacho kusukuma kwenye thread hii ni ushabiki wa party politics kuliko ukweli. Kwanza, siyo kweli kwamba hakuna nchi duniani yenye lugha tofauti za kufundishia. SIYO KWELI. Nitakuwa mifano michache...
 
Mnyonge mnyogeni haki yake apewe, Lisu leo amenigusa kwenye swala la lugha ya kufundishia. Jambo hili limekuwa mwiba kenye elimu na maisha ya Watanzania miaka na miaka.. Ni ukweli usiofichika kwamba lugha ya kufundishia ni tatizo kubwa sana kwenye mfumo wetu wa elimu. Magufuli mwenyewe ni mhanga Mawaziri wetu ni wahanga, Wabunge ni wahanga. Tuunge mkono chadema vijana wetu wapone....
Lugha ni bidhaa.
Lazima kama nchi tuwe na export nyingi kuliko imports ili tuwe na sababu ya kutumia lugha yetu ktk biashara ambapo mazingira ya watu wanaotuhitaji kibiashara ni makubwa.
Lazima tuwe na Ufumbuzi mwingi na uzalishaji mkubwa wa kiushindani na kisayansi.

Research centres na program za ufumbuzi zikiongezeka ndiposa kuanza kupaisha kiswahili kibuashara.

Sekta ya Kilimo na Mifugo na uvuvi ikipata uwekezaji mkubwa na wa kisayansi hapa Nchini-Kiswahili kitapata soko kubwa sana na huu ndiyo mitizamo sahihi kuhusu Kiswahili.
 
Ni muda mchache uliopita tumemsikia mgombea flani akizungumza kilugha kwa utetezi kua wenyeji wa hilo eneo hawajui vizuri kiswahili.Sasa kwa hali kama hiyo unaona jinsi gani kama nchi hatujui lakufanya kuhusu kiswahili chenyewe,au hicho kingereza pamoja nakuboresha mfumo wetu wa elimu.
 
Kwa dunia ya leo lugha sio kigezo cha kumkwamisha mwekezaji kuwekeza na kupata matokeo chanya. Lissu mwenye amekaa Ubelgiji miaka 3, je alikuwa anaongea kifaransa, ki datchi au kijerumani? Kama unataka kuongea kiingereza au lugha yoyote ile ni juhudi zako mwenye zitakusaidia na utaongea tu.
Acha upumbav shenzy
 
Mnyonge mnyogeni haki yake apewe, Lisu leo amenigusa kwenye swala la lugha ya kufundishia. Jambo hili limekuwa mwiba kenye elimu na maisha ya Watanzania miaka na miaka.. Ni ukweli usiofichika kwamba lugha ya kufundishia ni tatizo kubwa sana kwenye mfumo wetu wa elimu. Magufuli mwenyewe ni mhanga Mawaziri wetu ni wahanga, Wabunge ni wahanga. Tuunge mkono chadema vijana wetu wapone....
Uganda wanatumia lugha za kienyeji na kiingereza. Kama huijui dunia, nyamaza! Unashabikia u-maimuna wa Lissu!
 
Mnyonge mnyogeni haki yake apewe, Lissu leo amenigusa kwenye swala la lugha ya kufundishia. Jambo hili limekuwa mwiba kenye elimu na maisha ya Watanzania miaka na miaka.. Ni ukweli usiofichika kwamba lugha ya kufundishia ni tatizo kubwa sana kwenye mfumo wetu wa elimu. Magufuli mwenyewe ni mhanga Mawaziri wetu ni wahanga, Wabunge ni wahanga. Tuunge mkono chadema vijana wetu wapone.

Magufuli huongea kwa kiswahili na kuhubiri kukuza kiswahili si kwamba anakipenda sana. sababu kubwa ni kwamba hajui English vizuri, Ingawa alikua mwalimu na PHD aliandika kwa kizungu. Yeye mwenyewe ni mfano mzuri wa halihalisi na shida tuliyonayo kwenye elimu yetu. Lakini cha kushangaza hajachukua hatua kundoa shida hii inayoliamiza tafa. Tundu lisu ameona tatizo na yupo tayari kulitatua.Tumunge mkono Lisu tuiokoe Tanzani.

Kwenye hili la elimu tuambiane ukweli. Hatutaendelea kwa kuhimiza vijana wawe wamachinga, wajaze mitaa wakichuuza vitu vya mchina wakati maduka yapo. Leo Barabara, Reli nk ni wageni wanajenga. kwani nani alienda kujenga Reli China au Korea? Kijana akitoka na zero form 4 utampeleka wapi? CCM imetuangusha kwa tangu Uhuru. Tanzania tunahitaji mabadiliko.

Vijana wetu wengi wanashindwa kupata maarifa ya kutosha mashuleni na vyuoni kwa sababu tu hawaelewi lugha inayotumika kuwafunza. Mfano;mtihani wa kitato cha 4 si mgumu kiasi cha zaidi ya nusu ya wahitimu kupata alama (division) 4 na 0.

Wawekezaji wakija Tanzania wanashindwa kupata wafanyakazi wanaoweza kuwasilana nao vizuri na wenye weledi na marifaya ya kutosha kwenye lugha. Matokeo yake wanaamua kuajiri Wakenya kwenye nafasi za juu. Uliza Managers kwenye makampuni makubwa hapa kwetu ni akina nani. Tunge mkono Lisu Tupate Tanzania mpya.

Tanzania itaweza tu kusonga mbele endapo tutaamua kuborosha elimu yetu itowe wasomi wenye viwango vya kimataifa na sio kupelka watoto shule kwa mazoea tu lakini watoka watupu.

Hakuna nchi yoyote Duniani amboyo ina mifumo miwili ya lugha za kufundia kama ilivyo kwa Tanzania. Wanachi waliona tatizo hilo wakamua kuazisha shule zinazofundisha kwa Kingereza ili kuziba pengo, hivyo Tanzania hakuna watoto wanafunzwa kwa Englishi na Wale wa Kiswahili.

Tundu Lisu na Chadema ameamua kulivalia njuga swala hli tumuunge mkono.
Katika elimu yetu pia sasa hivi turudishe au tuweke mitaala ambayo itatuwezesha kuhifadhi culture yetu , iwe kucheza sindimba, aka nana na ngoma nyinginezo na hiyo isijalishe kabila la mtu bali huyo mtu awe anaishi eneo hilo kwenye ngoma hiyo, na hiyo elimu itolewe kwenye elimu ya msingi, akifika secondary ndio aanze huo utamaduni wawengine
 
Watu kama wewe ni aibu kwa Taifa. Ni hasara na fedheha.

Mnafaa mfungiwe mawe mazito shingoni mtupwe kwenye kilindi cha bahari ili mliondolee taifa letu zuri laana ya ujinga.
Safi saana matusi kwenu ndo ilani ya uchaguzi mwaka huuu. Mkiongozwa na kile kiwanda chenu cha matusi kinachotafuta ikulu
 
Tatizo Bongo watu ni vilaza mno, kila kitu wanataka Serikali ndio ifanye yani mtu hawezi ata kujiongeza, rafiki yangu yero ameondoka kama mwaka tu ameenda Zanzibari Nungwi, amerejea kama week hivi wote tumeshangaa jamaaa masai anaongea lugha tatu, kiengereza kitaliano na kispanyola na shule hajawahi kwenda, endeleeni kupumbazwa na Lissu.
 
Back
Top Bottom