The Assassin
JF-Expert Member
- Oct 30, 2018
- 5,082
- 20,806
Mimi ni moja ya watanzania waliobahatika kuzaliwa kati ya moja ya mbuga ya wanyama maarufu sana hapa Tanzania na Duniani kwa ujumla. Miaka nakua mimi tulikua tunaishi Mbugani baadae tukaja kuondolewa, hivyo wanyama karibu wote nimekua nikiwaona kwa macho yangu, hivyo ningetamani huo urithi kuwarithisha watoto na wajukuu zangu.
Miaka ya hivi karibuni ujangiri ulishamiri, hadi watu wakawa wanaitwa malkia wa pembe za ndovu, malkia wa tembo kwa sababu ya umaarufu wao wa kuua tembo, faru, viboko, twiga na mbaya zaidi hadi twiga wakawa wanapandishwa ndege kwenda nje ya nchi. Hii hali ilikua inatishia kuondoa kabisa urithi wetu, watoto wetu wangekuja kuwaona faru kwenye tv au kulipia kwenda kuwaona ulaya.
Nashukuru Serikali ya awamu ya 5 ilichukua njia ngumu ya kupambana na ujangili. Mimi binafsi niliungana na kauli ya waziri wa maliasili aliposema akimkuta mtu kaua tembo anamuua, mimi nisingemuua tu, kwanza ningempiga pipe kabla ya kumuua. Haiwezekani ubinafsi na tamaa ya watu wachache watumalizie urithi wetu, haikubaliki.
Serikali ya Magufuli iliamua kuwashughulikia waharamia kwa njia za kijeshi, ukikamatwa mbugani basi unabadilishwa jina, inakua ndio mwisho wa ndugu zako kukuona. Wale maharamia wa kienyeji wale wanaoua wanyama kwa ajili ya nyama tu wale ni miaka 30 jela. Hii mbinu imepunguza sana kama sio kumaliza ujangili wa kimataifa nchini. Hongera sana wizara ya maliasili na serikali kwa ujumla.
Binafsi kwa hili naipongeza sana serikali.