Tuisaidie JF yetu, tusambaze elimu ya matumizi ya VPN

Club Mate

Member
Joined
Aug 1, 2025
Posts
29
Reaction score
125
Wakuu,

Inaonekana platform yetu pendwa bado imezuiliwa ingawa kifungo hicho kiliondolewa rasmi zaidi ya mwezi mmoja sasa. Bila VPN hutoboi...

Tuunganishe nguvu zetu ili kuwafahamisha watu wengi zaidi jinsi ya kuingia JF, kama jinsi akina Erythrocyte walivyopotea mwanzoni, yaani tuhakikishe kila mtu anajua, au vipi?

Nimefikiria kwenye posti za mitandao ya kijamii ya JamiiForums hasa zile ambazo zinakuwa na watu wengi, tukoment "Kwa nini jamiiforums.com haipatikani?". Tukiona mtu tayari ameuliza, tumjibu kuwa anahitaji kutumia VPN kuingia kwenye jukwaa na tumpe maelekezo ya jinsi ya kupakua na kuiseti.

Ikiwa yote mawili tayari yamefanyika, basi tu-like na kuzipush comments hizo.

Tufanye hii iwe kampeni, tusiwaruhusu hao mboga watufungie bila maelezo!

Halafu, hivi kwanini tusiende kwa wingi kwenye page ya TCRA kuwauliza kwanini wanatunyima kupata JF wakati kifungo chao kiliisha?
 
Proton na Cloudflare zipo Playstore kila mmoja apate hizi yaani ni kutelezaa tu
 
Unamfahamisha vipi mtu kuwa mimi naingia jf kwa kutumia vpn ili hali ukiwa mtumiaji wa jf wewe mojakwa moja utakuwa unatumia kwa kificho? Kila mtu apambane kivyake.
 
Wazo zuri sana 👍🏾 kuna VPN nyingi za bure kama Turbo, X na zingine zimenisaidia kupata access ya jukwaa💪🏾🔥unaweza ku-download ukawa nazo kwenye simu yako
 
Fafanua hapa
Jinsi ya Kutumia VPN kwenye Simu (Proton VPN & Cloudflare WARP)

Proton VPN
  1. Pakua App
    Fungua Play Store au App Store
    Tafuta: Proton VPN → Pakua
  2. Fungua App
    Chagua Continue as Guest (bila kufungua akaunti)
    Au unaweza Sign up ukitaka huduma zaidi.
  3. Unganisha (Connect)
    Bonyeza Quick Connect
  4. Ruhusu VPN
    Bonyeza Allow ikikuuliza
  5. Ukiona Connected — VPN iko ON
  6. Kuzima, Bonyeza Disconnect

Cloudflare WARP
  1. Pakua App
    Tafuta: 1.1.1.1: Faster Internet
  2. Fungua App
    Kubali ruhusa zote (Allow permisions)
  3. Washa WARP
    Bonyeza ON
  4. Ukiona WARP Connected — uko salama
  5. Kuzima Bonyeza OFF
 
Lets do this wana JF, Sauti ikiwa kubwa huwa wanalegeza, Tunaoenda kwenye page za TCRA kuwasalimia tufahamiane hapa :Alarm::Alarm:
 
Wakuu,

Inaonekana platform yetu pendwa bado imezuiliwa ingawa kifungo hicho kiliondolewa rasmi zaidi ya mwezi mmoja sasa. Bila VPN hutoboi...

Tuunganishe nguvu zetu ili kuwafahamisha watu wengi zaidi jinsi ya kuingia JF, kama jinsi akina Erythrocyte walivyopotea mwanzoni, yaani tuhakikishe kila mtu anajua, au vipi?

Nimefikiria kwenye posti za mitandao ya kijamii ya JamiiForums hasa zile ambazo zinakuwa na watu wengi, tukoment "Kwa nini jamiiforums.com haipatikani?". Tukiona mtu tayari ameuliza, tumjibu kuwa anahitaji kutumia VPN kuingia kwenye jukwaa na tumpe maelekezo ya jinsi ya kupakua na kuiseti.

Ikiwa yote mawili tayari yamefanyika, basi tu-like na kuzipush comments hizo.

Tufanye hii iwe kampeni, tusiwaruhusu hao mboga watufungie bila maelezo!

Halafu, hivi kwanini tusiende kwa wingi kwenye page ya TCRA kuwauliza kwanini wanatunyima kupata JF wakati kifungo chao kiliisha?
Lets do this wana JF, Sauti ikiwa kubwa huwa wanalegeza, Tunaoenda kwenye page za TCRA kuwasalimia tufahamiane hapa
 
Wakuu,

Inaonekana platform yetu pendwa bado imezuiliwa ingawa kifungo hicho kiliondolewa rasmi zaidi ya mwezi mmoja sasa. Bila VPN hutoboi...

Tuunganishe nguvu zetu ili kuwafahamisha watu wengi zaidi jinsi ya kuingia JF, kama jinsi akina Erythrocyte walivyopotea mwanzoni, yaani tuhakikishe kila mtu anajua, au vipi?

Nimefikiria kwenye posti za mitandao ya kijamii ya JamiiForums hasa zile ambazo zinakuwa na watu wengi, tukoment "Kwa nini jamiiforums.com haipatikani?". Tukiona mtu tayari ameuliza, tumjibu kuwa anahitaji kutumia VPN kuingia kwenye jukwaa na tumpe maelekezo ya jinsi ya kupakua na kuiseti.

Ikiwa yote mawili tayari yamefanyika, basi tu-like na kuzipush comments hizo.

Tufanye hii iwe kampeni, tusiwaruhusu hao mboga watufungie bila maelezo!

Halafu, hivi kwanini tusiende kwa wingi kwenye page ya TCRA kuwauliza kwanini wanatunyima kupata JF wakati kifungo chao kiliisha?
Naomba maelekezo kwenye computer nafanyeje kuipata jamii forum? Hiyo vpn naisetije??
 
Kutumia VPN wanasema ni kosa kisheria
hapana, kutumia bila kibali ndo kosa --- wanataka ujaze fomu ya maombi ya kutaka kutumia vpn ukiwa umetaja sababu za kutaka kutumia, na kuanisha vifaa utakavyotumia hiyo vpn na detail zake

uamuzi ni wako hapo --- ila kimsingi ni utapeli mtupu
 
Back
Top Bottom