Tuisaidie Taifa Start ili nchi isipate aibu!

Tuisaidie Taifa Start ili nchi isipate aibu!

Mara ya mwisho mimi kujishighlisha na timu za bongo ni wakati Micho akiwa kocha wa Yanga. Toka wakati huo hadi leo si Yanga wala Taifa Stars nawafuatilia.

Nasikia jana mmepigwa tena, kichwa cha mwenda wazimu. Mtamkumbuka Tenga.
 
Walipocheza Starz,na Mozambique nilishangilia Mozambique, mlisema mimi sio mzalendo.!!Hata Leo ningeiona hiyo game ningeshangilia hao Madagascar inaonekana inaujua mpira.

Presha aliyonipa Moyes mwaka Jana yatosha!!

siku starz ikicheza naangalia clips za Gaucho na Zidane, napata satsfication nzuri kuliko nyie mnaoangalia stars.


In short mpira sio fani yetu,tuuvumbue mchezo mwingine tu

Watanzania wanapenda mpira sana ila hatuna team zenye weledi wa kutupa furaha.
 
Hatua ya kwanza ni kumuondoa Malinzi,then kufukuza huyo kocha aliyemleta.Si kweli kwamba hatuna wachezaji wazuri Maximo alipata mafanikio na kina Tegete,Ngasa,Nizar,Maftaha,Nditi,Nyoni,Boni,Nsajigwa,Mapunda,Yondani iweje hawa wa sasa wanafungwa kila siku

Safi kabisa. Kufukuza kocha ni kutibu homa badala ya ugonjwa wenyewe. Homa ni dalili tu. Malinzi out.
 
Kwanza huyo Jamal Malinzi aondoke kabisa TFF akatafute kazi nyingine za kufanya, hana ubunifu, hana mawazo, hana ujanja, haijuwi soka, hawezi kuiendeleza soka hata awepo hapo miaka 100.

Sijuwi hao waliomchaguwa walikuwa na kigezo kipi kilichowafanya wachaguwe.

cc Bishanga

Jamani alibuni jezi mpya
 
Last edited by a moderator:
Kila mashindano hakuna tunachokiweza. Miaka 30 na zaidi tangu timu ishiriki kombe la afrika. Ikiwezekana em timu ya taifa ipumzike kwanza kushiriki mashindano ijijenge hata kwa miaka 3 alafu tuone inakuwaje.
 
Kwa Taifa Star hii, tutaondoka na kapu la magori katika mechi za kufuzu Afcon.

NOTE: Misri, Nigeria, Chad tupo nao kundi moja.
 
Kipigo cha Taifa Star na Swailand 1-0 na kisha dhidi ya Madagascar Cha 2-0. Kimenifanya nitafakari sana na kukumbuka misemo ya Wahenga isemayo midomo uumba.Na hasa kauri za watu wazima [Wazee].

Kauli ya Rais Mstaafu Mzee Ally Hassan Mwinyi mmoja ya viongozi wenye busara za hali ya juu kuwahi kutokea Tanzania, alisema; "Soka ya Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu, kila mtu anajifunzia kunyoa".
Mzee Mwinyi alisema hayo, baada ya klabu ya Simba kufungwa na Stella Abidjan mabao 2-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika fainali ya Kombe la CAF mwaka 1993. Na ninakumbuka aliwahi kurudia kusema hivyo; "Soka ya Tanzania bado kichwa cha mwendawaimu,", baada ya kushuhudia matokeo mengine mabaya.

Kauli hii nzito ambayo imekuwa kinywani mwa maisha ya Watanzania..toka ilipotolewa na kuendelea kuwa nukuu kila mara timu ya Taifa inapopokea kipigo toka kwenye timu za mataifa mengine, kauri hiyo imenifikilisha sana na kunipa muda wa kuona mimi kama Mtanzania nina sehemu gani katika kuona Taifa Star inatokana na kauri hiyo.

Watu wazima na viongozi wa dini watanielewa kwa haya nitakayosema ''MIDOMO YETU INAUMBA'' ndio kusema midomo ya Mzee Wetu Mwinyi nayo imeendelea kuumba.

Kilichotokea Kwa Kauri ile, ilikuwa ni matamanio ya Mzee Mwinyi kuona Taifa Star inashinda mechi zake kimataifa,lakini kila iliposhiriki matokeo iliyoleta nyumbani yalikuwa hayamfurahishi Rais Mwinyi [Kama Baba Mwenye Nyumba-Tanzania] kwa kipindi hicho kama Rais wa Tanzania.Katika kuonyesha hisia yake hiyo akajikuta anatumia misemo ya WAHENGA wake [WAZEE WALIOTANGULIA KUASISI KAURI HIZO] kuwa Tanzania ni kama kichwa cha mwendawazimu ambae kila anaetaka kujifunza basi wake mkasi atanyoa kadri jiko lake litakavyoona.

Wakati kauli hii inatoka nilikuwa kinda sana...1993...na leo ni Baba wa Watoto kauli hii imeendelea kuwa MWIBA wa UKWELI wa maisha yetu Watanzania katika mpira wa soka.

Binafsi nimeshawishika kujiunga na baadhi ya Watanzania kushauri yafuatayo, na kuwaomba wafuatao;

1: RAIS MSTAAFU MWINYI NA MARAIS WENZIE;

Kujiandaa kuwapokea Taifa Star wa leo pale atakapofuatwa na Watanzania kwa ajili ya ushriki wake katika kuufanya moyo wake kama ilivyo miyo ya Watanzani wengi wanavyokwaza na matokeo ya Taifa Star, kukubali KWA UMOJA wetu tubadilishe AKILI YETU na kuanza kuwa na MIOYO YA KUIONA SI KICHWA CHA MWENDAWAZIMU bali MKUKI WA MASAI WA KITANZANIA KUKABLIANA NA SIMBA YOYOTE YULE.

Kwa kauli mpya maalumu kinywani mwa Rais huyo Mstaafu kuomba akiwa na Wazee, Viongozi wa Kidini, Na Wanamichezo wa Tanzania pamoja na Wapenzi wa Michezo Tanzania kauri itakayomtoka iwe ''TAIFA STAR NI MKUKI WA WATANZANIA KUWASHINDA WASHINDANI WETU WOTE KWENYE MCHEZO HUO''.Tamko ilo liendane na ishara za vitendo katika tukio [Event] maalumu kuwakabidhi wachezaji walioko katika tukio hilo kila mmoja MKUKI WAKE huku wao wakimkabidhi MIKASI ambayo atashirki kuichoma MOTO ishara ya kuonyesha UMIKASI tuliokuwa tunanyolewa nayo umekwisha sasa tutakuwa washambuliaji kwa ASILI YA KIMASAI kumkabili mnyama yoyote.

2: CHAMA CHA SOKA [TFF] NA SHRIKISHO LA MICHEZO TANZANIA [BMT]

Kuanda tukio [Event] maalumu litakalo tumika kama tukio ka kihistorai maalumu kwa ajili ya Mzee Mwinyi kushiriki katika tukio hilo kufanya ishara maalumu ya ufutaji wa Kauri hiyo CHUNGU kwa Watanzania wote wapendao soka la Tanzania.
TFF na BMT kwa umoja wao waandae Tamasha ilo maalumu litakalo ratibiwa nao katika moja ya siku za mwisho wa jumaa yani Jumamosi [Saturday] kwa kuanda Tamasha ya Mechi ya Kirafiki Kusindikiza tukio hilo Maalumu ambalo Mzee Mwinyi atalifanya Kabla Ya Mechi husika ya kirafiki Katika Uwanja Mpya wa Taifa.Mzee Mwinyi akiongozwa na Rais Jakaya Kikwete, Mzee Mkapa, Wazee wapige dua la Asili, Viongozi wa Dini zote nao Wapige Dua zao kwa ajili ya kuomba Baraka za Ushindi ili iwe ni tangulizo la kiimani kila mara timu zetu hasa Taifa Star zinaposhrikia michezo n mataifa mengine.

Mechi hiyo ya Kirafiki ni Timu ya Taifa Star Wadogo Kwa Wakubwa Wakike na Kiume zote kufanywa Mseto mmoja na kisha Kugawanywa mara mbili kisha kushindana zenyewe.Mechi hii ikawe chachu ya ushindi daima.Refa wa mechi hizo wanaweza kuwa ni viongozi wa kidini toka kwenye mseto wa imani.

3:VIONGOZI WA KIDINI
Ushriki wa wazee wa dini zenye kutambulika Kwenye shughuri za Kitaifa, nia ni kuongoza maombi na Ibada kiimani katika kuibadilisha mioyo na akili zetu [Mindset] Watanzania ambazo kipindi cha Rais Mstaafu Ally Hasaan Mwinyi alikuwa na dhamana zetu Watanzania hivyo siku hiyo akiwa na Viongozi hao wakidini, Wazee Wa Jadina Marais wenzake watakuwa na mawazo mapya ya kiimani juu ya timu zetu za TAIFA ngazi zote.Na kwa niaba ya Watanzania wapokee dua toka kwa viongzoi wa Kidini katika kufunga mlango wa kuwa kichwa cha mwendawazimu na kufunguwa ukulasa mpya wa kuwa na mlango mpya wa kukabidhi MKUKI kama ishara ya siraha ya Ushindi Kitaifa.

4: WAZEE WA KIJADI [MACHIFU NA WAZEE WA KIMILA
].
Ushiriki wao nao ni muhimu kwa kuwa nao ni sehemu ya jamii, kupitia dua zao za kijadi wanafungua milango ya wahenga wao kusimama mbele na nyuma ya Watanzania kila inapo itwa siku ya mechi zetu na mataifa mengine katika mashindano yoyote yale na kokote pale Duniani.

5: WANAMICHEZO NA WAFADHILI WA MICHEZO
Ushriki wa Wanamichezo na Wafadhili mbalimbali wa michezo kuwa sehemu ya tukio hilo kwa kuwa michezo na ufadhili ni MOYO mmoja katika kuleta ushindi wa Timu ya Mchezo wowote ule.Katika tukio hilo sio Mbaya Mara baada ya Mzee Mwinyi kutoa Mikuki kwa Wachezaji wa timu ya Soka siku ya tukio. Tukio hilo pia liendane na kuwepo na Mwakilishi kwa mmoja mmoja wa timu zinazocheza au shiriki michezo ya Kimataifa kutoka na Ligi Kuu [VPL].Pia kuwe na mwakilishi mmoja mmoja wa michezo mbalimbali tunayoshiriki Kimataifa kama Riadhaa, Ngumi, Mchezo wa Kikapu, Mpira wa Pete, na mingineyo yoyote yenye kuweza kuwapa vijana wa Tanzania ajira.

6: WATANZANIA

Hawa ndio washriki wakuu wa Tamasha la kufuta MINDSET zao, hawa ndio walengwa wa kusudio la kuwajenga KIROHO [SPIRITUALLY] kujiona kila timu yao inapoingia kwenye mashindano ya kimataifa basi wao TIMU yao NI WASHINDI DAIMA.Tamasaha hili lifanyike uwanja wa TAIFA MPYA na kiingilio bure cha Msingi wapatikane WAFADHILI kulifanya liwe na mvuto wa ina yake na kuweka kumbukumbu ya UTAIFA kuwa ile kauli NZITO YA UWENDAWAZIMU IMEKWISHA ZIKWA...LASMI KWA TAIFA.Na vijana wa kizazi kipya ambao kauri hii hawakupata kuiskia wakati inatolewa bali, wameiskia kama nukuu..Basi ni muda lasmi wapate NUKUU lasmi ya KITAIFA na kila TAIFA linaposhirki basi WATANZANIA wote kwa ujumla Watamke kama tumaini la USHINDI na ata ITOKEAPO tukafungwa tuone tuna nafasi ya kulekebisha makosa.

7: VYOMBO VYA HABARI;
Ushriki wa vyombo vya habari ni kuhakikisha mtizamo wa Taifa kuhusu Timu zetu za Taifa zinatoka kuwa Kichwa cha Mwendawazimu.Hapa ni Uzarendo...Ni sehemu ambayo Kila chombo cha habari kitumike katika kuhamasisha kauri mbinu ya kuweka hamasa kwa Watanzania kuondokana na ushriki wao katika hukumu ya kujiona wao ni kichwa cha mwendawazimu.Ka biidii ya dhati ya vyombo vya habari Taifa linatoka katika kujiona wanyonge wa Mashindano ya Kimataifa na Kuwa ni Washindi wa Michezo hiyo Kimataifa.Kwa wale wenye imani ya Kikirstu kuna misemo kama ''ALIWAZALO MJINGA NDIO LIMTOKEALO''.Hatuna budi sasa kwa nyakati hizi AKILI zetu Watanznaia ziendane na kuwaza mambo chanya [positive] na si has [Negative].

Tufike sehemu kama Taifa tujitanabaishe kwa ujumla wetu,mioyo ya kushindwa isiwe ni mawazo ya KITAIFA.Mashindano ya Kimataifa yatuunganishe kuwa washindi kabla ya kuingia Uwanjani.

8: MALINZI FAMILY:
Na hakika kwa wenye ufahamu familia hii, hamko kwenye soka au sekta ya michezo ka bahati mbaya.Wamejitanabaisha kama familia ya Wanamichezo.Mdogo wa Malinzi Senior Dionis ni Jamal Malinzi ambae ni Rais wa TFF ambao ndio wenye HATI MILKI ya lugha ya kichwa cha mwendawazimu, lakin pia Malinzi Senior Dions Malinzi yeye ni Kiongozi wa Baraza la Michezo Tanzania kwa awamu ya pili sasa.Kwa umoja wao wakiiunga nguvu zao na kuandaa Tamasha la kuondoa IMANI YA KICHWA CHA MWENDAWAZIMU kwenda MKUKI WA USHINDI WA WATANZANIA.Kwa kushrikiana kwao wanaweza kuasisi mabadiliko rohos [Spirt] ya jinsi Watanzania tunavyopokea timu zetu tunavyoshriki michezo kimataifa.Inaanza na kutamka kwa mdomo kisha uumbaji unafuata.Mungu alisema naiwe Mchana kukawa na nuru na kuwe na giza ikawa Usiku.

Jukumu hili la family hiyo iliyoko kwenye uongozi wa michezo ni kuongoza kutuandaa akili zetu Watanzania kuanza kufikilia kwa mtizamo chanya [Positive Perceptions].


Jisomee barua hiyo, nimeichukua kama ilivyo Toka
kwa Maulid Kitenge

"BARUA YA WAZI KWA ALLY HASAN MWINYI.
====================================
AWALI YA YOTE KWANZA KABISA NAPENDA KUKUPA HESHIMA YAKO MZEE WANGU ,
RAIS WANGU MSTAAFU ALHAJ ALLY HASAN MWINYI SHIKAMOO MZEE.
NIA NA DHUMUNI YA BARUA HII NI KUKUTAKA WEWE UKIWA KAMA MZEE WETU
KUTENGUA KAULI YAKO ILEEE ULIYOSEMA TANZANIA NI KICHWA CHA MWENDAWAZIMU.
KUMBUKA MZEE WANGU MANENO YA MTU MZIMA YAKITOKA HUWA HAYARUDI MATUPU .
VIJANA WAKO TUNATAABIKA NA KAULI YAKO KWA MAANA MPAKA LEO INATUTAFUNA.
ALHAJI MWINYI TUNAKUOMBA KWA MOYO MKUNJUFU
TENGUA KAULI YAKO YA KUWA TANZANIA NI KICHWA CHA MWENDAWAZIMU
ILI KULINUSURU TAIFA KATIKA MASWALA YA MICHEZO HUSUSANI MPIRA WA MIGUU.
MZEE WETU HIVI SASA TUPO KATIKA HALI MBAYA KULIKO VILE
KABLA HUJATOA KAULI YAKO KWA MAANA HAPO MWANZO TULIKUWA
TUNAJIKONGOJA YANI UAFADHALI ULIKUWEPO.
ZAMANI TIMU ILIKUWA HAINA MAANDALIZI MAZURI KAMBI ILIKUWA INAWEKA JESHI LA WOKOVU ,
WACHEZAJI WANAENDA MAZOEZINI NA DALADALA HUKU POSHO KUKIWA HAKUNA
ILA WALIPIGANA NA KUILETEA NCHI HESHIMA.
MHESHIMIWA TANGU UTOE KAULI YAKO ILE TAIFA STARS IMEKUWA KWELI KICHWA CHA MWENDAWAZIMU.
HAKUNA WA KUINUSURU TAIFA STARS ZAIDI YAKO WEWE ALHAJ ALLY HASANI MWINYI.
ONA LEO HII TUNAFUNGWA NA NCHI AMBAYO MFALME WAKE HANA
ANACHOWAZA ZAIDI YA KUOA VIGORI KILA MSIMU UFIKAPO.
MZEE WETU TUNAKUOMBA TENA NA TENA YANI TUPO CHINI YA MIGUU YAKO
TENGUA KAULI YAKO ILI KUINUSURU STARS YETU.
SINA MENGI ZAIDI MZEE WANGU ILA NATUMAI UJUMBE WANGU UTAKUFIKIA NA UTAUFANYIA KAZI.
WAKO KATIKA UJENZI WA TAIFA."
***** wako mimi ******

 
Kwa Taifa Star hii, tutaondoka na kapu la magori katika mechi za kufuzu Afcon.

NOTE: Misri, Nigeria, Chad tupo nao kundi moja.
Aiseeeee yaani jana niliona aibu jinsi timu yetu ilivyokuwa inapigishwa samba na nchi kama madagascar, jinsi Oscar Joshua alivyokuwa anapigwa tobo, Nyoni alivyokuwa uchochoro upande wa kulia, jinsi boko alivyokuwa anatoa ulimi nje nje kama mbwa anaetoka mawindoni.

Ila iliniuma sana nilipomuona kocha kilaza amevaa kofia yenye rangi ya bendara yetu ya tanzania....
Yaani kwa starz ile ya cosafa kukutana na Misri na Nigeria tutakula kama za Brazil na German.,..
 
Malinzi ajiuzulu tu, ni wakat muafaka sasa aondoke, mbona simba na yanga timu ikiboronga viongozi wanawajibika?
 
Aiseeeee yaani jana niliona aibu jinsi timu yetu ilivyokuwa inapigishwa samba na nchi kama madagascar, jinsi Oscar Joshua alivyokuwa anapigwa tobo, Nyoni alivyokuwa uchochoro upande wa kulia, jinsi boko alivyokuwa anatoa ulimi nje nje kama mbwa anaetoka mawindoni.

Ila iliniuma sana nilipomuona kocha kilaza amevaa kofia yenye rangi ya bendara yetu ya tanzania....
Yaani kwa starz ile ya cosafa kukutana na Misri na Nigeria tutakula kama za Brazil na German.,..

Kwa kweli ni aibu tupu kwa Taifa kubwa na maarufu kama Tanzania kufungwa na timu ndogo na ambazo kwa FIFA rankings ziko chini yetu kwa mbali!! Hata commentaries za watangazaji wa Supersport zilikuwa zinalivua nguo taifa, kama vile: TZ ni kama wamekuja matembezini, Tanzanians are very casual and not serious in their play, why have the TZans not learned this far and changed their game plan?...etc..ect!!

Jamani tusikubali tena kuendelea na aibu hii na timu hii kwenye mechi zetu za AFCON na CHAN. Tufanyeje?:

- Kwanza tufumbe macho na kocha huyu mdachi atimuliwe mara moja. Aheri kwa kipindi hiki tumpe timu kocha mzawa e.g. Mkwasa (ashajifunza mengi kwa Pluijm), ili walau selection ya wachezaji izingatie realities na performance
- In the long run, bora tumrudishe Kim Poulsen, kwani alikuwa na mipango longterm ya kutumia vijana na pia timu ilikuwa inacheza mpira unaoeleweka ref: vs. Ivory Coast, Morocco, etc. Huyu mdachi analipua tu kwani mipango kwa ajili ya mbeleni
- TFF: fukuza kamati yote ya ufundi iliyowekwa kishikaji na kuishia kurundika wahaya kwenye uongozi...iiundwe upya kwa kuzingatia weledi
- Rudisha jezi zetu za zamani, hizi jezi mbaya za rangi ya ajabu ajabu weka pembeni kwani zinaonekana zina minuksi!!
- Rudisha utaratibu wa kuwa na Taifa Stars B yenye vijana tu na ipwe fursa ya kwenda kwenye mashindano e.g. CHAN
 
Kwa Taifa Star hii, tutaondoka na kapu la magori katika mechi za kufuzu Afcon.

NOTE: Misri, Nigeria, Chad tupo nao kundi moja.

Tuipe starz tissue za kutosha maana watapakazwa gundi mpaka basi
 
hakuna ushauri hapo iyo inaonekana kufanya vibaya ndio.asili yetu maana miaka nenda miaka rudi tunakuwa kichwa cha mwendawazimu
 
Toka umeingia TFF hakuna mafanikio yoyote, uwezo wa kiongozi yeyote hupimwa kwa kuangalia idadi ya vikombe na mechi ulizoshinda , toka umeingia madarakani hakuna tulilopata, timu inazidi kuwa dhaifu imefika hatua tunafungwa na vitimu dhaifu kama swaziland, madagascar.
Unapeleka timu kwenye mashindano haina hata maandalizi, unakeeeeera
Jiuzulu kabla hatujakungoa
 
Hakika kakangu malinzi kwa timu ya taifa umepwaya.sjui ni sababu hipi ilikufanya kumuondoa kim poulsen na kumleta nooij ushaur wang timu wape wazawa tujue moja
 
Namkumbuka Sana Leodgar Chilla Tenga Na Tulichokifanya Watanzania Ni Kutoka Ktk Afadhali Na Kwenda Ktk Potelea Mbali a.k.a Tumeruka KOJO Kudadadeki Sasa Tumekanyaga KIMBA Tena Lile La Mtu Mzima Na Lililo Komaa Halafu Zito. Tumeyataka Wenyewe Haya Na Ndiyo Kwanza Kabakiza Miaka 3. Mwaka Huu TUNANUNA Kwa Mengi!
 
Hakika kakangu malinzi kwa timu ya taifa umepwaya.sjui ni sababu hipi ilikufanya kumuondoa kim poulsen na kumleta nooij ushaur wang timu wape wazawa tujue moja

Timu imeenda haina hata mazoezi, akina ngassa walikuwa south, wamekusanywa tu na kupelekwa, kama maandazi.
 
Mwenyewe anasema mafanikio ni kuwa siku hizi tunaona mechi zote ambazo taifa stars huwa inacheza, yeye hayo ndio mafanikio, Na sijui huyu kocha walimtoa wapi na kwa nini anabaki mpaka sasa.
 
Namkumbuka Sana Leodgar Chilla Tenga Na Tulichokifanya Watanzania Ni Kutoka Ktk Afadhali Na Kwenda Ktk Potelea Mbali a.k.a Tumeruka KOJO Kudadadeki Sasa Tumekanyaga KIMBA Tena Lile La Mtu Mzima Na Lililo Komaa Halafu Zito. Tumeyataka Wenyewe Haya Na Ndiyo Kwanza Kabakiza Miaka 3. Mwaka Huu TUNANUNA Kwa Mengi!


Siongezi neno maana umemaliza. Ang'olewe kuokoa soka letu.
 
Malinzi tunataka taarifa leo ya kuwa kocha kashatimuliwa sio ujinga na upuuz eti tunajenga timu kwa kocha kuita timu kwa copy na paste mpaka majeruhi wanaitwa!alaf eti kuna mkurugenzi wa ufundi.upumbav mtupu yan nina hasira mpka bas
 
Back
Top Bottom