Kuna jamaa yangu anasoma UDSM mwaka wa pili, leo kanishangaza kwa kuniambia kwamba kuna baadhi ya wahadhiri wa chuo hicho, wakiwemo maprofesa, ambao husomesha tuisheni kwa baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho.
Habari hizi zimenishtua sana kwani sikutegemea wanafunzi wa chuo kikuu kusomeshwa tuisheni. Wadau mliopo hapo Mlimani naomba mtuhabarishe hii inakuwaje. Je, tuisheni inafanyika hadharani au mafichoni? Kazi ya mhadhiri ni kuelekeza--sio kufundisha. Ikiwa mwanafunzi hajaelewa mafundisho ya Profesa ni juu yake kujisomea au kujitafutia maarifa mwenyewe. Tuition & Spoon Feeding Syndrome itaiua elimu yetu.
Hii tuisheni ktk Chuo Kikuu ni dalili ya anguko la elimu yetu. Na hawa wanafunzi ndiyo lile zao la wanafunzi waliojiunga sekondari za kata huku wakiwa hawajui kusoma na kuandika. Madhara ya wanasiasa kuifanya elimu yetu kichwa cha mwendawazimu ndiyo yaliyotufikisha hapa na bado tutaendelea kushuhudia madudu mengi tu siku zijazo.
Je, nini kifanyike kurudisha elimu yetu kwenye reli?
Nawasilisha.
:israel: