Tuisheni hadi Chuo Kikuu?

Tuisheni hadi Chuo Kikuu?

Ukisikia kuwa unatakiwa ulipe Tuition fees huwa unaelewaje? Tuanze na hapa kwanza

TUITION FEE ni ada ya taaluma, yaani malipo kwa ajili ya mafundisho unayopewa na wahadhiri. Na hizi fedha zinalipwa moja kwa moja chuoni na mwanafunzi husika. Je, wewe unaelewa nini kuhusu tuition fee? Je, fedha unazomlipa profesa kwa kukufundisha masomo ya ziada wewe unaziita TUITION FEE? Na zile unazolipa chuoni moja kwa moja unaziitaje?
 
Habari zenyewe huna uhakika nazo halafu unamake conclusion unategemea nini.
Wapi kwingine umesikia kuna hiyo unaita tuisheni au ni UDSM pekee yake?
Huyo aliyekwambia hakukwambia kila kitu kilivyo?

huyo aloniambia yeye hasomi tuisheni. wewe unayesoma tuisheni ndiye utuambie inakuwaje. je, mnalipa kwa unit au kwa kipindi? na ni kiasi gani kwa kipindi/unit?
 
tuition fee ni ya kusomea tuisheni? hizo hela mnalipwa cash kama boom? wewe lazima utakuwa kizazi cha division 5. BTW kuwa na GPA kubwa uliyoipata kwa kukariri sio kigezo cha kuelimika au kuwa na maarifa.

Usipanic mkuu,
Najua kila kitu, I just wanted to make funny out of the matter. Usihangaike na mimi sana. Usiku mwema
 
Kuna jamaa yangu anasoma UDSM mwaka wa pili, leo kanishangaza kwa kuniambia kwamba kuna baadhi ya wahadhiri wa chuo hicho, wakiwemo maprofesa, ambao husomesha tuisheni kwa baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho.

Habari hizi zimenishtua sana kwani sikutegemea wanafunzi wa chuo kikuu kusomeshwa tuisheni. Wadau mliopo hapo Mlimani naomba mtuhabarishe hii inakuwaje. Je, tuisheni inafanyika hadharani au mafichoni? Kazi ya mhadhiri ni kuelekeza--sio kufundisha. Ikiwa mwanafunzi hajaelewa mafundisho ya Profesa ni juu yake kujisomea au kujitafutia maarifa mwenyewe. Tuition & Spoon Feeding Syndrome itaiua elimu yetu.

Hii tuisheni ktk Chuo Kikuu ni dalili ya anguko la elimu yetu. Na hawa wanafunzi ndiyo lile zao la wanafunzi waliojiunga sekondari za kata huku wakiwa hawajui kusoma na kuandika. Madhara ya wanasiasa kuifanya elimu yetu kichwa cha mwendawazimu ndiyo yaliyotufikisha hapa na bado tutaendelea kushuhudia madudu mengi tu siku zijazo.

Je, nini kifanyike kurudisha elimu yetu kwenye reli?

Nawasilisha.

:israel:

Unamaanisha zao la Ndalichako.

Kwi kwi kwi teh teh teh.
 
TUITION FEE ni ada ya taaluma, yaani malipo kwa ajili ya mafundisho unayopewa na wahadhiri. Na hizi fedha zinalipwa moja kwa moja chuoni na mwanafunzi husika. Je, wewe unaelewa nini kuhusu tuition fee? Je, fedha unazomlipa profesa kwa kukufundisha masomo ya ziada wewe unaziita TUITION FEE? Na zile unazolipa chuoni moja kwa moja unaziitaje?

Isome tena post yako
Au kaiandike upya
For sure bado hujagraduate na sasa hivi hope upo unalia na hela ya Field kuchelewa kutoka.Na aim yako wala haikuwa hicho ulichiandika umezunguka sana kutaka kudeliver ulichotaka be straight
 
huyo aloniambia yeye hasomi tuisheni. wewe unayesoma tuisheni ndiye utuambie inakuwaje. je, mnalipa kwa unit au kwa kipindi? na ni kiasi gani kwa kipindi/unit?

Hivi unakielewa unachokiandika?
 
Back
Top Bottom