Shida ni kwamba kizazi cha sasa tumeingiwa na ubinafsi sana. Matokeo yake kila mtu anajifikiria yeye na kusahau kujitoa kwa wengine. Na akijotoa anajitoa kwa malengo ya kupokea maradufu ya alichotoa.
Ukitaka kulijua hili jaribu kuwa mkarimu na watu kwa kujitoa utaona usumbufu na ukaribu watakaofosi kwako. Kimsingi shida ilianza na aina ya familia tulizojenga miaka ya kuanzia 1980's. Watoto wa kizazi hicho ndio watu wazima wa sasa.
Tulizoea kuletewa kila kitu bila kushiriki kutafuta. Zamani watoto na wazazi walifanya mambo pamoja kama kulima,kuvuna, kutazama mifugo,na mambo ya kijamii. Ila kizazi cha 1980's mostly hawa tuliokulia mijini tulilelewa na utamaduni wa ajabu sana.
Watoto tunaletewa kila kitu kuanzia nguo,chakula,vitu vya kuchezea bila kujua vinatoka wapi. Baba pekee ndie alikuwa mtafutaji ila mama na watoto tukawa tunasema tunachotaka na kupewa.
Matokeo yake ile mentality ya kupewa ndio imekomaa kichwani kwahiyo code ya maisha tunayoielewa ni kupewa ndio upendo na sio kutoa.
Kuna wazazi wamewafunza watoto wao tofauti kimalezi kwa kuwafundisha kujitoa,kushiriki sana mambo ya wengine, kumsaidia mtu bila kutaraji malipo,kuthamini zaidi mahitaji ya wengine, kupambana kutafuta kwaajiri ya wengine na kadhalika na ndio hao sasa wamekuwa watu wazima wa kutegemewa kwenye hii jamii ya sasa na wanazongwa na watu wanaowapenda na kuwa muhimu kwenye jamii.
Ila kwa wastani wale ambao tumekuwa makuzi ya kuishi kivyetu, wazazi hawahangaiki na kutushirikisha maswala la kupanga bajeti za maisha,hawakututengenezea utamaduni wa kushirikiana na ndugu au wanajamii wengine kwa kujitoa kimasomaso kuwasaidia na kuwatatulia shida zao,ndio hawa sasa tumekuwa watu wazima tunaona kusaidia wengine ni kujidhurumu au ni pata potea,tusipopewa chochote tunahisi hatupendwi au kujaliwa,tunatafuta cha kututosha wenyewe akija mwenye shida tunamuona kama hana utimamu wa akili kwa kutaka kutumia tulichotafuta kama ni chake au kinamhusu.
So hizo formula ulizozisema zinaweza kuwa suluhu ya muda ya hizi changamoto za mahusiano ya kijamii tunazopitia ila nikwambie tu kuwa kuna picha kubwa ambayo hatuitazami na ndio inatutesa.
Unaweza kusema watu wamekuwa wa hovyo siku hizi ila chunguza mwenendo wako na wa kila m'moja utaelewa kuwa tunachangamoto za kimalezi zinatutafuna kama descendants au uzao wa toleo la wazazi waliolea watoto nje ya mfumo wa tamaduni zetu za asili za kuishi kijamaa kama wanajamii.