Elius W Ndabila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 324
- 649
TUISHIE TU KWENYE KUANDIKA HUKUMU AU TWENDE MBALI ZAIDI?
Na Elius Ndabila
0768239284
Jana Mh Rais alimpongeza Jaji wa Mahakama kanda ya Msoma ambaye aliandika hukumu kwa lugha ya Kiswahili. Mh Rais hakuishia kumpongeza tu, bali jana hiyo hiyo alimteua kuwa Mhe Zepharine Nyalugenda Galeba kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Mteule huyo ameapishwa leo Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma.
Wakati akiapishwa, pamoja na mambo mengine Mhe Rais amemshauri Waziri wa Katiba Mhe Dkt Mwigulu Lameck Madelu Nchemba kuwa apeleke mswaada Bungeni ili Mahakama zianze kuandika hukumu kwa lugha ya kiswahili ambayo ni lugha rafiki kwa Watanzania na ni kuonyesha uasisi wa Baba wa Taifa ambaye aliysunganisha Makabila zaidi 121 kuongea lugha moja ya Kiswahili.
Ninampongeza Rais kwa ujasiri huo na moyo ambao amekuwa nao juu ya kukuza hii lugha adhimu ya kiswahili.
Lakini wakati Mhe Rais anashauri hilo, mimi nimeenda mbali kuwa kwa nini sasa tusione haja ikiwezekana hata sheria zinazotungwa na Bunge kuandikwa kwa kiswahili? Tumeona Wabunge wakifanya mijadala kwa lugha fasaha ya kiswahili, lakini linapokuja swala la kuandika sheria zinaandikwa kwa Kingereza na wakati mwingine Sheria zinapoanza kutumika Wabunge nao wanakuwa wanazishangaa!
Mshangao huu wakati mwingine mtaani tunatafsiri kuwa labda wabunge baada ya kutunga sheria wanaoenda kuandika tena kwa lugha za kiingereza wanabadilisha? Ninakumbuka wakati sheria ya Kikokotoo inataka kuanza kutumika Wabunge wengi tukiwauliza hii sheria inasemaje nao walikuwa hawaelewi. Leo tukiwauliza hili la bodi ya mikopo likoje kutoka asilimia 8 hadi 15 wengi wao hawajui.
Sasa kwa nini sheria za bunge nazo zisiandikwe kwa lugha ya kiswahili kutoka kwenye muswada ili wabunge waweze kuwa na uelewa wa pamoja?
Ninadhani hili halitasubiri kauli ya Mh Rais, bali wabunge wetu tuliowaamini wanaweza kutusaidia kulitafuna.