Tuisome, tuipitishe Katiba Inayopendekezwa

Tuisome, tuipitishe Katiba Inayopendekezwa

nyimbag

Member
Joined
Feb 28, 2015
Posts
41
Reaction score
17
‘Tuisome, tuipitishe Katiba Inayopendekezwa'

Natumia furusa hii kuishukuru Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa kujali umuhimu wa kuwapo misingi
Baadhi ya wananchi wa mkoani Tanga wakishiriki moja ya midahalo ya katiba inayopendekezwa .
Natumia furusa hii kuishukuru Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa kujali umuhimu wa kuwapo misingi ya maadili ya viongozi wa umma ndani ya katiba kwa masilahi ya Watanzania wote.

Ni ngumu nchi kupata maendeleo ikiwa jamii ya watawala haina misingi mizuri ya maadili. Katika Rasimu ya Pili ya Katiba Iliyopendekezwa suala la maadili kwa viongozi wa umma yalitiliwa mkazo kwa kiasi kikubwa na bila shaka maadili ndiyo msingi muhimu wa uwajibikaji kwa viongozi wa umma kwa masilahi ya Taifa.

Ukiukwaji wa maadili ya utumishi wa umma ndicho chanzo cha rushwa, umaskini, uwajibikaji mbovu pamoja na migogoro katika jamii kwa sababu ya jamii kukata tamaa pamoja na kutowaamini viongozi wenye dhamana ya kuwatumikia.
Tangu rasimu hii ilipowasilishwa kwa Rais na baadaye katika Bunge la Katiba kumekuwapo na kauli nzito na za lawama dhidi ya Bunge kwa kupitisha rasimu mbovu na hivyo haifai kukubaliwa na wananchi.

Tuwe watulivu
Nawasihi Watanzania kuwa watulivu na kuwa na utamaduni wa kutopenda kusikiliza yanayosemwa bila kujipa nafasi ya kuyafuatilia kwa kina.

Ninatumia nafasi hii kuwafahamisha Watanzania kwamba wale wanaosema kwamba misingi ya maadili haikuwekwa katika Katiba Inayopendekezwa ni waongo, misingi ya maadili kwa viongozi na watumishi wa umma imewekwa na kuzingatiwa katika Katiba Inayopendekezwa kama ilivyokuwa katika Rasimu ya Tume.

Bunge lilifanya kazi yake
Kwa kuona umuhimu wake, Bunge la Katiba likapitisha sura nzima inayohusu maadili na miiko ya uongozi kwa viongozi na watumishi wa umma tena kwa mapana katika ibara mbalimbali.

Sura ya Nane ya Rasimu ya Katiba Inayopendekezwa ndiyo imebeba maudhui ya maadili na miiko ya uongozi na utumishi wa umma na sura ya kwanza inahusu maadili ya uongozi na utumishi wa umma na sehemu ya pili inahusu miiko ya uongozi wa umma.
Ibara ya 28 (1) (a) pia ibara ndogo ya (2) inaeleza vyema maana ya dhamana ya uongozi wa umma na imeweka wazi kwamba madaraka anayopewa kiongozi wa umma ni dhamana na atatumia madaraka hayo na kutekeleza wajibu wake kwa kuzingatia masharti ya katiba hii.

Ibara ya (29) (1) (a-c) inataja na kubainisha kanuni za uongozi wa umma pia katika ibara ndogo ya (2) (a-h) Bunge limepewa wajibu wa kutunga sheria zitakazosimamia maadili ya viongozi wa umma. Vilevile katika ibara ndogo ya (3) Katiba imeweka wazi bila kubagua kwamba viongozi wa umma inajumuisha viongozi wa kuteuliwa pamoja na wale wa kuchaguliwa.

Pamoja na mambo mengine, dhamira pamoja na mazingatio ya kuweka misingi mizuri ya maadili kwa Bunge maalumu imejidhihirisha wazi katika ibara hii ndogo ya (2) na Katiba hii inalielekeza Bunge kutunga sheria itakayoanzisha mitalaa inayohusu Katiba, maadili na uraia, shuleni na vyuoni.

Ni wazi kwamba Katiba imetengenezwa katika misingi imara ya kuwa na mizizi ya kuondoa tatizo la kukosekana kwa maadili katika nchi yetu kwa kuwa jamii itakuwa inaandaliwa kuanzia chini kujali misingi ya maadili. Katiba Inayopendekezwa ni nzuri na pongezi kwa wajumbe wote wa Bunge Maalumu walioshiriki kuitunga Katiba hii.

Sehemu ya pili ya sura ya Nne ya Katiba hiyo inahusu miiko ya uongozi wa umma katika ibara za 29 pamoja na 30. Ibara ya 29 (1) inamlazimisha kiongozi wa umma kuheshimu na kutii miiko na maadili ya uongozi wa umma, ibara ndogo ya (2) inatoa wajibu kwa Bunge kutunga sheria zitakazoainisha miiko inayotakiwa kuzingatiwa na kiongozi wa umma, kuweka utaratibu wa kumwondoa kazini kiongozi wa umma atakayekiuka miiko na maadili ya uongozi wa umma, kuanisha vitendo ambavyo kiongozi wa umma hatakiwi kuvitenda pia Bunge litaainisha orodha ya viongozi wa umma watakaofungwa na ibara hii. Vilevile ibara ya (31) imeweka wazi marufuku vitendo ambavyo kiongozi wa umma hatoruhusiwa kuvitenda.

Katiba imejitosheleza katika eneo hili, wajibu uliobaki ni wa wabunge watakaokuwa na jukumu la kutunga sheria kuhakikisha wanatunga sheria nzuri na zenye meno makali ya kuwatafuna viongozi na watumishi wa umma watakaokiuka miiko na maadili ya utumishi wa umma.

Jambo muhimu la kuzingatia na kushukuru ni kwamba kwa mujibu wa Katiba hii suala la miiko na maadili ya uongozi kwa watumishi wa umma limekuwa ni la kikatiba kuliko ilivyo sasa na sheria ambazo hazina msingi mzuri katika Katiba tuliyonayo sasa ya (1977).
Katiba Inayopendekezwa ina misingi mikali mno ya kuwadhibiti viongozi wa umma iwapo watakiuka maadili kwa mujibu wa Katiba hii.
Ni wazi kwamba kwa muda mrefu kumekuwapo na wizi wafedha za umma kwa baadhi ya viongozi na watumishi wa umma na wamekuwa wakizificha kwenye akaunti za nje ya nchi kutokana na ulegevu wa sheria zilizopo sasa kushindwa kulikabili tatizo hili na hapakuwapo ha hatua za wazi na nzito za kumchukulia kiongozi wa namna hii.Ibara ya 30 ya Katiba hiyo imelipa wajibu Bunge kutunga sheria itakayoweka masharti kwa kiongozi wa umma kufungua akaunti za nje pia ni wazi kwamba wizi na ufichaji wa fedha za umma kwenye akaunti za nje kama ilivyo sasa utadhibitiwa.

Pia, katika ibara hiyohiyo ya (30) (2) (f) Bunge limepewa wajibu wa kutunga sheria itakayoweka utaratibu wa utwaaji wa mali za kiongozi wa umma zinazopatikana kwa kukiuka sheria (maadili na miiko) kama Katiba inavyobainisha na sheria itakavyoelekeza.

Taasisi za uwajibikaji
Katika Sura ya 15 Katiba Inayopendekezwa imetaja Taasisi za uwajibikaji miongoni mwazo ni Tume ya maadili ya viongozi wa umma ambayo imetajwa katika sehemu ya kwanza ya sura hii. Ibara ya 228 (1) inatoa mamlaka ya kikatiba ya kuanzishwa Tume ya maadili ya viongozi wa umma.

Ibara ya 229 (1) imeweka utarartibu mzuri wa uteuzi wa wajumbe wa tume hiyo pamoja na sifa zao kwamba wajumbe hao watateuliwa na Rais baada ya kupendekezwa na kamati ya uteuzi (hapa mamlaka ya Rais ya uteuzi yamepunguzwa) na ibara ya 230 inaainisha muundo wa kamati ya uteuzi ambayo itakuwa na wajumbe huru wanaopatikana kwa mujibu wa Katiba na wametajwa na katiba moja kwa moja.

Kwa hiyo wajumbe wa Tume ya maadili ya viongozi wa umma hawateuliwi na Rais moja kwa moja. Pia wajumbe wa kamati ya uteuzi nao hawateuliwi na Rais kufanya kazi yao ila wapo kikatiba na majukumu yao yapo kikatiba hivyo wako huru kufanya kazi zao.

Ibara ya 231(1) inaweka wazi majukumu ya Tume ya maadili na hayana mipaka kwa viongozi wote wa umma kwenye mihimili yote ya dola, taasisi na idara nyingine zote za umma. Tume hii ina mamlaka ya kuhakikisha maadili na miiko ya uongozi wa umma inalindwa na kuheshimiwa. Ibara ya 227(1) inatoa uhuru wa Tume ya Maadili kufanya kazi bila kuingiliwa.

Kwa mtu yeyote anayetaka taifa hili lipige hatua kimaendeleo na jamii nzima ibadilike kimaisha na kuwa na maisha bora na yenye usawa, kamwe hawezi kubeza katiba hii Inayopendekezwa. Tuisome katiba hii kwa kina na tujitokeze kwa wingi kuipitisha Katiba hii kwa kura nyingi za ndiyo.
Mwandishi ni mwanasheria. Anapatikana kwa simu 0784 646 220 ktb tuisome.jpg:rip:
 
We farasi wa Sengerema. Huo ujinga peleka kwenu . umekosa sifa za kuitwa wanaume. Katiba peleka kwenu Kwa baba ako . jinga sana we we. Vya ccm vitakuvua nguo. Tafuta chako
 
Kama ni kweli mwandishi ni Mwanasheria, with due respect, nimesikitishwa sana na hoja zake na hata lugha yake. Mwandishi akumbuke kuwa uteuzi wa MaDC umeshafanyika. Na ajitahidi kulinda heshima ya taaluma ya sharia. Ni hayo tu
 
jifunze kusoma na kusikiliza hoja tofauti na mawazo kisha jibu kwa hoja usitukane tukane ovyo
 
Back
Top Bottom