Tujadili: Athari za mitandao ya kijamii na maisha yetu ya mahusiano

Tujadili: Athari za mitandao ya kijamii na maisha yetu ya mahusiano

Daby

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2014
Posts
33,894
Reaction score
76,810
Asaalam.

Wote tuliopo humu ni wapenzi wakubwa wa mitandao ya kijamii tukianza na huu uliyotuleva yaani JF.

Nguvu ya mitandao ya kijamii kututoa katika uhalisia tunaoishi ni kubwa saana. Muda mwingi unaweza kujikuta unautumia kwenye mitandao na kuyasahau maisha yako halisia.

Ok, hoja yangu ni wale watu mliopo kwenye mahusiano/ndoa mna wake na watoto mnakutana na changamoto gani zinazosababishwa na mitandao hii mnayotumia! mnapambana nazo vipi? Wenza wenu walishalalamika kuhusu hizi changamoto? huwa unayachukuliajr malalamiko yake? yana ukweli au ni usumbufu tu?
 
Binafsi:

Ni mtumiaji wa mitandao hasa JF muda mwingi unakuta nipo busy kusoma humu au kuchangia.

Changamoto kubwa ninayokutana nayo ni kutowapa watu naokuwa nao usikivu pindi ninapokuwa humu.

Unakuta mtu analalamika nipo hapa lakini unatype tu hakuna attention.

malalamiko:

Huwa nayapokea maana yanaukweli ndani yake.
 
Sisi tusio kwenye mahusiano wala hatuna familia haturuhusiwi kuchangia?
Mnaruhusiwa kuchangia. Hauna mtoto? hauna marafiki wa karibu unaoshinda nao muda mwingi?

Hauna mtu ambaye huwa anahitaji attention yako?
 
Mda wa familia ni mda wa familia simu inakua pemben..ukiwa na mtu mmetoka out simu nayo iwe pemben kumpa mtu attention

Ni matter tu ya kujicontrol otherwise simu ndo itakucontrol,.
 
Mda wa familia ni mda wa familia simu inakua pemben..ukiwa na mtu mmetoka out simu nayo iwe pemben kumpa mtu attention

Ni matter tu ya kujicontrol otherwise simu ndo itakucontrol,.
Unaweza ukajilimit hivi kwa asilimia zote? upo vizuri saana
 
nikiwa na mizunguko huwa natembea na simu ndogo
sitaki karaha za simu mimi
Ukiwa umetulia ndiyo unazitumia? unapokuwa umetulia hamna watu wanakuwa wamekuzunguka au unakuwa umejifungia mwenyewe!
 
Umri wako ni mdg kiasi cha kukosa mahusiano na familia?!
Ukubwa wa umri sio kigezo cha kuwa na familia wala kuwa katika mahusiano.

Haya tueleze namna unavyokabiliana na athari za mitandao kwenye mahusiano yako
 
Ukubwa wa umri sio kigezo cha kuwa na familia wala kuwa katika mahusiano.

Haya tueleze namna unavyokabiliana na athari za mitandao kwenye mahusiano yako
Nadhani ungesema sio kigezo kimoja tu.

Ila ukubwa wa umri ni moja ya kigezo cha kuwa na familia. Ukiwa mwanamke wa umri wa miaka 40tunategemea kwa kiasi kikubwa uitwe mama wa watoto au mtoto.

Na bahati nzuri wengi wapo hivyo.
 
Ukiwa umetulia ndiyo unazitumia? unapokuwa umetulia hamna watu wanakuwa wamekuzunguka au unakuwa umejifungia mwenyewe!
napenda sana kuongea nikishika simu muda Hui nakua mpweke kama mud a Hui
ukiona nimepotea jukwaani tambua Nina kampani ya nguvu no break
 
Nadhani ungesema sio kigezo kimoja tu.

Ila ukubwa wa umri ni moja ya kigezo cha kuwa na familia. Ukiwa mwanamke wa umri wa miaka 40tunategemea kwa kiasi kikubwa uitwe mama wa watoto au mtoto.

Na bahati nzuri wengi wapo hivyo.
Nakubali kukubaliana nawe Daby
 
napenda sana kuongea nikishika simu muda Hui nakua mpweke kama mud a Hui
ukiona nimepotea jukwaani tambua Nina kampani ya nguvu no break
Umetisha.... Mimi sipendi kuongea nikiwa na simu karibu tu ni kimya hadi utakaponigutua
 
Back
Top Bottom