matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 7,968
- 19,368
Wakuu huu ndio msimamo wangu katika kutoa msaada kwa chochote nitakachokuwa nacho. Sitaki kusaidia Pesa nataka huduma au vitu, Kama ni nauli, nitakukatia tiketi au namlipa konda, kama ni ada nitakupa bank slip. Kama ni chakula nitakununulia au nitatuma mtu akuletee manually kama uko mbali.
Hii imenisaidia kukwepa walaghai wengi. Pia hii nilijifunza kwa yule msamalia aliyemuhudumia matibabu mtu aliyepigwa. Alimpa huduma ila hakumuachia hata pesa ya nauli kurudi alikokuwa anakwenda.
Leo nimepata shida baada ya muokota makopo akiwa hana pesa ya kula ilala stand. Nimemchukua nampeleka kwa mama ntilie hataki anataka anipeleke yeye kwenye chimbo lao la kula maukoko Karume.
Tumebishana sana nikaamua nimpe buku mbili ili aende akale anakojua maana amenishinda tabia.
Wakuu mnapata changamoto gani katika kusaidia watu.