Ubaguzi upo sana na ni Mpana sana, hata kwetu sisi Weusi tunabaguana, nitakupa mifano miwili bila kutaja majina ya sehemu husika.
Nilienda kwenye moja ya hoteli za Kifahari jiji Dar kwa ajili ya ku confirm chumba nilichobook week moja nyuma, nakumbuka hiyo siku ilikuwa jumamosi nilikuwa nimejivalia kawaida tu, nikimaanisha sikuwa smart, lakini hii haikunizuia kuingia kwenye hiyo hoteli.
Nikafika mapokezi nikaunga mstari kama wengine niliowakuta....nakumbuka mbele yangu kulikuwa na wazungu na pia nyuma yangu kulikuwa na wazungu, ilipofika zamu yangu, yule muhudumu alimwita mzungu aliyekuwa nyuma yangu na kuniacha mimi, sikufanya lolote, nilijua labda alikuwepo kabla yangu.
Alipomaliza nikaona amemwita tena mzungu mwingine aliyekuwa nyuma yangu, hapo sikuweza kuvumilia nikaingilia kati....
Cha kushangaza sikuambiwa sababu na wala hawakuona kama nahitaji kuombwa radhi....
Nilimaliza kilichonileta pale, nikaomba kuonana na Mkuu wao wa kazi, ambaye ni mtu ninaye fahamiana maana huwa naitumia sana hiyo hoteli ....issue tukaimaliza kiungwana ila nilijisikia vibaya sana kubaguliwa nikiwa ndani ya Nchi yangu tena na Mweusi mwenzangu, kisa ameona Wazungu.
Kisa cha pili, ni katika Hospitali moja kubwa tu Jiji Dar, nilikuwa na mgonjwa wangu pale....
Kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu nikawa nashindwa kuwahi muda uliopangwa wa kuona wagonjwa, nikawa na chelewa, lakini naongea namlinzi ananielewa napita....
Sasa akabadilishwa mlinzi, siku hiyo nafika akanikatalia kabisa, nikaaa nje nafikiria cha kufanya, Mara wakaja Wazungu wakaongea nikaona wameingizwa, nikajua wanaweza kuwa m Dr, mda si mrefu wakaja Wahindi nao wakaingizwa, hapo sasa nilipoona yamefikia huko, kilichoendelea ni siri yangu...
Ubaguzi wa sisi weusi kwa weusi upo na unaumiza sana....