Habari wana JF
Mwenzenu nimeoa (mke mfanyakazi) miaka mitatu iliyopita na kujaaliwa ka baby boy mmoja tu.
Tatizo langu ni, mke wangu kamwachia majukumu yooote msichana wa kazi! Kwa mfano, usafi wa nguo zangu, maandalizi ya chakula na kazi zote za nyumbani.
Hilo mimi sijali lakini najiuliza kuhusu hili, ninaporudi nyumbani na kifurushi mkononi hata kama mke wangu amekaa tu hana kazi yoyote atamwita msichana wa kazi na kumuamuru anipokee. Anaponipokea anasema, shikamoo baba......, pole........., karibu............., tena kwa unyenyekevu wa hali ya juu. Mke wangu desturi hiyo hanaa!!
Atakapoandaa chakula house girl huyu huyu ataninawisha mikono na kunikaribisha chakula kwa unyenyekevu mkubwa akisema `karibu chakula baba`. Wife wala habari hana, na siku akiandaa msosi wife atasema `Baba nanii....chakula tayari`.
Asubuhi chai napo ni vivyo hivyo, atapewa house girl viatu asafishe (kubrash) then atanirudishia na kunambia kwa utulivu, viatu tayari baba!!
Mbaya zaidi juzi nikamkuta chumbani kwetu kwenye bafu (master) anafulia huko huku wife akiwa amekaa barazani na wenzie wanapiga story. Nikamuuliza unafanya nini huku na kwa ruhusa ya nani, alinijibu kuwa mama kamwambia afulie nguo zetu kule (za mimi na wife) then afanye na usafi wa kule msalani na chumba kizima, pia nahisi alitakiwa afue hata nguo za ndani coz nilikuta zimelowekwa pale pale.
Kiukweli nilichukia sana na akili ilinituma nimchape kitu yule binti (ku-mdo) but ni busara tuu iliyoniepusha.
Nimejaribu kumrekebisha mara kadhaa ananisikia na kunielewa but anaonekana ni mvivu kutimiza wajibu wake. Wife ni msikivu sana but sielewi tatizo nini jamani.
Swali langu ni kwamba, wanaume wenzangu mnayarekebisha vipi mambo kama haya coz kikawaida hisia zinaweza kuhamia kwa binti kwa jinsi alivyoachwa kuwa karibu nami na hasa wife alivyojiweka mbali ili nisije zua balaa.
Asanteni sana
kaka za leo, mimi ni mara chache sana kusoma hizi mada za mapenzi, na nimeona wengi wanakupa ushauri ambao hauikidhi haja na ndo maana wengi wamekimbilia kukwambia kuwa tayari roho ya kutaka ku M-do inakunyemelea. Mimi naamini na niwakumbushe hao, ungekuwa na roho ya ku m-do wala usingeleta hii mada ung m-do kimya kimya.
Kaka jinsi ya kukwepa hilo tatizo ni rahisi sana, wewe mpige mkwara huyo house girl, kila akifanya kazi zinazoashilia kukutega hasa kuingia chumbani mwako piga mkwara hasa, mkataze asifue nguo zako kama unaweza, ila kama mkeo mbabe utazifua mwenyewe. Hafu nguo za ndani za kwako UFUE mwenyewe na mke wako afue za kwake.
Weka ka utaratibu HG ajue mipaka yake,kuruhusu BEKI 3 kuingia chumbani ni sumu.Unajua kuna baadhi ya matatizo Wanaume huyasababisha wenyewe, tangu lini nguo yako ya ndani ukubali ifuliwe na Mercury (HG) au mkeo, fua mwenyewe mara tu unapoenda kuoga kuondoa baadhi ya matatizo.
Hata nguo zako ikibidi fua mwenyewe, acha Umangi meza, Mbona wazungu wanaume wanafua wenyewe, utasema kwao kuna mashine si wote wenye mashine na wakija africa wanafua wenyewe.
La tatu, uchunguzi niliokwisha uona, wanawake huwa wanalegea miili yao haraka kadri wanavyokuwa, hivyo hupelekea kuwa wavivu kwa namna fulani, kwa hiyo lazima ujue hilo na usihusianishe na uvivu wa kujitakia.
Pia kama amesoma, wengi hupenda sana kutumikisha HG, cha msingi weka mipaka kwa kuwa mambo ya ndoa hayaangalii Elimu, majukumu yako pale pale. Usijaribu kumwambia mkeo kuwa kwa kazi anazofanya HG na ukarimu wake anakutega, utaharibu- We kuwa mkali kwa HG hadi awe anakuogopa.
La mwisho kabisa, HG huwa wanakuja wakiwa wanyonge, wakishafika kwa kuwa huwa hawafikilii maisha na kila kitu kipo wanapendeza kweli kweli, zipo hadithi nyingi tena za kweli watu kibao wame wa-do. USIJARIBU Ku DO Mercury UTAVUNJA NDOA na UTAPATA AIBU MTAANI-HUTAAMINIKA TEANA.
Kukabiliana na hayo Uwe unampiga mkwara HG manake kumpiga mkwara mkeo hutaweza, ukimpiga mkwara mkeo, badaye mkitulia mkiwa kwenye bed kwisha habari, UNASAHAU na anaweza akukunyima kabisa, siku nzima hutafanya kazi vizuri.
Nawasilisha.