Naomba tujadili kwa mapana na marefu kauli hii ya Rais Samia inaashiria nini? Najua humu kuna wachambuzi na ma-time traveller wengi wanaweza kutuonesha muelekeo
Akiwa Tanga alisema jeshi lisitumike na wanasiasa. Swali, mwanasiasa gani anataka kulitumia, na analitumiaje? Kwanini sasa hivi tunaambiwa hivi wakati wanasiasa wa CCM walilitumia kwa kupewa mabus kwa ajili ya kusafirisha wanaccm
Je, wanasiasa gani ambao Rais Samia hataki walitumie jeshi?
Suala la pili, jeshi lisiwe na upendeleo upendeleo gani ambao Rais anaumia ambalo jeshi limeonekana linataka kuufanya na kumkwaza boss wao mpaka analionya au kulitaka lisifanye hivyo hapendezwi na yanayotaka kufanyika.
Nini kinaendelea na ukiunganisha tetesi za kukamatwa na kushikiliwa kwa wanajeshi au mamluki wa Uganda na wa Zanzibar ambao wako ndani ya selo za jeshi na tetesi za kukamatwa Mafwele na jeshi zinaashiria kuna kitu jikoni kinapikwa japo mpishi haonekani