Tujadili mapungufu ya Sera yetu ya Viwanda. Unadhani ina mapungufu gani?

Tujadili mapungufu ya Sera yetu ya Viwanda. Unadhani ina mapungufu gani?

TIC bado kabisa sio facilitator ktk business in Tz.. Viwanda ili vikue haraka, sera na sheria za kodi ni muhimu sana ziwe rafiki, la sivyo viwanda vyote vitauliwa na kodi ambayo sio rafiki kwa ukuaji viwanda, kodi ni jambo kubwa ndio bridge kubwa ya kufa au kukua kwa viwanda, ukiacha factors zingine kama umeme, raw materials etc.. Kodi ikikosewa tu ikiwa kubwa au mtu hajaanza hata biashara unataka kodi wakati hata kujenga tu kiwanda bado, viwanda vinakufa, nashauri mtu aanze kulipa kodi sahihi sio kubwaaa, pale tu uzalishaji unapoanza..
 
Uwwi jaman hii sera hii, nasikitik kuziona sindano za kushenea nguo ni Made in china...
 
Umetafsiri kiswahili kabisaaa,Agriculture industry haina maana kama ulivyotafsiri!
Yeah ni kweli mkuu, lakini unapo izungumzia sera ya viwanda, mimi nadhani hata hiyo Agriculture imo ndani yake humo humo. Ijapo Agriculture industry ni neno pana kidogo likiwa na maana ya tasnia ya kilimo au sekta ya ya kilimo kwa kiswahili. Lakini inabidi uelewe hivyo hivyo.
 
Umetafsiri kiswahili kabisaaa,Agriculture industry haina maana kama ulivyotafsiri!

Huyo kilaza hajui lolote, huyo ndio wale mabingwa wa kubeba mabox ya kura za wizi, ndio maana anakuja na hizo tafsiri za kiswahili. Hao ndio wale wazee wa job hundred(kazi kwelikweli)
 
Mkuu, hawa makamanda walioko humu ndo unataka mjadili nao sera ya viwanda? Uwezo wa kujadili sera wameutoa wapi? Wajadili sera halafu matusi atukane nani? Hawa ni watu wa porojo tu na mtusi tu!
 
Habari za leo wakuu,

Uzii huu utakuwa maalum kuijadili sera yetu ya viwanda.

Bila kutukana wala kumnyoshea mtu yeyote kidole, naomba kila mmoja atoe maoni yake.

Mada: Wewe unahisi sera yetu ya viwanda ina mapungufu gani?

Zingatia ili taifa letu liweze kuendelea linahitaji kuwa na sera bora ya viwanda. Sera bora ya viwanda inatakiwa kutoa dira ya maendeleo ya uchumi wa taifa.

Zingatia muda mwingine sera inaweza kuchukua mda mrefu kuleta matokeo chanya.

Sote tumeona jitihada zinazo fanywa na serikali yetu ya awamu ya tano na sita katika kutoa motisha kwa watanzania kujenga na kuanzisha viwanda.

Lakini pia tumeona jinsi ambavyo serikali imetumia jitihada kufufua taasisi za umma. Serikali imefufua ATCL, TTCL, n. k.

Zingatia mfumo wowote wa biashara ya kiuchumi hauwezi kufanya kazi vizuri bila serikali kuingilia. Hivyo ni lazima serikali nayo iingie kwenye mfumo huo ili kazi iende vizuri. Ndio sababu mnaona kwenye usafiri wa anga mnaiona serikali kupitia ATCL, kwenye mawasiliano mnaiona serikali kupitia TTCL, n.k.

Serikali ikiwa karibu na mfumo wa kiuchumi ni rahisi kupata taarifa zinazo husu mzunguko mzima wa kiuchumi, kasoro na matatizo mbalimbali. Mimi nadhani pia kuiachia sekta binafsi iendeshe mfumo mzima wa uchumi peke yake sio vizuri na swala hili lina athari kiuchumi.

Nikija kwenye swala la mchakato mzima wa sera yetu ya viwanda. Sera yetu ni nzuri sana na itatuletea faida nyingi sana huko mbeleni. Ila nilikua napenda ili sera yetu ifanikiwe asilimia 100 hasa kwenye swala la ujenzi wa viwanda, nadhani ingechagua baadhi ya viwanda vile ambavyo tunaona tunaweza kuviendesha vizuri na vikatatuletea faida nyingi kama vile utoaji wa ajira nyingi, mapato mengi na bidhaa nyingi.

Nilikua nasoma jarida moja jinsi ambavyo china wanapigana kukuza uchumi wao, wao katika sera yao ya viwanda wamechagua utengenezaji wa magari ya umeme. Hivyo nguvu yao yote wameilekeza kwenye uwekezaji wa viwanda vya magari ya umeme, utafiti na ubunifu katika viwanda vya magari ya umeme.

Naomba niishie hapa.

Hivyo ndugu yangu kama una maoni dondosha maoni yako

Usitukane.
Peleka upuuzi huko. Viwanda vipya 6000 vimeishia wapi? Hujui hata unazungumza nini wewe pimbi.
 
Naomba nichangie kwa kiasi, sera ya viwanda inapaswa kwanza kuwa shirikishi, waandaaji wasijifungie vyumbani, pili viwanda ni cross cutting sector, hapo kuna karibu wizara zote, na idara nyingi za serikali, mfano TRA, TFDA, TFC, nk, sasa ili tusonge mbele tuiombe wizara Mama, ya viwanda na Biashara ifanye uratibu stahiki ili tuanze safari sahihi ya kuelekea tunakohitaji kufika

Na zaidi ya yote kuwepo na utashi wa kisiasa unaomaanisha
Habari za leo wakuu,

Uzii huu utakuwa maalum kuijadili sera yetu ya viwanda.

Bila kutukana wala kumnyoshea mtu yeyote kidole, naomba kila mmoja atoe maoni yake.

Mada: Wewe unahisi sera yetu ya viwanda ina mapungufu gani?

Zingatia ili taifa letu liweze kuendelea linahitaji kuwa na sera bora ya viwanda. Sera bora ya viwanda inatakiwa kutoa dira ya maendeleo ya uchumi wa taifa.

Zingatia muda mwingine sera inaweza kuchukua mda mrefu kuleta matokeo chanya.

Sote tumeona jitihada zinazo fanywa na serikali yetu ya awamu ya tano na sita katika kutoa motisha kwa watanzania kujenga na kuanzisha viwanda.

Lakini pia tumeona jinsi ambavyo serikali imetumia jitihada kufufua taasisi za umma. Serikali imefufua ATCL, TTCL, n. k.

Zingatia mfumo wowote wa biashara ya kiuchumi hauwezi kufanya kazi vizuri bila serikali kuingilia. Hivyo ni lazima serikali nayo iingie kwenye mfumo huo ili kazi iende vizuri. Ndio sababu mnaona kwenye usafiri wa anga mnaiona serikali kupitia ATCL, kwenye mawasiliano mnaiona serikali kupitia TTCL, n.k.

Serikali ikiwa karibu na mfumo wa kiuchumi ni rahisi kupata taarifa zinazo husu mzunguko mzima wa kiuchumi, kasoro na matatizo mbalimbali. Mimi nadhani pia kuiachia sekta binafsi iendeshe mfumo mzima wa uchumi peke yake sio vizuri na swala hili lina athari kiuchumi.

Nikija kwenye swala la mchakato mzima wa sera yetu ya viwanda. Sera yetu ni nzuri sana na itatuletea faida nyingi sana huko mbeleni. Ila nilikua napenda ili sera yetu ifanikiwe asilimia 100 hasa kwenye swala la ujenzi wa viwanda, nadhani ingechagua baadhi ya viwanda vile ambavyo tunaona tunaweza kuviendesha vizuri na vikatatuletea faida nyingi kama vile utoaji wa ajira nyingi, mapato mengi na bidhaa nyingi.

Nilikua nasoma jarida moja jinsi ambavyo china wanapigana kukuza uchumi wao, wao katika sera yao ya viwanda wamechagua utengenezaji wa magari ya umeme. Hivyo nguvu yao yote wameilekeza kwenye uwekezaji wa viwanda vya magari ya umeme, utafiti na ubunifu katika viwanda vya magari ya umeme.

Naomba niishie hapa.

Hivyo ndugu yangu kama una maoni dondosha maoni yako

Usitukane.
 
Usichanganye tasnia na viwanda
Tatizo ni kiswahili kuwa na maneno machache ila nadhani umepata kuelewa kile nimekieleza pale mkuu. Unaweza kuelewa hivi mimi pale nazungumzia industrial policy ambayo imelenga kwenye establishment of production industries (factories) both small and large and revive of old industries (factories) like General tires e. t. c. bila kusahau lengo likiwa ni to create employments, ndio lengo kuu.
 
Huyo kilaza hajui lolote, huyo ndio wale mabingwa wa kubeba mabox ya kura za wizi, ndio maana anakuja na hizo tafsiri za kiswahili. Hao ndio wale wazee wa job hundred(kazi kwelikweli)
Tunahitaji maoni chanya mkuu, matusi hayatatufikisha popote.
 
Sera iliyopo ipitiwe upya, nahisi sera iliyopo imetelekezwa au imepitwa na wakati.

Serikali awamu hii mbona hawaonyeshi kwenye matamko wala vitendo kama inarejea kwenye sera ya viwanda?!
Je?malengo yapo?mbona Waziri wa fedha haonyeshi kwenye bajeti kuwa kodi na tozo fulani imerekebishwa kuvutia uwekezaji katika uanzishwaji na ukuaji viwanda.

Tupendekeze maeneo ya uwekezaji viwanda kwa lengo mahsusi ili kuleta maendeleo na kukuza pato la taifa.

Je?!Serikali ipo tayari kutoa misamaha ya kodi au unafuu wa kodi na kuvutia uwekezaji katika sekta ya viwanda na biashara?

Tuchukue mfano KIGOMA eneo lilosahaulika huku ikiwa na fursa ya kukuza uchumi wa nchi,unaweza kuifanya kuwa ni eneo na mkoa NAMBA 2 au 3 wenye kuongeza pato la Taifa:
1.Maeneo yatengwe kwa ajili ya viwanda katika mji wa Kigoma na yajulikane na kutangazwa kupitia TIC, na kushawishi uwekezaji wenye nafuu ya kodi kwa atakayejenga kiwanda eneo hili, na tuweke fursa ya kuweza kuuza bidhaa katika soko la nchi jirani DRC,Rwanda na Burundi.Ikiwezekana wawekezaji toka nchi zinazo ongea kifaransa wapelekwe ukanda wa Magharibi ya nchi(Kigoma),kwani DRC ni soko kubwa!Hata wachina tuwashawishi kuwekeza ukanda wa Magharibi ili kuhudumia soko la DRC.
Na msamaha wa kodi uwe kwenye Maeneo ya pembezoni tu kama Kigoma,Rukwa ili kuvutia ukuaji wa uchumi na maendeleo sawa katika maeneo haya.Wizara ya fedha wakubali "Mkakati Uchumi" kukuza na kuongeza pato maeneo yenye kupakana na nchi jirani, lakini hayakuendelezwa(Ruvuma,Rukwa,Mtwara,Kigoma)
2.Maeneo ya EPz yawepo na muwekezaji akija akute Serikali imeweka mazingira rafiki ya kibiashara(BOT wafungue ofisi iwepo kanda ya Magharibi!,usafiri wa Meli kati ya DRC na Burundi uwepo).HAIWEZEKANi watu watoke DRC waje kuchukua bidhaa Dar es salaam wakati mambo yote tungeyamalizia Kigoma na kufanya wengi wafike Kigoma na kupaisha pato la Taifa.
3.Taratibu za ufunguaji viwanda ziwe wazi
4.Wizara ya fedha ikubali kufanya kazi kwa karibu na Wizara ya Viwanda na Biashara.
 
Anapromote ujamaa lakini hatofaulu sababu Zama na nyakati zinakataa. Bila uchumi muingiliano huwezi songa.
 
Mfumo wa elimu hautoi tija kwa viwanda
 
Back
Top Bottom