Tanzania kwa mtazamo uliopo sasa wa viongozi na taasisi kama TRA, OSHA, Halmashauri za miji, NEMC, n.k;kamwe haiwezi kuwa nchi ya uchumi wa viwanda.
Usitegemee kama kutakuwa na mwekezaji mjinga ambaye ataenda kuwekeza mahali ambapo kila siku sheria na kodi zinabadilika.
Unaomba kibali, kodi tofauti, unaanza kujenga kodi imebadilika, unaagiza mitambo kodi imebadilika, unaanza uzalishaji kodi imebadilika. Bado matamko ya maDC na maRC ambao hawajawahi kujenga hata genge lakini wanataka wakuamrishe namna ya kuendesha kiwanda.
Mahali ambapo sheria na kodi hubadilika kila mara, huchochea uchuuzi na siyo ujenzi wa viwanda. Hakuna atakayeenda kujenga kiwanda mahali ambapo hujui kesho sheria itakuwaje, kodi itakuwaje, Rais atasemaje, RC na DC watasemaje, OSHA na NEMC watasemaje!!
Mataifa kama Uingereza, sheria yao ya uwekezaji, haijawahi kubadilika tangu miaka ya 1950. Siyo wajinga kufanya hivyo.
Faida inayotokana na kiwanda huchukua miaka mingi mpaka kuanza kupatikana. Kabla hujaanza yakubidi ufanye projections zako. Kwa Tanzania haiwezekani. Utafanyaje projections wakati kila siku kodi na sheria zinabadilika?
Kwa nchi ya namna hii, unafanya tu biashara ya kuagiza vitu toka China, Thailand, India, Uturuki, n.k. Ukiona sheria na kodi zimepanda, unaacha. Sasa kama umejenga kiwanda, utafanyaje?
Kwa mazingira ya Tanzania yaliyopo sasa, sahau, sahau, sahau kabisa, ujenzi wa viwanda. Vitakuwa vinajengwa vidudu fulani, vinavyofanana na viwanda lakini siyo viwanda.
VAT for wholesellers and retailers kwa Ghana ni 3%, Tanzania ni 18%. Ghana kuna wakati uchumi wake ulikuwa unakua kwa kiwango cha 12%. Rais wao ni mchumi, na mwenye uelewa mzuri wa uchumi wa Dunia.
Note: HAKUNA NCHI YOYOTE DUNIANI ILIYOKUWA MASKINI AMBAYO IMEWAHI KUPATA MAENDELEO KWA KUONGEZA KODI, ISIPOKUWA KWA KUPUNGUZA SANA VIWANGO VYA KODI NA KUONDOA KODI NYINGI.
Adui mkubwa wa maendeleo ya uwekezaji ni uwingi wa kodi na kodi kubwa.
Sent using Jamii Forums mobile app