Tujadili: Matumizi ya camera/web-cameras kwenye vituo vya kupigia kura, kwa ajili ya kuongeza uaminifu na kuzuia hujuma ndani ya vituo

Tujadili: Matumizi ya camera/web-cameras kwenye vituo vya kupigia kura, kwa ajili ya kuongeza uaminifu na kuzuia hujuma ndani ya vituo

torosi

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2020
Posts
862
Reaction score
1,430
Wapwa,

Tujadili, matumizi ya teknohama yanazidi kukua kila siku, teknohama imekuwa nyenzo kubwa ya uhuru wa mawasiliano na habari. Najaribu kufikiria vipi kama Tanzania kwa kujali umuhimu wa teknolojia, tukaamua kutumia camera kwenye vituo vya kupigia kura, je itasaidia kuongeza uaminifu/transparency na kuzuia hujuma ndani ya vituo vya kupigia kura?

Zipo baadhi ya nchi ambazo zimewahi kutumia camera na ziliona mafanikio yake
  • Urusi (2012)
  • Ukraine (2012)
  • Georgia
  • Azerbaijan (2003, 2008, 2010)
  • Sierra Leone
  • Colombia
  • Albania (2009)

Tujadili changamoto, faida na hasara za kutumia camera kwenye vituo vya kupigia kura. Je hili linawezekana kwa mazingira yetu ya Uchaguzi?

Karibuni wapwa.
 
Mie ningeshauri kura zihesabiwa wazi kama walivyofanya Kenya pale Bomas ila kura zisafirishwe na special delegates labda waangalizi wa AU.

Faida ya kura kuhesabiwa wazi mbele ya umma na mkono kwa mkono itahakiki uhalali wa kura na kuakisi uhalisia wa maoni ya wananchi kuchagua Rais au Wabunge wao.

Mbona CCM walifanya hivyo kura za maoni nadhani wakiendelea na spirit hiyo hiyo hadi udiwani ubunge na Urais watajisafisha dhidi ya makosa ya huko nyuma ya Kuiba kura.

Kinachoshangaza wanakejeli upinzani umekufa ila tume huru hawataki!! Huwa sielewi wanataka nini hasa.
 
Mie ningeshauri kura zihesabiwa wazi kma walivyofanya Kenya pale Bomas ila kura zisafirishwe na special delegates labda waangalizi wa AU...

Hili kila mtu anajua kuwa linatakiwa kufanyika, hoja ya camera itasaidia sana ulinzi na transparency ndani ya vituo vya kupigia kura, since tumeshasikia mengi machafu ambayo huwa yanafanyika ndani ya vituo hivi
 
Hii hoja CCM na Tume yao hawawezi kuikubali kabisa..!!

Yaani kwenye GIZA unataka kupeleka NURU weeee!!
Mtu anayefanya siasa za kizandiki umwambie habari hizo?!! Yaani AFRICA, bwana sijui hata tulilaniwa vipi?!!! Yaani ni full ushenzi ushenzi tuuu!! Hadi wakati mwingine una ona bora mzungu ana huruma na wewe kuliko mwafrika mwenzako!!!
 
CCM hawawezi kukubali maana huwa WANAIBA kura. Kipindi Dkt. Slaa anagombea mwaka 2010 baadhi ya kura zake za Dar zilitupwa baharini
 
CCM hawawezi kukubali maana huwa WANAIBA kura. Kipindi Dkt. Slaa anagombea mwaka 2010 baadhi ya kura zake za Dar zilitupwa baharini

Je, njia hii ina faida? kama ipo, ni zipi na kama kuna hasara ni zipi?
 
Hii hoja CCM na Tume yao hawawezi kuikubali kabisa!

Yaani kwenye GIZA unataka kupeleka NURU weeee!!
Mkuu inawezekana ila watazitoa kama zile za Lisu Dododma
 
CCTV camera za kule Dodoma zilizoondolewa na Kalemani siku ya shambulio la Lissu mmeshaziona?
 
Wapwa,

Tujadili, matumizi ya teknohama yanazidi kukua kila siku, teknohama imekuwa nyenzo kubwa ya uhuru wa mawasiliano na habari. Najaribu kufikiria vipi kama Tanzania kwa kujali umuhimu wa teknolojia, tukaamua kutumia camera kwenye vituo vya kupigia kura, je itasaidia kuongeza uaminifu/transparency na kuzuia hujuma ndani ya vituo vya kupigia kura?

Zipo baadhi ya nchi ambazo zimewahi kutumia camera na ziliona mafanikio yake
  • Urusi (2012)
  • Ukraine (2012)
  • Georgia
  • Azerbaijan (2003, 2008, 2010)
  • Sierra Leone
  • Colombia
  • Albania (2009)

Tujadili changamoto, faida na hasara za kutumia camera kwenye vituo vya kupigia kura. Je hili linawezekana kwa mazingira yetu ya Uchaguzi?

Karibuni wapwa.

Kwa post hii buku saba hawez Kuja kuchangia
 
Back
Top Bottom