Tujadili mechi ya Simba Vs Yanga leo

Yanga oyeeeeeeeeeeeeeeeeeee naona usajili wa dirisha dogo ulikuwa safi.
Aibu kwa yule Barasa na mwenzie.
 
Ni Kweli mara nyingi mpiga kelele huwa anashindwa.
Tunaomba muiombee YANGA ushindi.
 
nilisha tabiri matokeo haya mwanzoni mwa thread hii.
 
Kijana wewe ni jemadari jiniaz. umepanga tamathali na sentensi kimpangilio kulingana na ujumbe. sentensi zako zimekwenda shule, I guess unafundisha wanafunzi wa phd somo la kiswahili au wewe ni mshairi. Tunga kitabu ndugu yangu, usikalie iko kipaji. anyways, Yanga oyeeeeeeeeeeeeeeeee!
 
Hapana, lile la pili la Shamte Ally kuna jamaa alikuwa yupo muda mrefu tu kule mbele ya Kaseja hata kabla Ngasa hajapiga krosi
Ulikuwa Taifa au ulikuwa ukitazama game katika TV?
 
Hongera kwa Yanga na Pole kwa Simba.


Hapa ndipo utaona ni kwa nini Chama Cha Majambazi kinashinda kila chaguzi kwa sababu ya allegiance ya Watanzania ni ngumu kubadilika.
 
Yanga oyeeeee.Capt Hadock upo???.Mpira dakika 90 babaake na wala si maneno miiiiingi..Yanga Daima Mbele Nyuma mwiko..Timu inacheza vizuri sana sasa hivi,hope kocha kawamudu wachezaji,wapinzani kaeni mkao wa kuliwa kwenye Raundi ya pili.Xmas naisherehekea kwa Uzuuuuuri kabisa..Bravo Yanga
 
Jamani punguzeni siasa tunataka mtusimulie huo mpira ulikuaje ati! huu ni ukurasa wa kumi sasa!😕


































TEAMS:
Yanga: Yaw Berko/Obren Curkovic, Nsajigwa Shadrack, Amir Maftah, Bakari Mohamed, Nadir Haroub, Athumani Idd, Nurdin Bakari, Abdi Kassim/ Shamte Alli, Jerryson Tegete, Mrisho Ngassa, Kigi Makassy/ Godfrey Bonny.

Simba: Juma Kaseja, Salum Kanoni, Juma Jabu, Kelvin Yondan, Joseph Owino, Jery Santos/ Ramadhan Chombo, Hilary Echessa, Mohamed Banka, Mussa Hassan/ Mike Baraza, Emmanuel Okwi/ Mohamed Kijuso, Haruna Moshi.
 
mmmhhh jamani pamoja na uchawi wa kaseja aliokuwa akifanya wamefungwa kweli MUNGU ADHIAHKIWI...
 

Balatanda,
Nipo mkuu. Hii tunaita "mende kuangusha kabati." Asavali mmepona manake ulikokuwa ulikuwa unapumlia mashine hata Fidel80 alikushinda maana ulijichimbia. Hata hivyo hongereni lakini subirini marudiano kwenye premier, maana mhandisi Phiri anarudi kwenye "drawing board.'
By the way kwenye International arena mmeshatolewa hata kabla hamjaanza wakati taifa kubwa ni mwendo mdundo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…