Tujadili mshahara wa TGS D kwa watumishi wanaoishi kwenye majiji

Tujadili mshahara wa TGS D kwa watumishi wanaoishi kwenye majiji

Leverage

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2021
Posts
2,125
Reaction score
3,150
TGS D ni kiwango cha mshahara kwa mtumishi mwenye shahada ya kwanza anaefanya kazi Serikali Kuu na Serikali za Mitaa (halmashauri). Baada ya makato ya PAYE, NHIF na TUCTA kiasi kinachobaki ni around Tshs. 540,000/-. Hapo sijaweka makato ya HESLB.

Sasa hapa tuijadili hii 540,000 inayobaki. Je, inaweza kuendesha familia kwa watumishi walio mjini DSM, Arusha, Mwanza, Tanga na Mbeya?

Kwa jinsi gani kiasi hiki kinaweza tosha:
1. Kulipa kodi ya nyumba
2. Chakula cha familia mwezi mzima
3. Nauli ya mtumishi kwenda na kurudi kazini hasa DSM
4. Mavazi ya familia
5. Chakula cha mtumishi akiwa kazini
6. Elimu ni bure ila kuna nauli na hela ya kula mtoto kila siku
7. Bili ya maji, umeme na king'amuzi

Leteni uzoefu hapa mnawezaje kumudu haya yote?

Karibu kwa mchango wako
 
Hapo hapo ofsini kwenu Kuna mlinzi wenu analipwa take home

270,000, amejenga, ana mke na anasomesha watoto watano.

My take: Hakuna mshahara mkubwa Wala mdogo, Ni suala la vipaumbele vya matumizi litakalowatofautisha mfanyakazi uyu na Yule kimaendeleo
 
Haitoshi kabisa.

Ila mimi nimeshachukua maamuzi ya kuishi kama niko Kongwa ndani ndani kabisa, ili baada ya muda nikishakuwa vizuri hayo maisha ya jiji nitayaishi tuu, nafanya yafuatayo:

1. Sina mpango wa kulipia king'amuzi.
2. Napanga karibu na kazini.
3. Chakula ni kam tuko Kongwa(Harage na dagaa kwa wingi).

Ova.
 
Hautoshi kabisa. Labda kidogo kwa Mbeya unaweza kuwa na nafuu. Kwanza hapo kuna baadhi ya machinga, wauza Karanga, wapiga debe, mamalishe na 'wanyonge' wengine wanakuacha mbali sana.

Kwanza hapo hata uchumi wa kati unakuwa hujaingia. Mfano.
 
Huyo mlinzi aliyejenga ukifatilia utakuta alikuwa askari mstaafu ila sio hawa wa miaka 20-25.
Hapo hapo ofsini kwenu Kuna mlinzi wenu analipwa take home
270,000
Amejenga, ana mke na anasomesha watoto watano.

My take:
Hakuna mshara mkubwa Wala mdogo, Ni suala la vipaumbele vya matumizi litakalowatofautisha mfanyakazi uyu na Yule kimaendeleo
 
Ikifika zamu ya kutujadili sisi migambo tunaofanya kazi Posta(jijini) na kuishi Mbagala(Mkoani) nitatia neno. Na mshahara wetu ni laki mbili na nusu hadi laki 3.

Sent from my Infinix X623 using JamiiForums mobile app
Mlinzi akijenga chumba kimoja huku umri wake 50's unasema maendeleo?
 
Mleta mada atakuwa mtoto wa mama alizoea kupewa pocket money laki mbili kwa mwezi kula kulala bure nyumbani chumba self contained cha peke yake anatumia gari ya wazazi mzazi anajaza mafuta na kila kitu .Umeme maji nk mzazi sasa akipangiwa kazi na mshahara laki tano anataka aishi maisha yale yale apate nyumba self contained yenya kasebule ka peke yake ale buffet na pizza nk kama alivyokuwa akila kwa wazazi haipo hiyo.

Nina mtoto wa jirani alikataa kwenda mbinga kikazi ualimu shule ya msingi akawa anatukana wazazi wake kuwa wana vyeo vikubwa serikalini hawampendi akasema kwanini nisipangiwe Dar es salaam? Akauliza kazi ya vyeo vyenu vikubwa ni nini kama hamnisaiidii mtoto wenu wakabaki wanatoa machozi tu sababu hata hiyo ajira kuipata ni Mungu aliyesaidia. Hawakujua hata watafanyaje baada ya huyo mtoto kumaliza course ya ualimu.

Kuanza maisha inatakiwa kushuka ndio maana kunaitwa kuanza maisha ulizoea kukaa kwa watu sasa zamu yako kuanza na wewe maisha!! Panga sehemu zinaoendana na kipato na uishi maisha ya kawaida tu digrii yako is not a big deal hata vijijini sasa hivi ziko kibao watu wanazo hawana kazi.
 
Huyo mlinzi aliyejenga ukifatilia utakuta alikuwa askari mstaafu ila sio hawa wa miaka 20-25
Hakuna Askari mstaafu anaeajiliwa na serikali kuu au halmashaur na akalipwa mshahara Kwan ngazi ya TGS
 
Back
Top Bottom