Tujadili mshahara wa TGS D kwa watumishi wanaoishi kwenye majiji

Tujadili mshahara wa TGS D kwa watumishi wanaoishi kwenye majiji

Msiwaa
Sisi wa Dodoma tusubiri uzi wetu.

Ila Dodoma wanaume wasio na kipato cha kueleweka sijui wanaishije maana mji mgumu huu.
Sisi wanawake ni mtelezo tu.
Mungu awasimamie wanaume zetu mlioko Dodoma. Tuko pamoja, hatuwaachi.
Msiwaache mtawaongezea msongo wa mawazo wanapambana sana
 
Wengi humu tunakunja laki 7, baada ya makato tuna laki 5 tu. Hao wa 2mill ni wateuliwa wachache sana
Hapo hapo kwa laki 5 hiyo, bado hujakopa ili ujenge nyumba ya kuishi au unununue kagari used ili na wewe utembee ukiwa umekaa kama wengine!

Bado Bodi ya Mikopo haijachukua 15% yao ya Basic Salary! Bado hujalipa ada, kutoa michango ya harusi! Kuwatumia wazazi kahela ka matumizi, nk!!
 
Haitoshi kabisa.

Ila mimi nimeshachukua maamuzi ya kuishi kama niko Kongwa ndani ndani kabisa, ili baada ya muda nikishakuwa vizuri hayo maisha ya jiji nitayaishi tuu, nafanya yafuatayo:

1. Sina mpango wa kulipia king'amuzi.
2. Napanga karibu na kazini.
3. Chakula ni kam tuko Kongwa(Harage na dagaa kwa wingi).

Ova.
Siyo kweli kwamba sisi tunaoishi huku Kongwa ni hohehahe kama unavyotaka Jamii ituelewe hivyo. Huku Kongwa tuna ving'amuzi vingi tu ambavyo tunalipia bila wasiwasi. Pia tunaweza kula nyama kama wenzetu sehemu nyingine, kumbukeni Kongwa Beef ipo tu jirani. Hatutegemei sana kazi za kuajiriwa bali wengi wetu ni wakulima sehemu za Kibaigwa na wengine wana biashara zao nzuri tu.
 
Hapo hapo kwa laki 5 hiyo, bado hujakopa ili ujenge nyumba ya kuishi au unununue kagari used ili na wewe utembee ukiwa umekaa kama wengine!

Bado Bodi ya Mikopo haijachukua 15% yao ya Basic Salary! Bado hujalipa ada, kutoa michango ya harusi! Kuwatumia wazazi kahela ka matumizi, nk!!
Maisha magumu sana
 
Ndugu zako walikuwa waaminifu
Nilisoma sheria ajira zikawa ngumu ilinibidi nijichanganye na postgraduate ya ualimu, then niliajiriwa as mwalimu 2015 , cha kwanza nilipanga karibu na kituo cha kazi tena single room nikajiapiza sitaoa na kipato hicho, no TV, gas ndogo , nilikuwa napika , then nikawa nimeunda kikundi cha kuchangiana kila mwezi laki mbili, nilikuwa wa mwisho nilipata million moja, then nikakopa million moja na nusu bank, nikanunua kiwanja na kuanza ujenzi wa chumba sebule hapo nilijenga mwaka , nilihamia humo kama ndege , then mwaka wa tatu nilianza kununua ngombe dume nawatumia watu home wanafuga, mwaka wa tano nilikuwa na madume kama watano nilipowauza nilifungua duka na kisha nikakopa milioni 1010000 then nilianza kununua mitamba na kuwapa watu kule home, Leo hii umri wangu 35 Naoa mwaka huu, Nina mashamba kwetu makubwa as mkulima mkubwa, nimejenga nyumba standard tu mjini, namiliki canter na Nina mifugo mjini ,Nina duka kubwa tu ,nasomesha watoto wangu 1 na wajomba 2 ila salary yangu ni 249000,_so pambana tu mzee utafika huo mtaji ni mkubwa
 
Kwa wakati huu inawezekana sababu mtu anaajiriwa kwa bahati na Mungu kumpenda baada ya kukaa mtaani takribani miaka 5 hadi 7. Kwanini asiwe na mtoto anaesoma?
Walikua wanasomaje kabla ya kupata hiyo ajira au walikua kayumba then kapata kibarua anataka awapeleke Tusiime
 
Unafahamu Wafanyakazi walio ajiriwa kuanzia mwaka 2014 mpaka leo bado hawajapandishwa madaraja/ vyeo vya kimuundo! na hivyo kuishi kwa mshahara ule ule wa TGS D sawa na hawa walio ajiriwa 2021?

Kwa hiyo unategemea mfanyakazi aliyeanza kazi mwaka 2014 mpaka mwaka huu wa 2021 bado awe tu hana familia au mtoto anayesoma?

By the way, kuna wahitimu wengine wanamaliza shule/vyuo wakiwa tayari wana familia kutokana na ukweli kwamba umri una waruhusu kuwa na hizo familia!
Kwani si kuna elimu bure?

Kwanin unataka kupeleka mtoto tusiime wakati kipato tia maji tia maji
 
Kwani wee ulitakaje labda?
Ajenge bangaloo au?

Au hujawaona waliostaafu (60s) hawana hata kiwanja achilia mbali hata icho chumbani kimoja alichonacho uyo mlinzi.

Tujifunze kuappreciate ata kwa vile vidogo walivyofanikiwa wenzetu.

Kwa maana hawajavipata kirahisi wamepambana Sana mpk kufika pale kwa levo yao.
Real talk
 
Mnajichomeka kwny majukumu ya hiyari halafu mnalalamika Maisha magumu

Katoto ka miaka 2 unaenda kuzamisha 2m kufundishwa kunywa uji na vingereza vya uongo na kweli ambavyo hata wewe ukijipa masaa 2 usiku daily unaweza
Si ndo hapo
 
Watoto siku hizi wanasoma wakiwa na miaka miwili chekechea.
Hata zamani walikua wanasoma chekechea,

Shida ni kwamba watu wanafata mkumbo,mshahara kiduchu unataka kuishi maisha ya juu its either leverage your income kama ID yako au live below your earnings ukishindwa kaa kwa kutulia
 
Mleta mada atakuwa mtoto wa mama alizoea kupewa pocket money laki mbili kwa mwezi kula kulala bure nyumbani chumba self contained cha peke yake anatumia gari ya wazazi mzazi anajaza mafuta na kila kitu .Umeme maji nk mzazi sasa akipangiwa kazi na mshahara laki tano anataka aishi maisha yale yale apate nyumba self contained yenya kasebule ka peke yake ale buffet na pizza nk kama alivyokuwa akila kwa wazazi haipo hiyo.

Nina mtoto wa jirani alikataa kwenda mbinga kikazi ualimu shule ya msingi akawa anatukana wazazi wake kuwa wana vyeo vikubwa lakini hawampendi akasema kwanini nisipangiwe Dar es salaam? Akaulize kazi ya vyeo vyenu vikubwa ni nini kama hamnisaiidii mtoto wenu wakabaki wanatoa machozi tu sababu hata hiyo ajira kuipata ni Mungu aliyesaidia. Hawakujua hata watafanyaje baada ya kumaliza course ya ualimu.

Kuanza maisha inatakiwa kushuka ndio maana kunaitwa kuanza maisha ulizoea kukaa kwa watu sasa zamu yako kuanza na wewe maisha!! Panga sehemu zinaoendana na kipato na uishi maisha ya kawaida tu digrii yako is not a big deal hata vijijini sasa hivi ziko kibao watu wanazo hawana kazi.
Nafukuza takataka hiyo nyumbn kwangu atakuja kuuza nyumba na mali zenu zingine,pumbavu eti mtoto usimfokee ndio maana sinaga mda wa kuchekacheka na watoto mwisho watakuwa kama huyo
 
Good morning
Nilisoma sheria ajira zikawa ngumu ilinibidi nijichanganye na postgraduate ya ualimu, then niliajiriwa as mwalimu 2015 , cha kwanza nilipanga karibu na kituo cha kazi tena single room nikajiapiza sitaoa na kipato hicho, no TV, gas ndogo , nilikuwa napika , then nikawa nimeunda kikundi cha kuchangiana kila mwezi laki mbili, nilikuwa wa mwisho nilipata million moja, then nikakopa million moja na nusu bank, nikanunua kiwanja na kuanza ujenzi wa chumba sebule hapo nilijenga mwaka , nilihamia humo kama ndege , then mwaka wa tatu nilianza kununua ngombe dume nawatumia watu home wanafuga, mwaka wa tano nilikuwa na madume kama watano nilipowauza nilifungua duka na kisha nikakopa milioni 1010000 then nilianza kununua mitamba na kuwapa watu kule home, Leo hii umri wangu 35 Naoa mwaka huu, Nina mashamba kwetu makubwa as mkulima mkubwa, nimejenga nyumba standard tu mjini, namiliki canter na Nina mifugo mjini ,Nina duka kubwa tu ,nasomesha watoto wangu 1 na wajomba 2 ila salary yangu ni 249000,_so pambana tu mzee utafika huo mtaji ni mkubwa
 
Walikua wanasomaje kabla ya kupata hiyo ajira au walikua kayumba then kapata kibarua anataka awapeleke Tusiime
Nilimaanisha kuwa kijana amemaliza chuo anakaa mtaani kabla ya ajira kwa miaka kadhaa baadae ndio anataka ajira akiwa tayari ametengeneza mazingira ya kuwa na familia.
Si wote ila baadhi yao hivyo usimshangae anaeanza kazi akiwa na mke na mtoto
 
Yaan we unaanza kazi tu unaanza kuwa na majukumu makubwa, familia watoto wanasoma etc.
Kama JAMAA anavyodhani alipoingia pale,kila kitu kikabaki vilevile,yaani majukumu hayaongezeki kwa mwajiriwa,hivyo no annual increment.
 
Back
Top Bottom