Nilisoma sheria ajira zikawa ngumu ilinibidi nijichanganye na postgraduate ya ualimu, then niliajiriwa as mwalimu 2015 , cha kwanza nilipanga karibu na kituo cha kazi tena single room nikajiapiza sitaoa na kipato hicho, no TV, gas ndogo , nilikuwa napika , then nikawa nimeunda kikundi cha kuchangiana kila mwezi laki mbili, nilikuwa wa mwisho nilipata million moja, then nikakopa million moja na nusu bank, nikanunua kiwanja na kuanza ujenzi wa chumba sebule hapo nilijenga mwaka , nilihamia humo kama ndege , then mwaka wa tatu nilianza kununua ngombe dume nawatumia watu home wanafuga, mwaka wa tano nilikuwa na madume kama watano nilipowauza nilifungua duka na kisha nikakopa milioni 1010000 then nilianza kununua mitamba na kuwapa watu kule home, Leo hii umri wangu 35 Naoa mwaka huu, Nina mashamba kwetu makubwa as mkulima mkubwa, nimejenga nyumba standard tu mjini, namiliki canter na Nina mifugo mjini ,Nina duka kubwa tu ,nasomesha watoto wangu 1 na wajomba 2 ila salary yangu ni 249000,_so pambana tu mzee utafika huo mtaji ni mkubwa