Tujadili mshahara wa TGS D kwa watumishi wanaoishi kwenye majiji

Mshahara haujawahi tosha na haitatokea ukatosha

Kikubwa ni nidhamu yako ya pesa
Hakikisha hela yako ya mshahara inazlisha hela nyingine

540,000/- kubwa sana
Kwanza kubaliana nayo
Pili iwekee mipango na namna thabiti kabla hujaitoa bank

Zipo biashara nyingi sana mjini hasa kwenye majiji hayo ambazo mtaji wake ni mdogo sana

Kwa mfano

Nimetoka kazini saa 9.30

Saa 11 naingia kwenye banda langu la matunda ambalo limegharimu laki na nusu labda

Matunda ya elfy 20. Hapa ntazalisha 20 ngingine kabisa ambayo itakuwa nguzo muhimu ga pili 20*30
600

Hiyo na haitaji kodi ya tra wala halmashaur jipatue kitambulisho cha mjasiliamali uomdokane na kero za jiji

Dar arusha Dodoma maeneo mengi ya miji yanamsongamano mkubwa na ndio mtaji
 
Haha mshahara mdogo upo, laki tano sio mshahara ni masihara. Hata mlinzi 270k kama kajenga basi kwa hela ya ujambazi pembeni ila muongo huu huo mshahara hujengi labda kama unaongelea kajenga banda la kuku. Tuwe wa kweli maisha yamepanda.
 
Haya matunda inatakiwa uyafuate sokoni alfajiri wakati huo unatakiwa kuwahi kazini. Kuna changamoto kidogo labda uwe na kijana mwaminifu
 
Hao wengine ni motivational speakers waache tu
Haha mshahara mdogo upo, laki tano sio mshahara ni masihara. Hata mlinzi 270k kama kajenga basi kwa hela ya ujambazi pembeni ila muongo huu huo mshahara hujengi labda kama unaongelea kajenga banda la kuku. Tuwe wa kweli maisha yamepanda.
 
Lakini pia mkuu ukitoka kazini 9:30 kwa mazingira ya DSM nyumbani ukiwahi basi ni saa 11 jioni hapo ubebe matunda ukapange road hiyo ni saa 1 usiku.
 
Haha mshahara mdogo upo, laki tano sio mshahara ni masihara. Hata mlinzi 270k kama kajenga basi kwa hela ya ujambazi pembeni ila muongo huu huo mshahara hujengi labda kama unaongelea kajenga banda la kuku. Tuwe wa kweli maisha yamepanda.
Njoo katav uone vijana wadogo kabisa wanavyofa ya maajabu

Unakuta mwl wa kawaida tu mshahara wa chini ya 540 yako Ila amejenga na anapangisha na

Watumishi wengi wamepanga nyumba za Walimu
 
Amejenga na ana familia, je anaishi kwa uhuru?
Anaweza kuamua ale nini au atumie usafiri upi au mazingira ndio yanamwamuru?
Hebu kuwa na huruma basi
 
Njoo katav uone vijana wadogo kabisa wanavyofa ya maajabu

Unakuta mwl wa kawaida tu mshahara wa chini ya 540 yako Ila amejenga na anapangisha na

Watumishi wengi wamepanga nyumba za Walimu
Kwi Kwi Kwi
 
Yaani tujadili D kwa sababu gani kwani hicho ndicho kima cha chini? Hujui kuna watuwana C na wanaishi jijini?
 
Ameeen
 
Hautoshi kabisa. Labda kidogo kwa Mbeya unaweza kuwa na nafuu. Kwanza hapo kuna baadhi ya machinga, wauza Karanga, wapiga debe, mamalishe na 'wanyonge' wengine wanakuacha mbali sana.

Kwanza hapo hata uchumi wa kati unakuwa hujaingia. Mfano.
😁😁😁😁 kwamba hata uchumi wa kati hajaingia!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…