Good topic mr
Mie concern yangu kubwa ni kwa hizi allowance ambazo wanapeana kwa minajili ya kua non taxed,kama allowance za wabunge au sis offc.
Kuchukua allowance na kuja kurefund back claims
Tuziangalie hiz sheria vema na makundi ambayo tanapaswa kunufaika na hili na sio wenye nacho zaid ya wasio nacho
Allowance hizi zinatozwa kodi na sheria ya kodi ya mapato kifungu cha 7(2)(a). Kifungu hiki ndio msingi wa kutoza kodi allowances. Kifungu 7(3) kimezitaja allowance na marupurupu mengine yaliyopo kifungu cha 7(2)(a) kama yakiwa kwenye mazingira fulani basi yasamehewe kodi.
Mfano allowance unayopewa kwa ajili ya kwenda nje ya eneo lak la kazi kusimamia ili kazi za mwajiri wako zifanyike allowance hiyo haitozwi kodi. Na msingi huohuo uliopo katika kanuni ya 4(1) ya VAT General Regulation 1998 wajiriwa ama mteja akilipiwa malazi na chakula VAT ya manunuzi (input VAT) haikubaliki isipokuwa kama ni kwa sababu na nature ya kazi ama mazingira. Kwa hiyo mtumishi akilipiwa malazi wakilipiwa chakula kwa sababu yuko nje ya kiyuo chake cha kazi au yuko "site" basi kanuni hiyo huruhusu VAT ya manunuzi kudaiwa katika kifungu cha 16(4).
TURUDI KWENYE ALLOWANCES:
Kimsingi allowances zote kwa mujibu wa sheria ni lazima zitozwe kodi isipokuwa ni kwa sababu zilizotajwa kwenye sheria ya kodi ya mapato kifungu 7(3).
MISAMAHA YA KODI YA MAPATO
Waziri amepewa mamlaka ya kusamehe kodi yoyote hata kama haijatajwa kwenye jedwali la 2 la sheria ya kodi ya mapato lililoorodhesha vipato vilivosamehewa kodi.
Kodi iliyosamehewa ndio iko kwnye jedwali la pili la sheria ya kodi ya mapato ambapo item "S" ndipo tunakuta ile fedha ya mwisho kabla ya bunge halijavunjwa karibia na uchaguzi baada ya miaka mitano ya kulitumikia bunge IMESAMEHEWA.
WABUNGE WAMESAMEHEWA ALLOWANCE?
Kwa mujibu wa sheria ya kodi ya mapato ukiacha gratuity zao (malipo ya kiinua mgongo wakati bunge linavunjwa) hamna hata sehemu moja wabunge wamesamehewa allowance zao za kila mwezi zinazoambatana na mishahara yao.....hakuna kabisa hata aje professor hapa kifungu hicho hatakiona......!!!!!!Allowance zote zinatozwa kodi!!!!!!!
JE NI SAWA KWA ALLOWANCES KUTOTOZWA KODI WAKATI SHERIA HAIJASEMA?
Mimi sijui isipokuwa sheria ya kodi ya mapato kifungu cha 7 hakiruhusu ubaguzi......(discrimination).
Sasa kwa nini wenguine watozwe na wengine wasitozwe wakati wale wasiotozwa hawakusamehewa popote? Hilo ni suala la kisera na kiutawala zaidi. Tuwashauri kitaalamu ni kwa kiasi gani linaumiza.