Mkuu Gwappo...
Ahsante kwa maada hii fikirishi. Maendeleo ya wagu, ongezeko la watu duniani yameleta haya tunayaita mapinduzi ya kilimo duniani. Hapo zamani katika maeneo yetu mengi idadi ya watu ilikuwa ni ndogo saana hivi kulima kwa asili ama kwa kutumia mbegu za asili kuliweza kusaidia katika kutosheleza mahitaji husika ya watu.
Tulikuwa na mbegu za asili ambazo huzalisha kidogo , hukabiliwa na magonjwa saana,hazistahimili ukame n.k.
Ongezeko la joto duniani , kukauka kwa vyanzo vya maji ukame na mengine mengine yamepelekea kuwa na tafiti zitakazo leta mbadala wa changamoto zote hizi na kusaidia kuongeza idadi ya uzalishaji na kuepukana na changamoto za usalama wa chakula duniani.
Hata hivyo kulima kibishara kwa maana ya chakula chenye afya inawezekana tuu ... changamoto ni kuwa mtu atazalisha kidogo kwa muda mrefu na kuleta hasara katika maana ya value ya muda.
N.B.
Kilimo cha kuangalia afya ndicho kilicho bora katika kuyapa maisha yetu maana . Lakini changamoto tuliyonayo katika maendeleo yetu hayatupi nafasi nzuri katika hili