Tujadili uhalisia wa kilimo biashara cha sasa na kilimo afya

Mamlaka ya chakula na sawa KAZI ni nini kufanya Biashara au kuregulate bidhaa za chakula zimeet standards za afya KWA mlaji?
Ni vema uwaulize wahusika. Hata sigara haukatazwi na serikali kuvuta, ila wanatoa onyo kuwa ni hatari kwa afya yako huku wakichukua kodi na kuhamasisha kulima tumbaku. Mtunza afya yako si serikali, ni wewe!
 
Umechambua vizuri sana Tychob na kuonesha bayana changamoto zilizopo. Lakini fikiria kama kinyesi cha ng'ombe, kuku, nk.; tungekuwa tunakusanya na kukitumia mashambani, tusingehitaji mbolea za viwandani. Na tungepata kwa bei nafuu huku tukiwapa faida wafugaji nao wakikusanya kwa wingi ili wauze badala ya kutupa ovyo.

Mbolea ya mabaki ya mimea (mulching) nayo tunatupa au kuchoma moto badala ya kuozesha ili irudi shambani kurutubisha ardhi.

Tunapaswa kubadili mtazamo wa kufikiri kwetu (change of mindset). Tunavyoona ni duni ndivyo vilivyo bora. Mtu akila bamia, mlenda au mchicha kwa viazi vitamu anaonekana amekula chakula duni kuliko aliyenunua hamburger au nyama za kwenye makopo super market!

Tunanunua kwa bei kubwa vya kuharibu miili wakati vya bei ndogo ndivyo vyenye faida kubwa mwilini.
 
Ni vema uwaulize wahusika. Hata sigara haukatazwi na serikali kuvuta, ila wanatoa onyo kuwa ni hatari kwa afya yako huku wakichukua kodi na kuhamasisha kulima tumbaku. Mtunza afya yako si serikali, ni wewe!
KWA hiyo Ina maana tunayo mamlaka isiyojali afya ya mlaji ?
Mamlaka hiyo iliwekwa na kina sisi au wawakilishi wetu si ndiyo?
Wawakilishi wetu ndiyo sisi si ndiyo?


Kutokana na ongezeko Kubwa la watu ,tukiendelea kutumia njia za asili Tunaweza timiza mahitaji ya chakula KWA kutumia njia ulizozitaja hapo juu?

Mass production inawezekana KWA mfumo huo?
 
Unazo akili, acha baya chukua jema. Usifanye jambo kwasababu wengine wanafanya au kwasababu serikali haijakataza. Jali afya yako mwenyewe maana ndiyo mtaji wako wa kwanza kabla haujawa wa serikali.

Ukiona Simba anakuja kukuparura usisubiri serikali itangaze kumkimbia - kimbia mwenyewe!
 
Tunafanya ubishi , umuch know, tunatafuta ushindi au ni tunatafuta suluhu ya Kupata chakula bora na salama?

Umeusoma mchango wangu ukauelewa?
 
Tunafanya ubishi , umuch know, tunatafuta ushindi au ni tunatafuta suluhu ya Kupata chakula bora na salama?

Umeusoma mchango wangu ukauelewa?
Ninachoandika ni ushauri tu kwa yeyote yule, una uhuru wa kuufuata au kuupuzia na hutalaumiwa. Na hakuna ubishi wala ushindani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…