Tujadili ukweli kuhusu Stem cells(Seli Shina)

Tujadili ukweli kuhusu Stem cells(Seli Shina)

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Nimekuwa na mgonjwa wa kansa. Nikawa na jamaa akanishauri kujaribu seli shina. Nikaungwa na mtalaam. Akanidokeza vitu vizuri kiasi cha kusema baada ya mwezi atapata nafuu kubwa hata kuachana Chemotherapy hapa Ocean Road.

Napata mashaka isijekuwa ni promo tu auze. Bei yake kubwa kiasi dozi ya mwezi na nusu ni laki 5. Japo kwangu sio shida, napambana mdogo wangu apone.

Sasa humu kuna watalaam wengi wanajua ukweli wa hivi vitu. Lakini pia kuna watu wana shuhuda. Kabla sijatoa hii laki 5.

Doctor anasema stem cell inasaidia;

1.Suluhisho kwa magonjwa zaidi ya 200
2. Kulinda seli shina za ngozi na mionzi hatari ya UV

3. Kuchelewesha kuzeeka kwa ngozi

4. Kuondoa sumu mbalimbali mwilini

5. Hulinda au kupunguza hatari ya uharibifu wa macho

6. Kuongeza kinga ya mwili na kuwa imara

7. Huongeza afya ya mfumo wa moyo

8. Huimarisha mishipa, viungo na mmeng'enyo wa chakula

9. Kuweka sawa mzunguko wa damu na cholesterol

10. Husaidia kuongeza damu kwenye mwili kwa wale wenye upungufu Bidhaa hizi ni 100% Natural na 100% Halal.
 
Binafsi sijui kuhusu ila nikiona dawa moja inatibu magonjwa mia moja red light inawaka kichwani naona ni promo tu.
 
Japo ujaeleza ni kansa ya wapi ngozi,utumbo,meno,matiti,ini lakini Stem cell ni UPIGAJI kwasababu inachotaka kufanya ni kama upandikizaji wa Cell mpya na izi Cell mpya zikikutana na zile halisi lazima reaction itokee kubwa kwa lugha nyepesi Side effects zake ni kubwa kuliko faida zake ivyo sikushauri Fata ushauri wa Daktar bigwa achana na wahanga njaa

Sent from my kiswaswadu using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom