Tujadiliane kuhusu michongo.

Tujadiliane kuhusu michongo.

Kwa swali ulivyouliza utasubiri sana

Kila biashara, kila secta, kila kazi inalipa. Ni wewe na unavyoifanya
Currently Kuna michongo mipya kila kukicha mfano kwa Sasa Kuna vijana jobless kupitia may be Uzi huu anaweza kujikwamua kiuchumi
 
Michongo ya kujiajiri na kufunga biashara na makampuni binafsi pamoja na shughuli za ubunifu ingekuwa bora zaidi
Mfano kwangu Mimi Nina fursa moja kwa mtu mwenye mtaji mzuri

BIASHARA YA KUSAFIRISHA DAGAA KUTOKA MWANZA HADI DAR ES SALAAM

Wazo la Biashara:
Biashara hii inalenga kununua dagaa moja kwa moja kutoka machimbo ya dagaa jijini Mwanza kwa bei ya jumla (takriban 500,000 TZS kwa gunia), kisha kuwasafirisha hadi Dar es Salaam ambako wanauzwa kwa bei ya rejareja kati ya 1,200,000 TZS hadi 1,500,000 TZS kwa gunia.

Hatua za Kuanzisha Biashara:
Tembelea machimbo ya dagaa Mwanza ujue bei ya wastani kwa gunia.Tafuta wateja Dar es Salaam, kama wachuuzi wa masoko ya mabibo, Tandale, au maeneo yenye uhitaji mkubwa wa dagaa.Nunua dagaa wenye ubora mzuri kwa bei nafuu kutokana machimbo ya dagaa.
•Nb.Hakikisha unajua msimu mzuri wa dagaa ili kuepuka kukosa bidhaa.


Tafuta njia bora ya kusafirisha dagaa, kama kutumia malori ya mizigo au mabasi makubwa.
Funga dagaa kwa usafi na ulinzi wa hali ya juu ili wasiharibike.
Tafuta wateja kabla ya kusafirisha dagaa ili kupunguza muda wa kuhifadhi bidhaa.Wasiliana na wauzaji wa rejareja wa Dar es Salaam na wape ofa nzuri kwa dagaa wa ubora.




Faida iliyopo kwenye hii Biashara:

Bei ya Kununulia Mwanza: 500,000 TZS kwa gunia.

Gharama za usafiri: 100,000–150,000 TZS kwa magunia (inategemea njia ya usafirishaji pia idadi ya gunia isiwe moja).

Gharama nyingine (hifadhi na usafi): 50,000 TZS kwa magunia.

Jumla ya gharama: Takriban 650,000 TZS kwa gunia.

Bei ya kuuza Dar es Salaam: 1,200,000–1,500,000 TZS kwa gunia.(Rejareja kwa sado)

Faida kwa gunia moja: Takriban 550,000–850,000 TZS.


Faida ya Mwezi:
Ikiwa unasafirisha magunia 10 kwa mwezi, unaweza kutengeneza faida ya 5,500,000–8,500,000 TZS, kutegemea bei na soko.

Mwisho kabisa,Kuna mdau siku moja tulikuwa nae Twitter anasema anazungusha mpaka 300M per month using 100M sijajua kama ilikuwa ni kweli au ni kamba lakini ni moja ya biashara ambayo inapesa sana ukitembelea Twitter (X) uka search Tricy Dagaa utaona jinsi anamafanikio makubwa kwenye hii biashara.
 
Back
Top Bottom