Tujadiri kuhusu wakazi wa Mwanza wanaoishi milimani kuhamishwa

Tujadiri kuhusu wakazi wa Mwanza wanaoishi milimani kuhamishwa

Lyetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2018
Posts
1,268
Reaction score
3,429
Habari za usiku wapendwa katika bwana.

Nimeona ni vyema hili suala tukalijadili ili tuone kama linamanufaa au hapana.

Mimi nimekulia Igogo ambapo ni moja ya sehemu iliyotajwa wakazi wake watapaswa kupisha uwekezaji, hadi hivi sasa wazazi wangu wanaishi Igogo, Igogo napajua vyema.

98% ya wakazi wa Igogo ni masikini sana, Je huu mpango wa kuwahamisha hatuoni kama utakwenda kuwanufaisha?

Ntakupa mfano.

Mkazi wa igogo anayeishi kwenye nyumba iliyochakaa yenye mabati ya mapipa tena inavuja, asiye na uwezo wa kujenga makazi mapya, kipato chake kinatosha kula tu hata mavazi ni changamoto.

Lakini mkazi huyu eneo lake lina thamani ya milioni 40. Je tumuache aendelee kuishi hapo kwenye makazi yaliyochakaa au tumpe M40 akajenge makazi mapya eneo lingine.

Igogo imepakana na chuo cha bugando ambacho kinahitaji makazi ya karibu kwajili ya wanafunzi na wafanya kazi.

Wakazi wa igogo wameshindwa kuitumia iyo fursa kwa sababu hawana uwezo. ( makazi machache yanayokidhi mahitaji yamejengwa na watu kutoka nje ya Igogo)

Igogo ni karibu kabisa na kati kati ya jiji ambapo wafanya biashara wakubwa wanahitaji majengo ya kuhifadhi bidhaa zao.

Wakazi wa igogo wameshindwa kutumia hiyo fursa ya kujenga majengo ya kupangisha kwajili ya wafanya biashara wakubwa kuhifadhi bidhaa zao kwa sababu hawana uwezo.

Igogo ni eneo zuri ambalo limetizama ziwa ambapo panafaa kwa Ujenzi wa hotels nzuri ila wakazi wa igogo wameshindwa kuitumia hiyo fursa kwa sababu hawana uwezo.

Je, tuendelee kuwaacha waishi hapo kwenye nyumba chakavu kwenye eneo ambalo automatically linahitaji uwekezaji ambao wanaigogo hawaumudu?

Je, kuwaondoa Igogo watu hawa wanaoishi maisha duni kutawahathiri kwa namna yoyote?

01e2914ba25eec5dcca1c9adc2718a30.jpg


slum+tourism+mwanza+1.jpg
 
Ni jambo jema jiji linapaswa li reflect hadhi yake sio kuwa na slums katikati ya jiji..wahamishwe tu kwa manufaa mapana ya ustawi na maendeleo ya jiji.

Afrika tubadilike.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kwa hiyo masikini watakuwa wanahamishwahamishwa kwenye maeneo yao kila panapoonekana pana fursa? Kila sehemu ina fursa nyingi kwa maana hii masikini watahamishwa sana tu kila waendapo
 
Hata mimi nikizobumba naenda waamisha mahala flani Kirumba, uzuri kwenyewe hamna nyumba, ila hamna barabara pia, japo ikiwepo barabara kunafikika kirahisi.

Ili mji wa Mwanza ubadilike unahitaji uwekezaji wa maana.
 
Walipwe tu iwafaidishe isiwafaidishe ni juu yao
 
Kwa hiyo masikini watakuwa wanahamishwahamishwa kwenye maeneo yao kila panapoonekana pana fursa? Kila sehemu ina fursa nyingi kwa maana hii masikini watahamishwa sana tu kila waendapo
Aisee wahamishwe,niliingia Mwanza mara ya kwanza mwaka 1995 nikiwa na hamu kabisa ya kuiona Mwanza, nilishangaa kuona vijumba cha Igogo na Kirumba mlimani,nikajiuliza hii Ng'wanza waesamayo???Mwanza inaharibiwa image ni hivi vilima ,ni heri wangepanda miti kuliko kujenga huko,miji ya wenzetu wanaojenga milimani ni matajiri but kwa mza maskini ndo wamejenga milimani halafu cha ajabu serikali imewapelekea maji na umeme tena kwenye makazi holela jaman jaman
 
Back
Top Bottom