Ni kipindi kizuri cha kupumzika bia ili kusafisha ini, kunywa maji mengi, juice na matunda kwa wingi! Pia ni kipindi kizuri kuacha ngono zembe!!
Lakini naomba kuuliza swali la msingi, kwa wale waliokwenda kwenye misa za Jumatano ya majivu jana, yale majivu maana yake nini?
ni kweli kabisa, unajua kuna faida sana ya kupunguza haya magud taim tunayoyala mazee
Kazi kwangu ni kupunguza ile alcohol, yaani nikiangalia serengeti inavuja jasho ndio napata shida lakini nimepasi jana kwahiyo zimebaki 39.... tartiiibu najikongoja
dadangu hapa nakupa mia pasenti, lakini tukumbuke sisi si wakamilifu na lazma pawe ka pa kuanzia mema au kupunguza mabaya, na nyakati kama hizi za toba ndio mahala pake
mimi si mkamilifu na najua siko peke yangu, ila tukianzia kipindi hiki tunapata nguvu ya ziada kwale wanaotuombea na pia tunakuwa wengi kwa mpigo hivyo kupunguza vishawishi
sasa kwa sisi wenye ndoa zetu?...:d
Hahahahahahaha! Yaani nimecheka kwa sauti! Duh! Unavyohesabu siku, tunaomba siku uzalendo ukikushinda uje utuambie hapa tafadhali!
do the oppositesasa kwa sisi wenye ndoa zetu?...😀
hayo mabadiliko ni kwa ajili ya kwaresma tu au ndiyo mwanzo wa kubadilika? kama ndo mwanzo wa kubadilika basi hongereni ila kama ni kwaresma tu bora muache maana utakuwa ni unafiki.
Ni kipindi kizuri cha kupumzika bia ili kusafisha ini, kunywa maji mengi, juice na matunda kwa wingi! Pia ni kipindi kizuri kuacha ngono zembe!!
Lakini naomba kuuliza swali la msingi, kwa wale waliokwenda kwenye misa za Jumatano ya majivu jana, yale majivu maana yake nini?
- kupunguza tungi kwa zaidi ya 50% maana kwa sasa hazipiti siku mbili mtu lazma ushtue tena si kidogo
Wakuu asalaam aleykum;
Jana katika pitapita yangu nikatua kwenye nyumba ya ibada ili kujiandaa vyema kwa ajili ya hiki kipindi cha kwaresma
kupunguza tungi kwa zaidi ya 50% maana kwa sasa hazipiti siku mbili mtu lazma ushtue tena si kidogo
HEHEHE!kwenye redi hapo lol!Mimi napunguza 100%
Maeneo yafuatayo naomba msinitafute, nitakuwa ibadani (Nasali, Natubu na Kuamini Injili):-
- Calabash (Mwenge)
- New Africa (Happy Hour)
- QBar (Nime-lipia Dstv tayari)
- Billionaire Club (Msasani)
- Makumbusho/Msasani Club (Nyoshi Al-Sadaat usinibeep)
- Bamboo (Akaunta usitume tafadhali nipigie)
- Na Nyumba zote za kulala Wenyeji za Gongo la Mboto na Sinza ( Vyumba Uza kila Ijumaa jioni msiniweeke)
Tubuni na Kuamini Injili