Tujenge Tabia ya kujitazama kwenye vioo

BabaMorgan

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2017
Posts
4,869
Reaction score
13,137
Kuanzia mwishoni mwa mwaka 2019 mpaka sasa hali yangu ya kiuchumi imeyumba kama kijana nipo katika harakati za kuhakikisha narudi kwenye hali nzuri ya kiuchumi tokea mwaka Jana nimekuwa mtu nisiyefocus sana kwenye muonekana kuanzia mavazi mpaka style ya kunyoa kwa hiyo mi na kioo tumekuwa tofauti kama kaskazini na kusini.

Recently nimekuwa nikipokea shikamoo nyingi Mara ya kwanza sikuchukulia personal kutokana na ukanda niliopo kusifika kwa heshima ila kadri siku zinavyoenda ndio nashtuka sababu hata wale ambao nina imani wananizidi umri wananipa shikamoo ndipo wazo la kujiangalia kwenye kioo likanijia nikapita kununua kioo cha buku nikaenda kutulia zangu Nyumbani nakujicheki.

Mpaka sasa siamini nilichokiona inshort nimeiona sura ya mzee mfanano wa Aliens Ila saa hivi nimetoka naelekea saluni kunyoa kwanza. Pamoja na mihangaiko Ila tujenge mazoea ya kujiangalia kwenye kioo maana kuna siku unaweza kuwahukumu wachawi kuwa wamekubadilisha sura kumbe uzembe wako wa kutojipenda na kujiangalia kwenye kioo.
 
Hivi kwann TZ hakuna salamu ya jumla ambayo mtu wa rika lolote awe na uwezo kumsalimia mtu yeyote bila mtafaruku mbali na shkamoo

Habari za Sahivi Kaka/Madam/Ndugu/Rafiki? Hii ipo poa.
 
Mad Max Niliwahi kumsalimia dada mmja ambaye ni mkubwa kidogo kwangu, "habari ya arubuhi" manake niliona kama shkamoo ataona namzeesha iv, hakujibu akasema iv we wa kuniambia shkamoo mm, dah wakati kuna wakubwa zaid yake huwa nawapa shkamoo wanaipotezea kiaina hata tukikutana mara ya pili siwez kumpa tena shkamoo
 
Hebu jipige selfie kwanza halafu ututumie humu tuone kama kuna ukweli wa kile unachokisema.
 

Mkuu, wanawake hawatabiriki ikija issue ya shikamoo. Nextime mlie kavu tu
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚
 
Hivi kwann TZ hakuna salamu ya jumla ambayo mtu wa rika lolote awe na uwezo kumsalimia mtu yeyote bila mtafaruku mbali na shkamoo
 
Basi Kuna mzee mmoja mwenye miaka kama 50+ ivi kitaa akisalimiwa na wadada anaitikia kwa kusema "Asante"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…