Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Wenye hoteli za njiani wengi hawatapenda hili bandiko. Lakini kusafiri na chakula ni muhimu hasa unapokua na watoto. Bei ya vyakula njiani ni kubwa pia ubora wake unatia mashaka.
Unakuta viazi vitamu viko kwenye karai vimepata vumbi la kutosha tu, vingine unanunua unagundua vimeanza kuoza havikua vya jana, vilibaki juzi na muuzaji anaokoa mtaji wake.
Fikiria uko na watoto, basi limesimama wote wnanataka kujisaidia, mkimaliza huduma hii, dereva ameanza kupiga honi mnatakiwa mrudi kwenye gari safari iendelee. Ukute dereva yuko kwenye ligi na dereva mwenzake wa basi lingine. Ukimfahamisha watoto hawajakula anaona unampotezea muda.
Gari linaweza kuharibika katikati ya pori.
Kama unasafiri na watoto andaa kikapu ndani weka chupa za maji, mkate, ukiweza nunua kilo ya nyama chemsha na uikaange. Matunda pia usisahau karatasi za kusafishia mikono.
Kuwa mstaarabu, mabaki ya chakula yahifadhi vizuri uyatupe sehemu stahiki.