Tujenge utaratibu wa kusafiri na vyakula vya kula njiani

Tujenge utaratibu wa kusafiri na vyakula vya kula njiani

Mimi wiki hii nilisafiri Arusha na Kurudi Dar jana, kwenda na kurudi nilikula karanga na korosho tu + maji, maana hili tumbo siliamini tena [emoji23][emoji23][emoji23] tena sehemu ya kula derva katupa dakika 10
Katika hizo dakika 10 kuna foleni chooni
 
Sijawahi kusafiri bila chakula.

Hii ni fundisho tangia udogo wetu kwani mama always alikuwa anaandaa maandazi na nyama za kukaanga na maji ya kutosha enzi zileee
Na kama ni safari za train kama ni mbali anahakikisha tunabeba na chupa ya chai ( najua vijana watanishangaa).

Ila huo ndio ulikuwa mfumo wetu. Na mpaka sasa ni mhenga wala sijutii kubeba kidogo

Nakumbuka kuna siku bus liliharibika njiani tena porini tulikaa masaa 4 tukisubiri spea ila kwa kuwa nilikuwa na vitafunio nikaenda na kukaa chini ya mti kabisa
 
Hata hivyo kula kula njiani si vizuri sana.
 
Wenye hoteli za njiani wengi hawatapenda hili bandiko. Lakini kusafiri na chakula ni muhimu hasa unapokua na watoto. Bei ya vyakula njiani ni kubwa pia ubora wake unatia mashaka...
Leo umeongea point tupu.

Tujenge nchi yetu, tulinde mazingira, tulinde afya, tuokoe uchumi wa familia.
 
Hapo dereva amebeti na mwenzake, ukiwa na tumbo la kuhara pole.
Aisee na wale wa kisukari sasa wa kujisaidia lila saa. Nilipanda Ally's nikakaa na mtu mzima dah yaliyotokea njiani yalihuzunisha sana
 
Back
Top Bottom