KERO Tujengewe kivuko imara, hili daraja Mtaa wa Kanga, Kinyerezi Mwisho mvua ikinyesha inakuwa hatari kwa wavukaji

KERO Tujengewe kivuko imara, hili daraja Mtaa wa Kanga, Kinyerezi Mwisho mvua ikinyesha inakuwa hatari kwa wavukaji

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Jamii Forums imekuwa nguzo muhimu katika jamii, hiyo ni kutokana na kuwezesha Serikali na mamlaka nyingine mbalimbali kutatua changamoto zinazowasilishwa na sisi Wananchi.

Kuna daraja liko Kinyerezi Mwisho ukiwa unaelekea kwa Komba ambalo hasa linatumiwa na Watembea kwa miguu, tunapata shida sana kupita nyakati za mvua.

Mvua ikinyesha unaweza kusubiria kwa saa tano ili maji yaishe au yapungue ndio uweze kupita hapo, ikitokea mtu una haraka au una dharura inabidi ulazimike kutumia njia mbadala ya kuzunguka kwa kuwa eneo hilo lililopo Mtaa wa Kanga haliwezi kupitika muda huo.

Tunaomba msaada wa kidharura tupate kivuko cha juu, Mkuu wa Mkoa, Mh Albert Chalamila alishawah kuja mwanzo wa Mwaka 2024 akaahidi kuwa baada ya wiki mbili daraja la dharura litajengwa ila mpaka sasa kimya.

Tunaomba sana tufikiriwe maana madhara mengi yameshatokea eneo hilo, waathirika zaidi ni Wanafunzi, wajawazito na wagonjwa.

 
Back
Top Bottom