Mad Max
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 26,961
- 77,890
Tuanze na nini maana ya Cruise Control?
Kwa maneno yangu, Cruise Control (CC) ni teknolojia iliopo kwenye magari inayosaidia gari litembee katika speed fulani aliyoiset dereva bila dereva kupunguza au kuongeza kwa kukanyaga mafuta au breki sana sana anapokua highway au barabara nyeupe isio na jam sana.
Kwahiyo inamsaidia dereva kupunguza kuchoka wakati wa kuendesha, inaongeza fuel efficiency, na inamfanya dereva ku-relax.
Sasa hii teknolojia ya CC haijaanza leo au jana, ilikua tokea kitambo ambapo ilikua simple tu kwamba gari inatembea speed fulani lakini siku hizi imeimprove kiasi inaweza hadi kupunguza au kuongeza speed kutegemea hali ya barabara.
Sasa ili kuielewa vizuri CC tuanze kwanza kujua aina zake, hapa tutazidiscuss aina nne tu ingawa najua zipo nyingi:
1. Cruise Control ya kawaida.
Hii ni basic CC ambapo baada ya dereva kuset speed anayotaka (tuseme mfano 60 km/h) gari itatembea speed iyo iyo hadi atakapoamua kucancell kwa kubonyeza button au kubonyeza breki.
Kwahiyo dereva anaanza kwa ku-activate CC (tuseme kuiwasha) kwa kubonyeza button ya CC, kisha dereva ana-set speed anayotaka, mara nyingi kwa kutumia buttons zinakua na alama ya + au - zilizopo kwenye steering wheel.
Baada ya hapo gari litaanza kutembea hiyo speed aliyoset hadi dereva atakapoamua kuongeza au kupunguza au ku-cancell CC.
Hii ipo kwenye magari mengi tokea ya miaka ya 90s, ila hasara yake kuu ni kwamba dereva anatakiwa kua makini kwani alichosaidiwa yeye ni kumaintain speed tu.
Mfano gari kama Nissan Xtrail 2008, Mitsubishi RVR 2010, nk.
2. Adaptive Cruise Control (ACC)
Hii inafanya kazi kama CC ya kawaida ila kwa kutumia camera, radar na sensors mbalimbali inauwezo pia wa kupunguza na kuongeza speed kutegemea na gari iliopo mbele au kitu kilichopo mbele.
Kwamfano, ukiwa umeset speed 60 km/h kama kwenye CC ya kawaida, ila gari la mbele yako likapunguza speed ikawa mfano 30 km/h inamaanisha na gari lako litashuka speed hadi 30 km/h kuendana na gari la mbele. Kwa English tuseme lime-adapt. Na gari la mbele likiongeza hadi 100 km/h lako litaongeza ila litaishia 60 km/h ile ulioset.
Hii ni nzuri zaidi aya CC ya kawaida kwani unaweza usiguse kabisa breki au mafuta kwa umbali mrefu sana ukiwa highway.
Kwakua inatumia camera na radar, kukiwa na mvua sana au ukungu au radar zikizibwa na matope/vumbi inaweza kupata shida kidogo.
Kumbuka magari mengi yenye ACC hayana uwezo wa complete stop, yaani kama gari la mbele limepunguza speed hadi kusimama lenyewe likifika speed flani (mfano 25 km/h) linalia alarm na kukuachia dereva umalizie.
Na pia, ata kama ACC ipo ON, inaanza kufanya kazi baada ya kufika speed flani, mfano 30 km/h ndio linajiendesha.
Magari kama Mazda CX-5 ya 2016, Subaru Forester 2017, Harrier 2013 yana hii kitu.
3. Dynamic Radar Cruise Control (DRCC) au Trafic Jam Assistant au Stop and Go CC
Hii ni advanced version ya ACC ambayo inaweza kupunguza speed hadi kusimama kama kwenye mataa iwapo gari la mbele limesimama. Na likianza kuondoka nalo linaamsha.
Kwahiyo hii version ya CC imeziba mapungufu ya ACC kwakua yeye anaweza kufika hadi 0 km/h na anaweza kuanzia 0 km/h kuanza kuondoka.
Mara nyingi teknolojia ya CC inakuja na majina kama City Driving Assistance au Trafick Driving Assistance kwasababu inafaa ata kwenye low speed.
Mfano kwenye Crown ya 2016, Rav-4 Hybrid 2019, Honda CR-V 2020, CX-5 ya 2018 nk.
4. Predictive Cruise Control (PCC)
Hii ni next level kwasababu inatumia GPS, ramani, sensors camera, radar nk kubadirisha speed kutegemea na magari ya mbele na hali ya barabara mfano kuna kona kali yenyewe inapunguza speed.
Iko complicated inavyofanya kazi kwani inatumia teknolojia ya gari na navigation system kujua ni speed gani inahitajika muda flani.
Kwakua inatumia navigation, lazima kuwe na GPS data ya high-quality. Kua na WiFi muda wote sio lazima, ila lazima uwe umesha-download ramani kwenye gari.
Magari ya Kijerumani kama 5 Series ya 2017, E Class ya 2019, A6 ya 2021 yana hii teknolojia.
Kwahiyo ni zipi faida za kua na CC na kuitumia muda muhafaka?
Kama tulivyosema hapo juu, faida zipo nyingi kuu kabisa kupunguza uchovu wa dereva especially kwa safari ndefu, pia kuongeza fuel efficiency kwani gari ina accerelate smooth kuliko dereva au rahisi ku-maintaint constant speed, pia inazuia ku-overspeed mfano upo kwenye vibao vya 50km/h ukiset 50km/h itabaki iyo iyo, na pia inaongeza comfortability.
Lakini, pamoja na kua na faida, matumizi ya hii kitu yanapunguza umakini wa dereva sana maana dereva anakua analiamini gari litasimama likifika somewhere bahati mbaya malfunction halisimami, pia kuna baadhi ya barabara sio nzuri kwa CC kwakua nyingi hazidetect vitu kama matuta au barabara mbovu, na pia kama kuna hali ya hewa ya ukungu au mvua kali haitaperfom vema.
Kwa mtazamo wangu CC ni nzuri sana, na kama ni mtu wa kusafiri safari ndefu (highway) nadhani ni moja ya feature ya kuizingatia wakati unatafuta gari jingine.