Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Akhsante Mungu fundiHongera sana mkuu.
Si useme tu Chris Lukosi badala ya kumung'unya maneno?Zamani, miaka ya 1983 nikiwa nafanya kazi Mutex, Musoma. Tullikuwa na ofisa mmoja wa ngazi za juu.
Inasemekana alikuwa ni mmoja wa wasomi wachache wa taaluma ya viwanda vya nguo enzi hizo. Tatizo lake lilikuwa moja. Saa zote alikuwa amelewa.
Enzi zile ilikuwa sio rahisi kufukuzwa kazi. Jamaa alikuwa wakati wowote amelewa. Asubuhi akienda kunywa chai lazima asindikize na glasi ya whisk. Wakati mwingine ililazimu apelekewe hati mbalimbali aweke sahihi akiwa baa. Lakini, hakuna aliyemkemea.
Hakuna kiongozi, jirani, wala mfanyakazi mwenzie aliyeweza kumkalisha na kumwambia hii sio nzuri kwa mstakabari wa afya au kazi yako. Niliondoka nikamwacha. Sijui kilichoendelaea.
Kwa sasa kuna watu maarufu, wana majina, wanafanya kazi vizuri lakini maisha yako nyuma ya pazia ni maisha ya ulevi wa kupindukia, umalaya, madawa ya kulevya n.k.
Matokeo yake tunaishia kupoteza vijana watenda kazi ambao kama wangekemewa, kushauriwa, kuambiwa, kuelemishwa labda wangesikia na kubadilika ili kuendana na maisha bora. Lakini tunapowapoteza kunakuwa na mbwembwe nyiiingi kwenye mazishi yao.
Hivi wanapokuwa wanayatenda hayo walio karibu nao hawawezi kuwakemea?