Tujifunze kujuliana hali kihisia si mafanikio tu

Tujifunze kujuliana hali kihisia si mafanikio tu

robbyr

Senior Member
Joined
Apr 8, 2017
Posts
129
Reaction score
221
FB_IMG_1725290254588.jpg

Picha: Pinterest

Tangu umekua na kujitambua kila mtu unayekutana naye huuliza una kazi, una nyumba au umeoa au utaoa/ kuolewa lini.

Maskini hukuna anayewahi kukuambia ikiwa una furaha au laaa!!!

Maisha si kama mlolongo wa kununua nyanya na mbogamboga sokoni.

Tambua kuwa wale wanao ziona dhoruba au taabu machoni pako, ukimya wa sauti yako na uzito ndani ya moyo wako ndio unahitaji kuwaruhusu kuwa sehemu ya maisha yako.

Tujifunze kujuliana hali kihisia kwani tutaokoa wengi na msongo wa mawazo, huzuni, na hata kutoa tumaini na nuru ya ushindi kwao.

Asante
 
Ni sahihi unalosema, lakini kwa dunia ya sahivi kumshirikisha mtu yako ya moyoni ni risk sana . Maana anaweza kuyatumia kama fimbo ya kukuchapia
 
Back
Top Bottom