Tujifunze kusamehe

Tujifunze kusamehe

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Huyu shost alipata mimba akiwa darasa la saba B, shost kaumbika mashallah. Wazazi walisononeka lakini walipiga moyo konde na kumsaidia binti kulea mimba. Binti alikwenda kufanya mtihani na mimba yake ingawa aliacha kwenda shule hivyo alipata cheti cha darasa la saba.

Baada ya kujifungua wazazi wake walimpeleka kwa mama yake mdogo akaendelee na shule wakati wao wanalea kichanga, Alifaulu vizuri na kujiunga na chuo baada ya darasa la 12. Alipata ajira na mume na kuolewa kwa chereko chereko.

Kwa mume uzazi uligoma kabisa, lakini mume wake alimpenda sana na alimpa zawadi na Vito vya thamani. Kuna wakati mume alimnunulia mkufu mzuri wa dhahabu.

Pale nyumbani aliishi na watoto wa wifi zake waliokuwa wanasoma na mtoto wake alikuwa likizo kwa mama lakini aliishi kwa babu na bibi yake. Kuna wakati ule mkufu wake wa dhahabu ulipotea shost aliutafuta sana na kuuliza lakini hakupata jibu. Mume alimwambia asamehe tu atamnunulia mkuu mwingine hali itakapo ruhusu lakini shost aliamua kwenda kwa mganga kununua jini makata kwa aliyeiba mkufu wake.

Baada ya wiki moja analetewa habari ya kifo cha mwanae, shost alifikiria ni watoto wa wifi zake ndiyo alwaliiba mkufu. Msiba huu ulimpa simanzi kubwa kwani uzazi kwenye ndoa ulikataa kabisa.

Kama shost angekuwa na moyo wa kisa when haya yasingemkuta.
 
Madam unaonekana na wewe una mashost weng sana tandale enhhee nna waswas wewe utakuwa kungwi wa mtaa...
 
Kwahiyo yeye lengo lake ni kuuwa mwizi au kuuwa mtoto wa mwenzie? Kama dhumuni lilikuwa ni kumshugulikia mhalifu, basi anapaswa afurahi...
 
Back
Top Bottom