Tujifunze Kutoka kwa Mafarao

BwanaSamaki012

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2023
Posts
212
Reaction score
250
Habari za jukumu wakuu

Ili nisiwachoshe naomba niandike kwa ufupi, hiki ambacho nimeona ni vyema kuwashirikisha

Kiasili asilimia 96% ya nchi ya Misri ni jangwa hali inayopelekea Misri kukumbwa na changamoto za kimazingira kama vile upungufu wa maji, ukame, joto kupita kiasi na changamoto nyingine nyingi za kimazingira

Pamoja na hayo yote bado kwa Africa, Misri ndio nchi ya kwanza Africa na ya sita duniani kwa uzalishaji wa samaki hasa wakufungwa ikizalisha 1.6 million tons of fish annually, wanaingiza zaidi ya USD 3.5 billion kwa mwaka, 80% ya wazalishaji wa samaki ni watu binafsi, sector hii imetengeneza ajila zaidi ya watu 300,000 nchini Misri

Tanzania imebarikiwa kuwa na vyazo vyingi sana vya maji, kuanzia maziwa makubwa, mito, mabwawa pamoja na bahari.

Lakini mbali na hivyo bado kwenye maeneo mengi wanaweza kuchimba visima na kupata maji yakutosha kutosheleza mahitaji ya jamii through out the year

Pamoja na yote bado hatu tumii ipasavyo rasilimali hii muhimu (maji) kwenye shughuli za kimaendeleo kama kilimo na ufugaji wa kisasa kama wanavyofanya Misri ambao rasilimali zao ni ndogo kuliko sisi

Naomba nijikite zaidi kwenye sector ya ufugaji samaki, ambayo kimsingi tumezidiwa mbali sana hata na majirani zetu Uganda

Mahitaji ya samaki nchini Tanzania ni makubwa ukilinganisha na upatikanaji wake hali inayopelekea bei ya samaki kupanda kila siku

Lakini kama tutatumia vizuri vyanzo vyetu vya maji ipasavyo kufuga samaki kama wanavyofanya Misri na Uganda tunaweza kujikwamua

Mfano kwa sasa hivi kilo moja ya samaki sato ni kati ya Tsh 10,000 hadi 13,000 kwa maeneo mengi nchini.

Ila kama utamua kuzalisha mwenyewe samaki na kisha kuuza au kutumia kama kitoweo gharama ya kuzalisha kilo moja ya samaki Sato kwa wastani ni itakuwa Tsh 5,000 tu

Hii ina include gharama za utengenezaji wa mazingira ya kufugia, vifaranga na gharama za uendeshaji wa mradi hadi kufikia mavuno.

Kama kuna uwepo wa maji wa kutosha kwenye mazingira yako unaweza kuanza kwa kufuga samaki wachache tu kwa ajili ya kitoweo, hii itakusaidia kupunguza unnecessary cost

Lakini pia kama kwenye mazingira yako unayo maji yakutosha na unamtaji unaweza kufanya ufugaji wa samaki kibishara kwa kufuga samaki wengi

Imagine unakuwa na kibwawa kidogo unafuga samaki wako, pembeni kuna kibustani ya mbogamboga au maua, unatumia maji ya bwawa la samaki kumwagilia bustani yako.

Hapa Kumbuka, maji toka kwenye bwawa la samaki yanakuwa na mbolea bustani yako itazidi kustawi maradufu, hii inakuwa ni advantage unapiga ndege wawili kwa jiwe moja

Usiwaze kuhusu wapi unaweza pata muongozo wa namna ya kufuga samaki kisasa au wapi utapata vifaranga, mimi niko hapa kukupa muongozo

Bei ya vifaranga ni Tsh 250 na ufugaji ni rahisi, kitu kizuri zaidi unachotakiwa kufahamu ufugaji wa samaki hauhusishi matumizi ya chanjo wala madawa ya kila mwezi, kazi yako inakuwa ni maintain ubora wa maji na kuwalisha samaki wako chakula kwa wakati. After 6 months you will see the results

Now is the time to utilize our resources more effectively. Let's begin by embracing the practice of eating what we cultivate.

Kwa jambo lolote kuhusu ufugaji samaki unaweza kunichech directly
Call/WhatsApp: +255758779170
bd59590e74584750b2d433bdebeca7f7.jpg
4695981b737841878f1b3ec0db587da5.jpg
0354cd96903f452eb4d4ddff248df8e5.jpg
f75b3c5b74184a6f929deecd73c34687.jpg
 
Unaweza tengeneza kama hivi bila kuchimba wala kujengea
 

Attachments

  • a07612ef4afe49dfa12f504d0733a69d.mp4
    2.1 MB
Mkuu tuombe afya tu nitakutafuta.

Swli langu lipo hivi ninavyoelewa mbolea za viwandani (NPK) sio salama sana kiafya vipi tena mnazitumia kwenye samaki?
 
Uko sahihi mkuu kuhusu mbole za viwandani, ila mimi hapo kwenye maelezo yangu nilikuwa nina maanisha organic manure
Sawa. Ikiwa natumia maji ya bomba nitaweza vipi kumwagilia bustani za mboga ili hali maji natakiwa kubadirisha kila baada ya muda kadhaa? gharama si itakuwa kubwa san?
 
Sawa. Ikiwa natumia maji ya bomba nitaweza vipi kumwagilia bustani za mboga ili hali maji natakiwa kubadirisha kila baada ya muda kadhaa? gharama si itakuwa kubwa san?
Sishauli utumie maji ya bomba kama unataka kufuga samaki kibiashara, unaweza kutumia maji ya bomba kama unafuga samaki wachache tu kwa ajili ya mapambo au matumizi ya familia

Lakini kama project yako ni ndogo unaweza afford, unajaza maji kwenye bwawa then unakuwa undischarged au unachota kwa ajili ya kumwagilia bustani then yakionekana kupungua unareplace yaliyopungua

Nikupe mfano, Kuna baadhi ya watu wanagarden nyumbani na wanatumia maji ya bomba moja kwa moja toka bombani kumwagilia lakini kama wakijaza maji kwenye bwawa watakalotumia kufugia samaki (liwe kama reserve tank) then kutokea hapo wakawa wanatumia kumwagilia unaweza one namna gani inakuwa ni advantage
 
Si shauli utumie maji ya bomba kama unataka kufuga samaki kibiashara, unaweza kutumia maji ya bomba kama unafuga samaki wachache tu kwa ajili ya mapambo au matumizi ya familia

Lakini kama project yako ni ndogo unaweza afford, unajaza maji kwenye bwawa then unakuwa undischarged au unachota kwa ajili ya kumwagilia bustani then yakionekana kupungua unareplace yaliyopungua

Nikupe mfano, Kuna baadhi ya watu wanagarden nyumbani na wanatumia maji ya bomba moja kwa moja toka bombani kumwagilia lakini kama wakijaza maji kwenye bwawa watakalotumia kufugia samaki (liwe kama reserve tank) then kutokea hapo wakawa wanatumia kumwagilia unaweza one namna gani inakuwa ni advantage
Naomba nisaidie mtaalamu.

Hivi Simtank unaweza kufugia samaki kwa matumizi ya nyumbani?

Mfano kama la ujazo wa lt2000, unadumbukizamo wangapi?

Naomba dondoo zako nipate mwanga kidogo ahsante.
 
Naomba nisaidie mtaalamu.

Hivi Simtank unaweza kufugia samaki kwa matumizi ya nyumbani?

Mfano kama la ujazo wa lt2000, unadumbukizamo wangapi?

Naomba dondoo zako nipate mwanga kidogo ahsante.
Kwenye simtank yenye ujazo wa lita 2,000 (2m²) napendekeza uweke samaki 20. Hii ni Kama hauna mechanisms yoyote ya kudhibiti ubora wa maji

Lakini kama unamechanism ya kudhibiti ubora wa maji au unauwezo wa kubadilisha maji wakati wowote yanapochafuka unaweza weka hadi samaki 100

Mechanisms za kudhibiti ubora wa maji ni bio-filters, ambayo utumika kuchuja taka (ammonia) na aerators hizi utumika kuongeza hewa ya ziada kwenye maji hasa nyakati za usiku
 
Back
Top Bottom