Bob Manson
JF-Expert Member
- May 16, 2021
- 4,158
- 7,787
Wakubwa shkamooni wadogo habari zenu.....
Tujifunze ku normalize kuwaambia watu kwamba wana tu inspire kwa matendo yao au style ya maisha yao, kuliko kujaribu kuwa kama wao na kuanzisha competition.
Binadamu hatupo sawa, kila mtu ana uwezo wake na umahiri wake katika jambo fulani, lakini vijana wengi wanapenda kufanya ushindani na marafiki zao kwasababu tu wamezidiwa kitu fulani.
Tunaishi katika dunia ambayo kupeana appreciation ni jambo adimu sana, sio rahisi kijana mwenzio kukuambia kwamba wewe ni hodari katika jambo fulani, yupo tayari aige na kufanya ushindani na wewe ilhali anajua hawezi kuwa kama wewe.
Mfano, Rafiki anajua kwamba una uwezo mkubwa wa kuchambua na kufahamu mambo mbalimbali, badala asikilize na kujifunza kupitia wewe, anataka naye aoneshe anajua na kusema kila mara, kumbe hajui kitu na anajidhalilisha kwa kusema asiyo yajua.
Umemfundisha na kumjuza mambo mengi, lakini akijua tu kwamba uwezo wako upo mbali sana, na yeye anataka wakati mpo pamoja awe anakufundisha na kukujuza mambo, na kiuhalisia hakuna cha maana anachosema ila anataka tu na wewe uone kama anajua.
Binafsi hali hii imenifanya nitengane na marafiki wengi sana, maana wengine wanafikia hatua ya kuanza chuki bila sababu za msingi. Ilifika wakati nikawa mpweke sana, ndipo nikajua kwamba nakosea kuwatenga bali napaswa kuishi nao kwa kuelewa kwamba wanakuwa inspired lakini hawawezi kusema.
Let's normalize telling people "you inspire me" instead of copying them and acting like they're your competition.