Tujifunze kwa Ramadhani Singano

Albinoomweusi

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
3,433
Reaction score
8,585
Anaandika @exaud_msaka_habari

Moja ya watu ambao tunaweza kuwatumia kama Mfano katika mijadala inayoendelea ni Fundi Ramadhani Singano

Moja ya Vijana wenye vipaji sana kuwahi kutokea Tanzania, ila ameishia kuwa mchezaji wa kawaida

Wafanyabiashara kwenye soka walimpotezea Dira sana walivyomtoa Simba kwa kigezo cha kufuata hela, ni kweli hela ni Muhimu ila kuna wakati kabla ya jela jenga kwanza ngome yako ambayo mbeleni itakupa hela unayoitaka mwenyewe

Yani leo Singano hata Timu ya Taifa haitwi, hayupo na hakuna anayemuulizia, uharaka wa maisha ulimpoteza kwenye soka letu

Wachezaji wetu nadhani wanatakiwa kuwa na watu sahihi sana wa kuwashauri vitu vya kufanya na wakati gani wafanye bila kuathiri vipaji vyao na Imani ya mashabiki

Sina maana wachezajo wasifuate hela, hayo ndio maisha yao ila wawe na uwezo wa kuona maisha baada ya kuweka hela mfukoni, na huo uwezo inabidi wawe nao wanaomzunguka, wakiwa na tamaa tu umekwisha

Meneja wa mchezaji anakuambia mimi hata akitokea Gwambina akaweka hela kubwa nauza mchezaji wangi Unajiuliza huyu amesema kweli au anatania

Unajiuliza huyu meneja hata anapataga nafasi ya kiwasiliana na mawakala wakubwa africa huko wamuuze mchezaji kwenye timu kubwa afrika au amekaa naye kama nyanya anasubiri yoyote aje na hela kubwa achukue?

Kuna wakati Heshima inaanza alafu hela inamwagika yenyewe tu,

ALL IN ALL TUSIWAPANGIE WACHEZAJI, TUWASHAURI
 
Labda kama Manager wa Tsabalala sio HENRY MZOZO, kila binadamu ana mapungufu yake lkn huyu tumpe HESHIMA yake ktk UVUMBUZI wa Vipaji! HENRY MZOZO ni Mtu wa Mpira kweli kweli! Anafanya kile wengi wasichoweza!

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Tumeona wanasema Shabalala anatakiwa yanga kapewa mkataba milioni 150 mara kuna timu tatu zinamhitaji afrika kusini, asichoelewa sasa hivi Simba ni miongoni mwa timu kubwa Afrika. Kwa nafasi yake nantimu ya Simba inavyocheza timu work anaweza kupotea jumla kwa sababu ya madalali
 

Kweli kabisa
 
Ni kawaida katika SOKA. UnaSHINE sehemu 1 unaenda kufeli sehemu ya 2!

JUAN SEBASTIAN VERON alifeli MAN U akaenda kukiwasha CHELSEA! THIERRY HENRY hakuwa na wakati mzuri JUVENTUS lakini ulizia balaa lake pale HIHJBURY na baadae EMIRATES! TORRES kakiwasha sana ATLETICO na LIVERPOOL lkn koote alikoenda baada ya LIVERPOOL alikuwa MZURURAJI tu!

SIMBA wana AJIB na GADIEL, wote kutoka YANGA! Hakuna cha maana wanachofanya pale kwa BANIANI! KELVIN YONDAN alitoka SIMBA wa Moto na akaenda kukiwasha YANGA!

MOGELLA! HAMIS GAGA! MRisho Ngassa! MWANAMTWA KIHWELU hawa waliwika SIMBA na YANGA kwa nyakati zao! Hussein Sharif "CASILLAS" alikiwasha sana MTIBWA SUGAR lkn alipokwenda SIMBA hamna alichofanya! SAID BAHAMUZI alikiwasha sana MTIBWA lkn kufika YANGA akaambulia patupu!

Juma Kaseja kakiwasha MAKONGO! Kakiwasha MORO UNITED! Kakiwasha SIMBA! Kila alipoenda anakiwasha! MANULA kakiwasha AZAM FC na bado anakiwasha SIMBA!

Kifupi sio sahihi kumlaumu SINGANO wala AJIB wala GADIEL wala DOMAYO... ni kawaida ktk soka kupanda na kushika! Ni kawaida ktk soka kuhama kutoka timu kwenda timu!

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Hatimae umefunga thread.

Singano alikosa kocha wa kumjua achezeshwe vipi..

Ndo maana Salah alishindwa Chelsea lakini ni big star Liverpool.

Kina Kluivert walishindwa AC Milan wakatamba kwingine.

Kina Kaka walivyotamba Milan wakashindwa kutamba Madrid...list ni ndefu.

Kanu alivyo onekana ndo basi tena Italia akaja kutamba Arsenal
 
Msimpangie mtu maisha, anayevuja jasho uwanjani ni yeye. Kwa sasa ndio umri sahihi wa kuvuna pesa, na eneo sahihi kwake ni pale mpunga ni mrefu zaidi.

Kuna club mchezaji anaweza kuvumilia kukaa kwa muda mrefu kidogo ili kuweka historia ya kubeba makombe makubwa ila kwa timu zetu za Tanzania bado sana kubeba makombe ya Afrika. Hivyo kubaki kwake Simba hakuna ulazima sana labda wamlipe vizuri.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Hahaha ana kwambia hapa kitaan kwangu hawajaja simba 😃😃 unajua hata gadiel michael wakat anaenda saini simba alimzimia simu meneja wake Jemedari kisha mchezaji akajiendea zake ku saini simba kimya kimya ...meneja akaja kuona picha tu mchezaj ka saini na mnyamaaa
Nimemsikiliza anayejiita meneja wa Mohamed Hussein Zimbwe,huyo jamaa ni kilaza na hata ulimwengu wa mpira wa leo umempiga chenga na hata thamani halisi ya mchezaji wake haijui kabisa.
 
Msimponze kijana. Umri unakwenda na nguvu zinapungua, ni mda wa kusaka kandarasi nene kwa masilahi ya familia yake. Hawezi kulipwa milioni 1.5 alafu chikwende alipwe 15 million.

Hivi kati ya wachezaji hao wawili nani anaisadia timu? Watanzania tuache unafiki, mashabiki hawajawahi kuridhika, dogo afikirie masilahi yake kwanza
 
Acha kudanganya watu Juan Sebastian Veron aliwasha Moto gani Chelsea?
 
Ila katika yote, naona wachezaji wengi waliotoka Simba kwa hii miaka ya karibuni na kuhamia Yanga walifanya mambo makubwa sana! Kuanzia Yondani, Amisi Tambwe, Ajib, Kessy, na wengineo wengi!

Ila walipotoka Yanga kwa mbwembwe na kuhamia/kurudi Simba, mambo yalikuwa tofauti kabisa! Mfano mzuri ni huyo Ajib na Gadiel Michael!
 
Heri zaidi ya ukorofi kwenye soka hana jipya yule
 
ningekuwa mimi naachana na meneja. jitu linaropoka tu linaweza kweli management. Atafute meneja timamu
 
ningekuwa mimi naachana na meneja. jitu linaropoka tu linaweza kweli management. Atafute meneja timamu
Wenzetu huko nje wameanza zamani haya masuala, unakuta Meneja mbali ya kusoma Sports Management lakini pia unakuta amesoma Sheria za Mikataba, Wengine wanaenda mbali zaidi wanasoma mpaka PR& Marketing, walau hata kama Ana watu wanamsaidia katika kusimamia wachezaji, lakini yeye mwenyewe anakuwa na basic knowledge, kwa hiyo with time Tutafika tu,

Mizozo kama hii ya kina Hery Mzozo nk inasaidia kujitizama sote na kuona upi ni mwelekeo sahihi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…