Albinoomweusi
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 3,433
- 8,585
Anaandika @exaud_msaka_habari
Moja ya watu ambao tunaweza kuwatumia kama Mfano katika mijadala inayoendelea ni Fundi Ramadhani Singano
Moja ya Vijana wenye vipaji sana kuwahi kutokea Tanzania, ila ameishia kuwa mchezaji wa kawaida
Wafanyabiashara kwenye soka walimpotezea Dira sana walivyomtoa Simba kwa kigezo cha kufuata hela, ni kweli hela ni Muhimu ila kuna wakati kabla ya jela jenga kwanza ngome yako ambayo mbeleni itakupa hela unayoitaka mwenyewe
Yani leo Singano hata Timu ya Taifa haitwi, hayupo na hakuna anayemuulizia, uharaka wa maisha ulimpoteza kwenye soka letu
Wachezaji wetu nadhani wanatakiwa kuwa na watu sahihi sana wa kuwashauri vitu vya kufanya na wakati gani wafanye bila kuathiri vipaji vyao na Imani ya mashabiki
Sina maana wachezajo wasifuate hela, hayo ndio maisha yao ila wawe na uwezo wa kuona maisha baada ya kuweka hela mfukoni, na huo uwezo inabidi wawe nao wanaomzunguka, wakiwa na tamaa tu umekwisha
Meneja wa mchezaji anakuambia mimi hata akitokea Gwambina akaweka hela kubwa nauza mchezaji wangi Unajiuliza huyu amesema kweli au anatania
Unajiuliza huyu meneja hata anapataga nafasi ya kiwasiliana na mawakala wakubwa africa huko wamuuze mchezaji kwenye timu kubwa afrika au amekaa naye kama nyanya anasubiri yoyote aje na hela kubwa achukue?
Kuna wakati Heshima inaanza alafu hela inamwagika yenyewe tu,
ALL IN ALL TUSIWAPANGIE WACHEZAJI, TUWASHAURI