Kweli hili jukwaa linastahili heshima kwasababu wengi pia tulipata msaada kutoka kwa watu tofaut tofaut ndani ya hili jukwaa, iweje leo hii tuligeuze sehemu ya Malumbano ya vyuo yasiyo na msingi.Umechaguliwa chuo kikubwa labda UDSM,SUA,MZUMBE n.k ni sawaa kwanini umdharau aliyechaguliwa TEKU,IFM,TIA,MUCCOBS..na unamdharau kwa misingi ipi? je hapo alipochaguliwa watu hawapati elimu bora? na je, kwan hcho chuo hakitambuliki na serikali ? Ama ,akisoma hapo ajira hatapata au? . na je? akisoma hapo hatohitimu ama!!
Umechaguliwa kwenye chuo kizuri sawa tunakubali chukua time yako kumshukuru Mungu kwa kuwa umepata Chuo na sio umuone mwngne hana maana kwan kwenye ajira pia anaeza kuwa Boss wako.
"we are intellectuals we should think twice"