Tujifunze maisha ya ndoa hapa

Tujifunze maisha ya ndoa hapa

gem platnumz

Member
Joined
Jun 7, 2021
Posts
12
Reaction score
10
Watu wengi leo tumebaki na tunajiuliza kwanini wimbi la kuvunjika kwa ndoa linakua kwa kasi sana mashauri Mahakamani kuhusu taraka yamekuwa Mengi kiasi kwamba yanataka kuzidi Mashauri ya kesi za Ardhi?

Siku moja alinifata ndugu mmoja akawa ananisimulia kisa chake mke wake amekuwa akimfumania akichat na boss wake juu kutaka kumuoa na amuache yeye huyo mwanamme na kumuahidi vitu vizuri na kwa maelezo ya yule ndugu mke wake atakuwa anatembea na boss wake sawa yote tisa anakumbuka alimusomesha Mpaka chuo kikuu alisumbuka kuuza yebo yebo juani kufukuzana na migambo wa jiji ili amsomeshe mke wake huyo.

Kisa hichi kilinikumbusha vitu vingi sana nikakumbuka nina karibia kesi saba za ndoa leo nauliza kwanini NDOA NYINGI ZA SIKU HIZI ZINAVUNJIKA?

img_4973-jpg.2484729
 
Sema mdada anaevaa kitenge Chake kwa heshima hivyo lazima mdumu
 
Ile thread ya kula tunda kimasihara, hata ambao hawajawahi kujaribu wataenda kujaribu.
 
Kwenye hizo kesi Saba ulizonazo major cause ya kuvunjika kwa ndoa ni nini ?
 
SEHEMU YA PILI( 2) YA THREAD HII YA KUHUSU MASWALA YA NDOA

Karibuni katika makala hii ya ndoa tena leo ningependa kuwaletea kisa cha pili cha ndg yangu ambae hakupenda litajwe hapa jina lake.

Alianza kunuiambia mwanzo ndoa yake ilikuwa kama ya Adam na Hawa kwenye bustani ya edeni alifurahi sana na alijihisi yeye ndo kama kazaliwa upya siku moja alikuja baba yake mzazi kumsalimia pale kwake kwa siku kadhaa kutokana na ugonjwa uliokuwa ukimsumbua baba yake hapo ndo mwanzo wa doa lilipoanza maana kila alipokuwa akirudi kutoka kazini alikuwa akimkuta baba yake ni mwingi mwenye huzuni kila alipokuwa akimuuliza shida nini baba yake alimuambia kuwa yupo sawa labda anakuwa na huzuni kutokana na maumivu ya ugonjwa tu ndo yanoyo sababisha anakuwa na huzuni.
Hivyo nilikuwa sitilii maanani nilikuwa najitahidi kuacha huduma zote kwakua nilishajua mzee anapitia maumivu ya ugonjwa ilinipasa nitafte msaidizi wa kiume pale nyumbani japo mwanzo mke wangu alikataa kwakuwa alikuwepo tu nyumbani ila nilimuondoa hofu kwakusema sasa kuna vitu baba atahitajikufanyiwa na yeye ni wa kike asingeweza kuvifanya alinikubalia nikamleta houseboy nyumbani
Baada ya wiki mbili tangu nilimlete msaidi wa kiume ambae nililetewa na rafiki yake mke wangu nilipokea simu kutoka kwa rafiki yake mke wangu akitaka tuonane kuna kitu alihitaji kuniambia litu cha mhimu hivyo ilibidi nimuambie aandae eneo tulivu nakuja maeneo atakayo andaa kweli alinitumia text na kunielekeza mida ya chakula cha mchana nilifika maeneo aliyonielekeza tukasalimia alianza kwanza kwa kunipa pole nikamshangaa maana mimi sina taarifa zozote mbaya taratibu aliaanza kuniambia mambo alikuwa anamfanyia baba yangu mzazi kwanza kwa kumnyima chakula pili kumuacha kwa mchana mzima na kutokomea anakojua yeye nilipata mshutko kidogo ikabidi niamkee haraka nakuwahi nyumbani kweli nilimkuta baba na house boy wangu baba alikuwa anakula na msaidi wa nyumba yule wa kiume ikabidi nikae nijiunge nao kula nikauliza mke wangu katoka wakasema katoka mda si mrefu kishingo upande nikaomba kuwaaga ila mzee aliniita na kuniomba nimpeleke akalale nilimpeleka katika chumba chake alihisihi nikae kidgo nikaa akaniambie na yeye pole mwanangu kwa ndoa yako nikamuuliza kwanini ananipa pole ilihali mimi na mke wangu hatuna tatizo lolote akanijibu mwanangu kabla ya kujibu tafakari ebu wiki moja ifanye kuwa wiki yenye kuujua ukweli juu ya mke wako


ITAENDELEA............
 
Kijana kataa ndoa , ndoa ni utapeli, ndoa ni wizi tumeibiwa mno , kataaa ndoa afya yako ya akili ni muhimu kuliko ndoa.
 
Back
Top Bottom