Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Kenya pamoja na kuwa na katiba mpya ila inaonekana bado kuna mambo hayakuwekwa sawa katika katiba hiyo.
Mambo kadhaa bado hayajaweza kupatiwa ufumbuzi kupitia katiba yao mpya hayo ni pamoja na;
1.Ubadhirifu mkubwa wa pesa za umma,
Nchini Kenya pesa za walipakodi bado zinafanyiwa ufisadi mkubwa sana kama sehemu nyingine za Africa kupitia miradi na tenda mbalimbali kubwa na hakuna uwajibikaji kabisa katika hili. Katiba yao haijaweza kutibu jambo ubadhirifu na ufisadi.
2.Mamlaka ya Urais bado haikuwekewa vizingiziti vya kutosha "checks and balances.
Tangu ameingia madarakani Rais Ruto amefanya mambo yanoyothibitisha hilo.
Amewafukuza kazi wakuu wa mashirika na wenyeviti wengi wa bodi za mashirika ya umma ambao waliteuliwa na mtangulizi wake Rais Uhuru,Kenyatta na anatuhimiwa kuwaweka "loyalists" wake katika nafasi hizo na nyingine nyingi hasa kutoka kabila lake la Kalenjin, hii sio afya kwa mshikamano wa nchi.
Yeye na makamu wake wamemuandama sana hadharani mtangulizi wake Kenyatta na familia yake kuhusu masuala ya kodi. Hii sio sawa, hayo mambo yalifapaswa kushughulikiwa na taasisi husika.
3.Uhamaji wa vyama kiholela kwa viongozi waliochagulia, muda mfupi baada ya Ruto kuchaguliwa wabunge wengi wa Azimio la Umoja walitimkia kwenye kambi ya Ruto, kuna tuhuma kwamba kuna biashara ya manunuzi ilifanyika na inaendelea kufanyika.
Siku tutakapoamua na kukubaliana kuwa na katiba mpya katika taifa hili ni vizuri turejee na tujifunze kutoka kwa hawa majirani zetu ambao tumekuwa tukiisifia sana katiba yao.