Sijali
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 2,672
- 1,814
Mwaka 1990, nusu ya raia wa Vietnam walikuwa fukara wa kutupwa zaidi yetu, wakiishi kwa nusu dola kwa siku! Leo, Vietnam kuanzia 2020 imefuta ufukara kabisa!
China, katika uhai wangu, miaka ya 60,70 ilikuwa nyuma kwa maisha ya mtu binafsi hata kuliko Tanzania! Leo, China ni ya kwanza duniani katika kila nyanja isipokuwa chache tu, na ni miaka kumi tu ijayo itaipiku Marekani.
Na ndiyo hivyo, ukitazama nchi nyingi Asia, kama India, Indonesia, Philipino nk stori ni hiyo hiyo. Ni dhahiri kabisa, uongozi wa dunia wa kiuchumi, kisiasa na kielimu utakuwa Asia. Time Magazine limekwisha tabiri kwamba kufikia mwaka 2030 asilimia 90 ya PHD za sayansi na teknolojia watakuwa Waasia!
Kwa upande mwingine, bara la Ulaya linakufa kiuchumi, kisiasa na hata kiutamaduni. Ni suala la muda tu kabla halijachukua nafasi ya tatu baada ya Asia na Amerika.
Ungedhania kuwa wataalamu wetu wa siasa wangejipanga kuanzia sasa kuelekea zaidi Asia, kama patna wa maendeleo. La hasha! Bado hawajang'amua 'transformation' hii kubwa ijayo na bado wanajikombakomba kwa Wazungu, wakiamini kuwa wanaendelea kuwa mabwana wa dunia!