Tujifunze na kuiga kutoka Asia, tuachane na kasumba ya kujikomba kwa Wazungu

Ni kweli
Lakini Asia pia ina man power yakutosha.......ina zaidi ya watu billion 4
Wanajitosheleza kwa mengi tu
 
Serikali Kazi yake hasa ni nini ? Je wakulima wanapewa ruzuku au vyama vya siasa ndivyo vinavyopewa ruzuku ?!!! Je serikali kwa kujua asilimia kubwa ya wananchi wake wanategemea kilimo je ni mipango gani inafanywa baada ya miaka 60 ya uhuru ili tusiwe tunategemea mvua katika kilimo chetu ?maana hali ya ukame na mvua zisizotabirika imekuwa ni janga kwa Nchi yetu !!? Au ni vyema watu wote tuwe ni watu wa kupiga madili ili tutajirike individualy kama ulivyoshauri ?!! ALIYESHIBA huwa hamjui mwenye njaa. !!
 

Mpaka tutakapojitambua, ndipo tutakapotoka kwenye hili lindi la umasikini. Inasikitisha sana kuona Afrika bado ina imani kubwa sana kwamba bila nchi za magharibi, hatuwezi kufanya lolote. Tumepumbazwa akili, tunaona kila kitu kutoka magharibi ni bora.
Mfano wanasema nchi zote zilizokuwa makoloni ya ufaransa bado hazina uhuru kiuchumi. Zinanyonywa waziwazi na ufaransa. Lakini hilo, halijawahi hata siku moja kuelezea namna zinavyonyonywa, lkn pia namna ya kujitoa na unyonyaji huo.

Kuhusu kuiga nchi za Asia, huo ndiyo uwe muelekeo wa Afrika. Tukajifunze wenzetu wamefanya nini, nasi tunapaswa kufanya nini kutokana na mazingira yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…